Uchaguzi 2020 Baada ya Membe na Maalim Sharif kujiandaa na Uchaguzi Mkuu, Msajili aibuka atia nia ya kukifutia usajili ACT Wazalendo

Hakuna kosa lolote lenye msingi wa kisheria ambao ACT wamevunja na hata kama lingekuwepo bado asingeweza kukifuta maana sheria inasema msajili hawezi kufuta chama kama imebakia chini ya miezi 12 kabla ya uchaguzi na sasa imebakia kama miezi mi3,kwahiyo msajili atasubiri sana!!
Nyie jidanganyeni, kitawekewa 'sanction' mpaka akili iwarudie! Kwangu Mimi hiyo Sheria ya kutokifuta mwaka mmoja wa uchaguzi inaweza Kuwa overruled kwa maslahi ya taifa!
 
Msajili kilaza kweli, anadai eti katibu mkuu wa ACT ndugu Ado Shaibu ajieleze kwa nini katumia maneno ya "Uchaguzi huu ni uchaguzi wa kufa na kupona".
Amesahau Nyerere mwenyewe alikiita Kilimo cha "Kufa na kupona". Hiyo ni nahau tu, ni kiswahili cha kawaida. Ni msemo wenye maana ya "Juhudi kubwa", "Ushindani mkubwa" au kwa kimombo "very serious".

Msajili aache kutumikia CCM, atumikie nchi kwa mujibu wa sheria!
Wewe akili zako hazina akili, hapa tunaangalia context ya kauli! Huyu anataka kuvuluga amani kwa umbulula wake...nimuombe msajili asiangalie Julia Wala kushoto akifutilie mbali hicho chama Cha kigaidi!
 
Nyie jidanganyeni, kitawekewa 'sanction' mpaka akili iwarudie! Kwangu Mimi hiyo Sheria ya kutokifuta mwaka mmoja wa uchaguzi inaweza Kuwa overruled kwa maslahi ya taifa!
Maslai ya taifa??? Kwani ACT imefanya uhaini? Yaani Membe na Maalim kujiunga ACT ndio uhaini?
 
Jana aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe alitangaza rasmi kujiunga na chama cha ACT Wazalendo

Mchakato wa Membe ulianza zaidi ya miezi minne iliyopita huku serikali ikifuatilia kwa karibu

Baada ya hivi karibuni kujiridhisha kwamba atajiunga na kuna uwezekano vyama pinzani vikamsimamisha kuwa mgombea wao,serikali kupitia ofisi ya msajili ikaibuka na kituko cha mwaka kwa kuwaandikia ACT barua ya kuwajulisha nia ya kuwaadhibu

Miongoni mwa sababu zilizotajwa kwamba ni za kutoa adhabu ni pamoja na chama hicho kuwahimiza wananchi kusimamia haki yao,kuitaka tume ya uchaguzi na vyombo vya dola kutenda haki ili uchaguzi uishe kwa amani na salama

Tayari Mutungi na timu yake kwa sasa wako katika hatua ya mwisho ya kutangaza adhabu hiyo kwa lengo la kuhakikisha CCM haipati upinzani unaostahili
Kama vip kifutwe tu
 
Wewe akili zako hazina akili, hapa tunaangalia context ya kauli! Huyu anataka kuvuluga amani kwa umbulula wake...nimuombe msajili asiangalie Julia Wala kushoto akifutilie mbali hicho chama Cha kigaidi!

Tukisema Msajili na NEC sio huru, hii ndio maana yake. Msajili kuona msemo wa “kufa na kupona” katika lenzi za CCM. Neno “amani ya nchi” limetumika vibaya sana kuanzia maRC na maDC kuweka watu ndani masaa 48 bila kwenda mahakamani halafu ghafla hakuwa uvunjifu wa amani umeweza kuthibitishwa.

Simple. Kama maneno hayo ni uchochezi, kuna sheria za uchochezi na Shaibu akamatwe na kushtakiwa. Haiwezekani kuwa na msajili anayetaka kuwa na uelewa binafsi wa alichosikia na kutaka kunyang’anya haki za kikatiba za raia bila kuthibitisha kosa!!

Je CCM ifutwe na msajili kwa sababu wanachama wake wanakamatwa na TAKURURU kuhusu rushwa???
 
