Baada ya miaka 39, Taifa Stars yafuzu kucheza michuano ya AFCON 2019 baada ya uicharaza Uganda goli 3-0, Uwanja wa Taifa-Dar

Baada ya miaka 39, Taifa Stars yafuzu kucheza michuano ya AFCON 2019 baada ya uicharaza Uganda goli 3-0, Uwanja wa Taifa-Dar

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Timu ya Taifa ya Tanzania(Taifa Stars) leo majira ya saa 12:00 jioni katika Uwanja wa Taifa uliopo jijini Dar inacheza na timu ya Taifa ya Uganda(The Cranes) katika mchezo wa kufuzu kucheza Michuano ya Mataifa ya Afrika(AFCON) nchini Misri

Lesotho yenye alama sawa na Tanzania itakuwa ugenini inamenyana na Cape Verde.

1553435574544.jpg
Msimamo wa Kundi ulivyo kabla ya Mechi za mwisho leo

Taifa Stars ili kufuzu AFCON pia inategemea na matokeo ya Lesotho ambapo iwapo Lesotho. Taifa Stars itafuzu iwapo itashinda dhidi ya Uganda na Lesotho atoke droo au afungwe na Cape Verde

Lakini iwapo Taifa Stars na Lesotho zote zitashinda badi Stars inabidi ishinde magoli mengi na kukaa juu ya Lesotho kwenye msimamo wa kundi kwa tofauti ya magoli ya kufungwa na kufunga

UPDATES:
Mashabiki wamevunja geti upande uwanja wa Uhuru na NBSP kuingia kwa nguvu kwenye Uwanja wa Taifa kushuhudia mechi ya Taifa Stars na Uganda.

Nguvu ya mashabiki imewashinda polisi na walinzi wengine na kulivunja geti hilo saa 10.33 jioni hali iliyowalazimu polisi kujipanga upya kuzuia hali hilo.

Katika kipindi cha takribani dakika tano kabla ya polisi kuzuia mashabiki wengi tayari walikuwa wameingia na kwenda moja kwa moja jukwaani
***

IMG_20190324_173137.jpg

Mashabiki kutoka sehemu mbalimbali awanaendelea kuingia uwanja
***

Polisi imewatawanya kwa mabomu ya machozi mashabiki waliotaka kuingia uwanjani kwa kupitia uwanja wa Uhuru katika mechi ya Taifa Stars na Uganda, kutokana na msongamano uliopo kwenye mageti ya Uwanja wa Taifa
***

IMG_20190324_180646.jpg
Vikosi vinavyoanza mchezo wa leo
***


Taifa Stars inapata goli la kuongoza dhidi ya Uganda goli lililofungwa dakika ya 21 na Saimon Msuva. Msuva alipokea pasi safi kutoka kwa John Bocco 'Adebayor'

Aidha, katika mchezo mwingine matokeo katika mchezo wa Lesotho na Cape Verde bado ni 0-0
1553441964308.jpg
***

MAPUMZIKO: Taifa Stairs inaenda mapumziko ikiwa inaogoza kwa goli 1-0 dhidi ya Uganda. Katika mchezo wa Lesotho na Cape Verde milango bado ni migumu

1553443106643.jpg
Stats zilivyo hadi Mapumziko
***


Taifa Stars inapata bao la pili kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Erasto Nyoni baada ya beki wa Uganda kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari dakika ya 51.

1553444604634.jpg
***

Goli la tatu kwa Tanzania kutoka kwa beki Aggrey Morris akimalizia kwa kichwa pasi ya John Bocco dakika ya 57

1553445060107.jpg
***

FULL - TIME
1553447053153.jpg

1553447442390.jpg
Stats baada ya mchezo kumalizika leo Machi 24, 2019

Baada ya matokeo ya leo, Tanzania na Uganda zinafuzu ambapo Uganda inaongoza kundi ikiwa na alama 13 na Tanzania ikiwa na alama 8
1553447706691.jpg
Tanzania imeandikisha historia baada ya kufuzu katika fainali ya bara Afrika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 39, kwa kuifunga Uganda mabao 3-0 katika mechi ya mwisho ya kufuzu ya kundi L, iliyochezwa Jumapili jioni jijini Dar es salaam.


