Uchaguzi 2020 Baada ya Membe na Maalim Sharif kujiandaa na Uchaguzi Mkuu, Msajili aibuka atia nia ya kukifutia usajili ACT Wazalendo

Uchaguzi 2020 Baada ya Membe na Maalim Sharif kujiandaa na Uchaguzi Mkuu, Msajili aibuka atia nia ya kukifutia usajili ACT Wazalendo

Naona michezo ya kikachero imeanza,Hio ni Zuga tu ili ionekane ACT nao wanapitia Magumu kama ya Chadema.

HAKUNA HATUA ZOZOTE ZITACHUKULIWA DHIDI YA ACT.
Tulishawastukia kitambo, hilo ni tawi kamili la ccm.
 
Kumbe hizi znazoitwa sheria zina makengeza sio?
TUIACHE SHERIA IFUATE MKONDO WAKE kwa kuzingatia kuwa hakuna aliye juu ya sheria na kwamba Tanzania ndiyo nyumbani. Hakuna kwengine kwa kukimbilia iwapo timbwili la kujitakia likiibuliwa na wanasiasa wachache wachumia matumbo.
 
mara kwa mara vyama vya upinzani vinapofanya makosa havitaki kukirri huwa wanaitupia lawama serikali na kutegemea hma ya wananchi,

Malengo yao siku zote ni kutaka kuonekana wanaonewa tu hata katika mambo ambayo yapo ndani ya uwezo wao kutoyafanya,
 
Mimi naona CCM kama chama Cha siasa imeishiwa pumzi.Sasa inatumia matawi yake ya pembeni,kama vyombo vya dola na tume ya uchaguzi kupambana!
 
Wale wanaoshusha na kuondoka na bendera za CHADEMA wanakua hawajafanya kosa kisheria?Au kwakuwa ni CCM basi sio kosa?
 
Isije ikawa huyu msajili anafanya haya wakati familia yake keshaiondoa nchini! Anachotaka kukifanya hata mtoto mdogo wa std1 anaijuwa athari yake, halina utetezi atakaoweza kuja nao.
 
Hebu Fikiria yule kiongozi wa umoja wa vijana wa CCM akihimiza kuwapiga wapinzani. Lakini kwenye hayo huwezi kumuona msajili akisema kitu.
Kuna mmoja alikuwa Iringa kahongwa u DC wa Arusha Kama fadhila baada ya kuwatishia kuwauwa Zitto na Mbowe
 
Taharuki mpya imeibuka ndani ya chama cha ACT Wazalendo baada ya uwepo kwa uwezekano mkubwa wa chama hicho kufutwa na msajili wa vyama vya siasa.

View attachment 1509112



Mpaka tufike Oktoba kuna mengi na kinachopangwa ni Magufuli kupita bila mpinzani

Ila patawaka moto!
Hajawahi shinda chochote bila kubebwa maishani, hawezi ushindani
 
Waliozoea kuongoza wanyama katu hawawezi ongoza watu wakapumzike October Hawa
 
Duh, yaani huoni makosa kweli au kipofu wa akili! Huyu msajiri mbona anapodoapodoa Sana!? Hebu kifutilie mbali ili liwe fundisho kwa kanjanja wote na ukuwadi wao kwa mabeberu! Wengine tunayo nchi hii tu ya Tz! Hawa wenye urais wa DRC, Oman, na Canada wasituvuluge Bali tuwAvuluge wa
Hakuna kosa lolote lenye msingi wa kisheria ambao ACT wamevunja na hata kama lingekuwepo bado asingeweza kukifuta maana sheria inasema msajili hawezi kufuta chama kama imebakia chini ya miezi 12 kabla ya uchaguzi na sasa imebakia kama miezi mi3,kwahiyo msajili atasubiri sana!!
 
Msajili kilaza kweli, anadai eti katibu mkuu wa ACT ndugu Ado Shaibu ajieleze kwa nini katumia maneno ya "Uchaguzi huu ni uchaguzi wa kufa na kupona".
Amesahau Nyerere mwenyewe alikiita Kilimo cha "Kufa na kupona". Hiyo ni nahau tu, ni kiswahili cha kawaida. Ni msemo wenye maana ya "Juhudi kubwa", "Ushindani mkubwa" au kwa kimombo "very serious".

Msajili aache kutumikia CCM, atumikie nchi kwa mujibu wa sheria!
 
Back
Top Bottom