Uko nje ya mantiki! Hebu fuatilia hiyo barua vizuri, pia fuatilia YouTube ili ujue Kama hayo yaliyosema na kufanywa na hao viongozi yanaliacha taifa letu salama Kama yakitekelezwa na wanaowahubiria kuyatekeleza! Acha mihemko, Mimi ninayo Tz tu, hao wenye raia pacha wasituvuluge! Msajiri yupo sahihi kuwashikilia kooni wapuuzi wanaoweza fikiri kuropoka chochote kwa maslahi yao...badala ya kuelezea sera zao wanahamasisha uvunjifu wa Sheria na amani! Huu ni upuuzi kabisa hasa kwa kutolewa na viongozi waandamizi wa chama Cha siasa!
 
Sasa sina wasiwasi na kiwango chako cha upembuzi wa mambo. Hasa uliposema niko nje ya mada - umefanya hivo kwa sababu hujiruhusu kuwaza sio tu nje ya box bali mbali kabisa nje ya boksi.

Nitarudia!! Msajili hapaswi kuadhibu chama cha siasa kwa fikra au hisia BALI kwa sheria!! Na kama kuna sheria zimevunjwa - zitumiwe hizo lakini sheria inatafsirika mahakamani tu. Msajili kupitia jamhuri amshitaki Shaibu na akitiwa hatiani aadhibiwe! Unataka afute taasisi ya umma kwa kosa la mtu mmoja?? Mangula alinyweshwa sumu - unadhani ni sahihi kusema CCM ni chama cha mauaji??? Najua utasema hizo si habari za kweli na hazijathibitishwa. Na hapa ndio point yangu - kuna sehemu mambo haya hushughulikiwa kwa kupitia sheria!!!
 
Taharuki mpya imeibuka ndani ya chama cha ACT Wazalendo baada ya uwepo kwa uwezekano mkubwa wa chama hicho kufutwa na msajili wa vyama vya siasa.

View attachment 1509112

Mpaka tufike Oktoba kuna mengi na kinachopangwa ni Magufuli kupita bila mpinzani

Ila patawaka moto!

Moto utawaka ACT mkuu.
Wa tz hatuna ujinga huo
 
Sasa sina wasiwasi na kiwango chako cha upembuzi wa mambo. Hasa uliposema niko nje ya mada - umefanya hivo kwa sababu hujiruhusu kuwaza sio tu nje ya box bali mbali kabisa nje ya boksi.

Nitarudia!! Msajili hapaswi kuadhibu chama cha siasa kwa fikra au hisia BALI kwa sheria!! Na kama kuna sheria zimevunjwa - zitumiwe hizo lakini sheria inatafsirika mahakamani tu. Msajili kupitia jamhuri amshitaki Shaibu na akitiwa hatiani aadhibiwe! Unataka afute taasisi ya umma kwa kosa la mtu mmoja?? Mangula alinyweshwa sumu - unadhani ni sahihi kusema CCM ni chama cha mauaji??? Najua utasema hizo si habari za kweli na hazijathibitishwa. Na hapa ndio point yangu - kuna sehemu mambo haya hushughulikiwa kwa kupitia sheria!!!

Sheria ipi tofauti na sheria ya vyama vya siasa unayoitaka wewe msajiri aitumie tofauti na alivyoeleza ktk barua zake.
Kazi ya msajiri nikusimamia sheria na kuchukua hatua.
Act wameonywa mara-nyingi kama barua zilivyorekodiwa hapo

Kwakuwa wameshindwa kujirekebisha hatua ya mwisho nikukifuta chama.

Wasipolidhika , basi wao ACT ndo waende mahakamani.

Ova.
 
18 Julai 2020
Mapya yaibuka sakata la ACT Wazalendo na Msajili vyama vya siasa

Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Bw. Addo Shaibu azungumzia barua ya Msajili wa Vyama Vya Siasa iliyobeba ujumbe wa kusudio la kuchukua hatua dhidi ya ACT-Wazalendo kutokana na alichokiita Msajili wa Vyama kuhusu kujirudia kwa matamshi ktk shughuli zake za kujiendesha kisiasa.

Msajili hawezi kisheria kufuta chama kinachoelekea kushiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika ndani ya miezi 12 (ulio mbele yake ). Msajili anadai anaweza kutoa onyo, faini au kufuta usajili. Kauli hizi mbili kati ya ACT -Wazalendo na Msajili wa Vyama zinapishana ktk tafsiri ya kisheria kuhusu adabu kipindi hiki kuelekea Uchaguzi Mkuu wacOktoba 2020.

Hilo limeanza kuleta dukuduku upande wa wanachama wa ACT- Wazalendo na kambi nzima ya vyama vya upinzani Tanzania.
Source : ITV Tanzania
 
Msajili tupa barua nyengine kwa ccm kwa kutamka mapinduzi daima huku Zanzibar, maana ya mapinduzi daima ni kuchochea uvunjifu wa amani, kuchochea mauwaji ya 1964.