Mabao ya Tanzania yalifungwa na wachezaji Simon Msuva katika dakika ya 21 ya mechi hiyo, huku beki Erasto Nyoni akifunga bao la pili kupitia mkwaju wa penalti.

Agrey Moris naye alihakikisha Tanzania inapata ushindi wa kuridhisha, baada ya kuifunga Taifa Stars bao la tatu katika dakika 57, kupitia shambulizi la kichwa lililomwacha kipa wa Uganda Dennis Onyango akishindwa kuokoa shambulizi hili.

Mara ya mwisho kwa Tanzania kufuzu katika fainali za AFCON ilikuwa ni mwaka 1980 nchini Nigeria na imefuzu nchini Misri, chini ya kocha Emmanuel Amunike raia wa Nigeria.

Wachezaji wote wa Taifa Stars waliocheza mechi za hatua ya makundi kufuzu kuelekea Misri, walikuwa hawajazaliwa mara ya mwisho nchi yao iliposhiriki katika michuano ya bara Afrika.

Licha ya kufungwa, Uganda imefuzu katika fainali hiyo ikiwa inaongoza kundi hilo kwa alama 13, huku Tanzania ikiwa ya pili kwa alama nane.

Kutofungana kwa Cape Verde na Lesotho, jijini Praia pia kumeisaidia Tanzania kufuzu.

IMG_20190325_082558.jpg
 
Hapa taifa watu ni wengi sana haijawahi kutokea,kusema ukweli unaweza kuhisi kiingilio ni bure. Kama wote wataingia ndani uwanja HAUTOSHI KABISA HATA KWA MACHO TU UNAONA.
TFF kama mmeuza tiketi zaidi ya 60k jiandaeni kama kuna janga kitatokea. Bado lisaa tu lakini watu wengi sana.
Taifa stars pigeni mpira mashabiki warudi na furaha... Asante
Mwenye updates tunaomba tuweke hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maelezo marefu hivyo bila hata picha?
 
Hapa taifa watu ni wengi sana haijawahi kutokea,kusema ukweli unaweza kuhisi kiingilio ni bure. Kama wote wataingia ndani uwanja HAUTOSHI KABISA HATA KWA MACHO TU UNAONA.
TFF kama mmeuza tiketi zaidi ya 60k jiandaeni kama kuna janga kitatokea. Bado lisaa tu lakini watu wengi sana.
Taifa stars pigeni mpira mashabiki warudi na furaha... Asante
Mwenye updates tunaomba tuweke hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Msaada tafadhali ni app ipi inaonyesha hii mechi?
 
Tanesco wasikate umeme, maama wao hawana uzalendo kabisa!
 
Baada ya Azam App Kutufanyia hila kwa kuondoa ZBC2 sisi watazamaji tunaokuwa mbali na TV na kulazimika kutumia App yao. Tukumbushane tu kuwa Binadamu wana wivu sana kwa wengine.

Roho ile ile mbaya ikawafanya watuondolee jambo jema walilotuanzishia.anyway wadau tunaokuwa mbali na TV tuwe tunapeana live streaming hapa.
 
Nisiwe mnafki ..

Kwa maslahi mapana ya taifa hili kimataifa ni vyema tufungwe na Uganda ili kuepukana na aibu pamoja na fedheha hapo mwakani AfCON

Miaka michache iliyopita tulifungwa 7 kwa 0 na hakukuwepo na jitihada zozote za kuridhisha ili kuzuia tukio kama hilo lisitokee tena
 
Baada ya Azam App Kutufanyia hila kwa kuondoa ZBC2 sisi watazamaji tunaokuwa mbali na TV na kulazimika kutumia App yao. Tukumbushane tu kuwa Binadamu wana wivu sana kwa wengine.

Roho ile ile mbaya ikawafanya watuondolee jambo jema walilotuanzishia.anyway wadau tunaokuwa mbali na TV tuwe tunapeana live streaming hapa.
Mbona ZBC2 ipo?
Acha ulalamishi..!
Ungewaeleza tbcssm waonyeshe live

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom