Kifimbo1958
JF-Expert Member
- Oct 24, 2015
- 821
- 343
Magufuri na CCM tena makubwa haya.Duh kuna watu wa ajabu humu.Ongera sana raisi wangu, umenitokea kunikosha sana kuona Timu inacheza vizuri, mungu akupe maisha marefu john Joseph pombe magufuri, ongera ccm kwa kazi nzuri mlioifanya taifa mpaka tumeibuka na ushindi
Tuliza akili, in the future usomapo nililoandika hii itakusaidia kunielewa.hakuna timu za vijana , hakuna miundombinu ya soka, ligi inachezeshwa kishabiki wewe unashangilia upuuzi
Duuh! tunaikalia tuPOLITIKI!!!
Tusifanye, maana ata USA na nchi zilizoendelea huwa hawafanyi chaguzi akitokea rais mchapa kazi.Naunga mkono hoja, ni kweli kabisa, ndio maana niliuliza...
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020? - JamiiForums
P
yaani politiki hizi ndugu yangu!!!!!
Wewe hapo.mhandisi ni nani?
Forget Form One Chemistry, I'm dealing with cutting edge stuff. The Hydrogen Bomb!Form One chemistry! OK?
hongera zako zna akil.Ukweli tulipangiwa kundi jepesi, ingawa hatuwezi beza juhudi za serikali kupambana na waharibifu wa mpira walioko magerezani.
Hongera wachezaji na makocha,
Hongera TFF,
Hongera Rais wa TFF Wallace Karia,
Hongera Makamu wa Rais TFF Athumani Nyamlani,
Hongereni Watanzania wenzagu
Usisahau kafara ya mtoto aliyetolewa hapo kwenye lango jana.Timu ya Taifa ya Tanzania(Taifa Stars) leo majira ya saa 12:00 jioni katika Uwanja wa Taifa uliopo jijini Dar inacheza na timu ya Taifa ya Uganda(The Cranes) katika mchezo wa kufuzu kucheza Michuano ya Mataifa ya Afrika(AFCON) nchini Misri
Lesotho yenye alama sawa na Tanzania itakuwa ugenini inamenyana na Cape Verde.
Msimamo wa Kundi ulivyo kabla ya Mechi za mwisho leo
Taifa Stars ili kufuzu AFCON pia inategemea na matokeo ya Lesotho ambapo iwapo Lesotho. Taifa Stars itafuzu iwapo itashinda dhidi ya Uganda na Lesotho atoke droo au afungwe na Cape Verde
Lakini iwapo Taifa Stars na Lesotho zote zitashinda badi Stars inabidi ishinde magoli mengi na kukaa juu ya Lesotho kwenye msimamo wa kundi kwa tofauti ya magoli ya kufungwa na kufunga
UPDATES:
Mashabiki wamevunja geti upande uwanja wa Uhuru na NBSP kuingia kwa nguvu kwenye Uwanja wa Taifa kushuhudia mechi ya Taifa Stars na Uganda.
Nguvu ya mashabiki imewashinda polisi na walinzi wengine na kulivunja geti hilo saa 10.33 jioni hali iliyowalazimu polisi kujipanga upya kuzuia hali hilo.
Katika kipindi cha takribani dakika tano kabla ya polisi kuzuia mashabiki wengi tayari walikuwa wameingia na kwenda moja kwa moja jukwaani
***
View attachment 1053045
Mashabiki kutoka sehemu mbalimbali awanaendelea kuingia uwanja
***
Polisi imewatawanya kwa mabomu ya machozi mashabiki waliotaka kuingia uwanjani kwa kupitia uwanja wa Uhuru katika mechi ya Taifa Stars na Uganda, kutokana na msongamano uliopo kwenye mageti ya Uwanja wa Taifa
***
Vikosi vinavyoanza mchezo wa leo
***
Taifa Stars inapata goli la kuongoza dhidi ya Uganda goli lililofungwa dakika ya 21 na Saimon Msuva. Msuva alipokea pasi safi kutoka kwa John Bocco 'Adebayor'
Aidha, katika mchezo mwingine matokeo katika mchezo wa Lesotho na Cape Verde bado ni 0-0
***
MAPUMZIKO: Taifa Stairs inaenda mapumziko ikiwa inaogoza kwa goli 1-0 dhidi ya Uganda. Katika mchezo wa Lesotho na Cape Verde milango bado ni migumu
Stats zilivyo hadi Mapumziko
***
Taifa Stars inapata bao la pili kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Erasto Nyoni baada ya beki wa Uganda kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari dakika ya 51.
***
Goli la tatu kwa Tanzania kutoka kwa beki Aggrey Morris akimalizia kwa kichwa pasi ya John Bocco dakika ya 57
***
FULL - TIMEStats baada ya mchezo kumalizika leo Machi 24, 2019
View attachment 1053145
View attachment 1053149
Baada ya matokeo ya leo, Tanzania na Uganda zinafuzu ambapo Uganda inaongoza kundi ikiwa na alama 13 na Tanzania ikiwa na alama 8
Tanzania imeandikisha historia baada ya kufuzu katika fainali ya bara Afrika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 39, kwa kuifunga Uganda mabao 3-0 katika mechi ya mwisho ya kufuzu ya kundi L, iliyochezwa Jumapili jioni jijini Dar es salaam.
Mabao ya Tanzania yalifungwa na wachezaji Simon Msuva katika dakika ya 21 ya mechi hiyo, huku beki Erasto Nyoni akifunga bao la pili kupitia mkwaju wa penalti.