Unaposema utalinda mapinduzi ya Zanzibar kwa maana utalinda ccm juu ya mapinduzi kuuuwa au nyenginevyo alimuradi ushindi ccm ikae madarakani.

Msajili wa vyama vya siasa ni double standard. Mnafiki mkubwa
 
Tukisema Msajili na NEC sio huru, hii ndio maana yake. Msajili kuona msemo wa “kufa na kupona” katika lenzi za CCM. Neno “amani ya nchi” limetumika vibaya sana kuanzia maRC na maDC kuweka watu ndani masaa 48 bila kwenda mahakamani halafu ghafla hakuwa uvunjifu wa amani umeweza kuthibitishwa.

Simple. Kama maneno hayo ni uchochezi, kuna sheria za uchochezi na Shaibu akamatwe na kushtakiwa. Haiwezekani kuwa na msajili anayetaka kuwa na uelewa binafsi wa alichosikia na kutaka kunyang’anya haki za kikatiba za raia bila kuthibitisha kosa!!

Je CCM ifutwe na msajili kwa sababu wanachama wake wanakamatwa na TAKURURU kuhusu rushwa???

Pale wagombea wa ccm wanapo apa kulinda mapinduzi ya Zanzibar na mapinduzi daima inamaantiki gani mkuu kwa usalama wa Zanzibar? Maana yake yake wako tayari kwa lolote ccm ikae madarakani hata kwa kura moja.

Msajili hajalima hata barua moja kwa ccm, ni unafiki na double standard
 
Sasa sina wasiwasi na kiwango chako cha upembuzi wa mambo. Hasa uliposema niko nje ya mada - umefanya hivo kwa sababu hujiruhusu kuwaza sio tu nje ya box bali mbali kabisa nje ya boksi.

Nitarudia!! Msajili hapaswi kuadhibu chama cha siasa kwa fikra au hisia BALI kwa sheria!! Na kama kuna sheria zimevunjwa - zitumiwe hizo lakini sheria inatafsirika mahakamani tu. Msajili kupitia jamhuri amshitaki Shaibu na akitiwa hatiani aadhibiwe! Unataka afute taasisi ya umma kwa kosa la mtu mmoja?? Mangula alinyweshwa sumu - unadhani ni sahihi kusema CCM ni chama cha mauaji??? Najua utasema hizo si habari za kweli na hazijathibitishwa. Na hapa ndio point yangu - kuna sehemu mambo haya hushughulikiwa kwa kupitia sheria!!!
Ndugu tunayo nchi moja iitwayo Tz, na Kama kikundi Cha watu waliojipenyeza Kama chama Cha siasa na kwa kuvimbiwa amani yetu wakaanza kuleta viashilia vya kutengeneza nyufa, ni wajibu wa mamlaka husika zilizokasimiwa mafaraka ku'monitor' kikundi husika kuingilia Kati haraka iwezekanavyo! Hatuwezi subiri mpaka waingie mtaani na kuleta machafuki wakati tunaweza kuling'oa gugu wakati bado kusambaa na kujomaa! Msajiri akifanyacho ni Cha kizalendo! Kama chama Cha ACT kinaongozwa na top leya yenye malengo wa kuivunja amani ya Tz, dawa ni kukifuta hata Kama tayari vote ballots zimeshatengenezwa! Hii ni kutokana na umuhimu wa amani yetu...of course kwa uelewa na uwezo wakona muono wako finyu huwezi kuelekea na utaishia kumuita majina yote yatakayokuja kwenye ufinyu wa akili zako! Lakini tunaoona mbali huwa tunaziba ufa kuepuka kujenga jengo lote baadae!
Nasisitiza Tena, maamuzi ya msajiri ya kukichukulia hatua stahiki chama Cha ACT wazandiki nayaunga mkono kwa asilimia zote ili liwe fundisho kwa wote wsnaotumika na wasiotutakia mema Tz! Mungu azidi ibariki Tz!
 
Msajili tupa barua nyengine kwa ccm kwa kutamka mapinduzi daima huku Zanzibar, maana ya mapinduzi daima ni kuchochea uvunjifu wa amani, kuchochea mauwaji ya 1964.

Unaposema utalinda mapinduzi ya Zanzibar kwa maana utalinda ccm juu ya mapinduzi kuuuwa au nyenginevyo alimuradi ushindi ccm ikae madarakani.

Msajili wa vyama vya siasa ni double standard. Mnafiki mkubwa
Acha kuleta mzaha kwenye Mambo yaliyo serious!
 
Back
Top Bottom