Baada ya Miaka 16 Leeds United yarejea tena Ligi Kuu Uingereza

Baada ya Miaka 16 Leeds United yarejea tena Ligi Kuu Uingereza

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Klabu ya Leeds United inatajwa kuwa na uhasimu mkubwa na vilabu vya Jiji la London vikiongozwa na Chelsea FC

EdMcSg8WsAEuIL_.jpeg

Leeds United wamefanikiwa kurejea EPL baada ya kuinyuka 1-0 dhidi ya Barnsley katika Uwanja wa Elland Road

Washindani wao wa karibu West Bromwich Albion walipaswa kushinda dhidi ya Huddersfield Town siku ya jana (Ijumaa) lakini West Bromwich walifungwa

Leeds United wanarejea baada ya kucheza madaraja ya chini kwa miaka 16 baada ya kushuka daraja mwaka 2004

Kocha Marcelo Bielsa ameiongoza Leeds United katika kampeni ya kusaka tiketi ya kurejea Ligi Kuu na kufanikiwa kufikisha alama 87 huku akiwa na michezo miwili mkononi
 
Haha ,

Alan Smith akaja nunuliwa na Furgeson Man U, kwa Bei kuubwa akaja flop hakuwika Sana Man U.
Ukawa usajili mzuri uliogeuka mbovu ghafla. Niliamini ni bonge la usajili kumbe kuna watu wamezaliwa kuwa walimu, ukiwabadilisha kuwa Wachungaji wanakula hadi Kondoo wakati wakiwa Walimu hawajawahi hata kutamani mwanafunzi.
 
Leeds wako makini kocha waliyenaye ni wan daraja la juu ana.historia kubwa anajua.anataka wachezaji wa aina gani pia ni mzoefu wa kucheza mechi kubwa wanaoikumbuka atletco bilibao ya kina Martnez anayechezea bayern iliyomfanya man u ya Ferguson kama Simba ilivyomfanya utopolo
 
Hongera Leeds united. Italeta ushindani EPL haswa kwa vilabu vikubwa
 
Itoshe kusema Leeds United karibuni English Premier League 2020/21
 
Klabu ya Leeds United inatajwa kuwa na uhasimu mkubwa na vilabu vya Jiji la London vikiongozwa na Chelsea FC

View attachment 1510089

Leeds United wamefanikiwa kurejea EPL baada ya kuinyuka 1-0 dhidi ya Barnsley katika Uwanja wa Elland Road

Washindani wao wa karibu West Bromwich Albion walipaswa kushinda dhidi ya Huddersfield Town siku ya jana (Ijumaa) lakini West Bromwich walifungwa

Leeds United wanarejea baada ya kucheza madaraja ya chini kwa miaka 16 baada ya kushuka daraja mwaka 2004

Kocha Marcelo Bielsa ameiongoza Leeds United katika kampeni ya kusaka tiketi ya kurejea Ligi Kuu na kufanikiwa kufikisha alama 87 huku akiwa na michezo miwili mkononi
Hawa ni Norwich tu wamekuja kutalii hamna kitu kabisa [emoji57][emoji57]
 
Sisi mashabiki tuliokua leeds United tukaamia chelsea ..turudi leeds?
 
Back
Top Bottom