Uchaguzi 2020 Baada ya Membe na Maalim Sharif kujiandaa na Uchaguzi Mkuu, Msajili aibuka atia nia ya kukifutia usajili ACT Wazalendo

Taharuki mpya imeibuka ndani ya chama cha ACT Wazalendo baada ya uwepo kwa uwezekano mkubwa wa chama hicho kufutwa na msajili wa vyama vya siasa.





Mpaka tufike Oktoba kuna mengi na kinachopangwa ni Magufuli kupita bila mpinzani

Ila patawaka moto!
 
Jana aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe alitangaza rasmi kujiunga na chama cha ACT Wazalendo

Mchakato wa Membe ulianza zaidi ya miezi minne iliyopita huku serikali ikifuatilia kwa karibu

Baada ya hivi karibuni kujiridhisha kwamba atajiunga na kuna uwezekano vyama pinzani vikamsimamisha kuwa mgombea wao,serikali kupitia ofisi ya msajili ikaibuka na kituko cha mwaka kwa kuwaandikia ACT barua ya kuwajulisha nia ya kuwaadhibu

Miongoni mwa sababu zilizotajwa kwamba ni za kutoa adhabu ni pamoja na chama hicho kuwahimiza wananchi kusimamia haki yao,kuitaka tume ya uchaguzi na vyombo vya dola kutenda haki ili uchaguzi uishe kwa amani na salama

Tayari Mutungi na timu yake kwa sasa wako katika hatua ya mwisho ya kutangaza adhabu hiyo kwa lengo la kuhakikisha CCM haipati upinzani unaostahili
 
Kuna watu wanawaombea wenzao wafe au wafiwe yaani utadhani wao hawajui maumivu yake kama wakigeuziwa upande wao.

Hivi yule Jecha kitendo tu cha kutoingia 5 bora unadhani amefurahia&kuridhishwa na matokeo yale?
 
Zitto ni strategist kama mwandishi Robert Greene. I wish baada ya uchaguzi aandike kitabu chake tujifunze mengi.

Kitendo cha Nec kutapata sababu ya mikakati ya chama chake ni wazi kwamba moto umekolea. Wapinzani mkiungana hakika mtakuwa mmewapiga CCM comeback ya kufa mtu kama ile ya Liverpool vs Barcelona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…