Agrey Moris naye alihakikisha Tanzania inapata ushindi wa kuridhisha, baada ya kuifunga Taifa Stars bao la tatu katika dakika 57, kupitia shambulizi la kichwa lililomwacha kipa wa Uganda Dennis Onyango akishindwa kuokoa shambulizi hili.
Mara ya mwisho kwa Tanzania kufuzu katika fainali za AFCON ilikuwa ni mwaka 1980 nchini Nigeria na imefuzu nchini Misri, chini ya kocha Emmanuel Amunike raia wa Nigeria.
Wachezaji wote wa Taifa Stars waliocheza mechi za hatua ya makundi kufuzu kuelekea Misri, walikuwa hawajazaliwa mara ya mwisho nchi yao iliposhiriki katika michuano ya bara Afrika.
Licha ya kufungwa, Uganda imefuzu katika fainali hiyo ikiwa inaongoza kundi hilo kwa alama 13, huku Tanzania ikiwa ya pili kwa alama nane.
Kutofungana kwa Cape Verde na Lesotho, jijini Praia pia kumeisaidia Tanzania kufuzu.
View attachment 1053454
Mafanikio ya Taifa Stars yametokana na Timu za Afcon kuongezwa, na sio Tanzania tu ilio nufaika kuna Burundi, Namibia, Madagascar ata na Kenya.Afcon zimeongezwa timu kutoka timu 16 adi 24, kama ingekua idadi ya zamani Taifa Stars isingefuzu pamoja na izo timu.Mkiwa na kiongozi mkuu ambaye hataki siasa anataka kazi tu ,mambo yote hubadilika kutoka juu mpaka chini ,tofauti na tulivyokuwa tunaaminishwa na baadhi ya wasomi hasa Chadema kwamba rais hata akiwa mwizi ,mvivu mzururaji mambo yataenda tu kisa eti urais ni taasisi?
Katika sekta ya michezo asante Taifa stars, Simba na bondia Mwakinyo
Asante kasi ya Rais Magufuli.
Sent using Jamii Forums mobile app
Any evidence hizo hela zimepotea?kwani 1.5trilioni zimepotea kipindi cha rais gani?
Kifuatacho ITVTimu ya Taifa ya Tanzania(Taifa Stars) leo majira ya saa 12:00 jioni katika Uwanja wa Taifa uliopo jijini Dar inacheza na timu ya Taifa ya Uganda(The Cranes) katika mchezo wa kufuzu kucheza Michuano ya Mataifa ya Afrika(AFCON) nchini Misri
Lesotho yenye alama sawa na Tanzania itakuwa ugenini inamenyana na Cape Verde.
Msimamo wa Kundi ulivyo kabla ya Mechi za mwisho leo
Taifa Stars ili kufuzu AFCON pia inategemea na matokeo ya Lesotho ambapo iwapo Lesotho. Taifa Stars itafuzu iwapo itashinda dhidi ya Uganda na Lesotho atoke droo au afungwe na Cape Verde
Lakini iwapo Taifa Stars na Lesotho zote zitashinda badi Stars inabidi ishinde magoli mengi na kukaa juu ya Lesotho kwenye msimamo wa kundi kwa tofauti ya magoli ya kufungwa na kufunga
UPDATES:
Mashabiki wamevunja geti upande uwanja wa Uhuru na NBSP kuingia kwa nguvu kwenye Uwanja wa Taifa kushuhudia mechi ya Taifa Stars na Uganda.
Nguvu ya mashabiki imewashinda polisi na walinzi wengine na kulivunja geti hilo saa 10.33 jioni hali iliyowalazimu polisi kujipanga upya kuzuia hali hilo.
Katika kipindi cha takribani dakika tano kabla ya polisi kuzuia mashabiki wengi tayari walikuwa wameingia na kwenda moja kwa moja jukwaani
***
View attachment 1053045
Mashabiki kutoka sehemu mbalimbali awanaendelea kuingia uwanja
***
Polisi imewatawanya kwa mabomu ya machozi mashabiki waliotaka kuingia uwanjani kwa kupitia uwanja wa Uhuru katika mechi ya Taifa Stars na Uganda, kutokana na msongamano uliopo kwenye mageti ya Uwanja wa Taifa
***
Vikosi vinavyoanza mchezo wa leo
***
Taifa Stars inapata goli la kuongoza dhidi ya Uganda goli lililofungwa dakika ya 21 na Saimon Msuva. Msuva alipokea pasi safi kutoka kwa John Bocco 'Adebayor'
Aidha, katika mchezo mwingine matokeo katika mchezo wa Lesotho na Cape Verde bado ni 0-0
***
MAPUMZIKO: Taifa Stairs inaenda mapumziko ikiwa inaogoza kwa goli 1-0 dhidi ya Uganda. Katika mchezo wa Lesotho na Cape Verde milango bado ni migumu
Stats zilivyo hadi Mapumziko
***
Taifa Stars inapata bao la pili kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Erasto Nyoni baada ya beki wa Uganda kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari dakika ya 51.
***
Goli la tatu kwa Tanzania kutoka kwa beki Aggrey Morris akimalizia kwa kichwa pasi ya John Bocco dakika ya 57
***
FULL - TIMEStats baada ya mchezo kumalizika leo Machi 24, 2019
View attachment 1053145
View attachment 1053149
Baada ya matokeo ya leo, Tanzania na Uganda zinafuzu ambapo Uganda inaongoza kundi ikiwa na alama 13 na Tanzania ikiwa na alama 8
Tanzania imeandikisha historia baada ya kufuzu katika fainali ya bara Afrika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 39, kwa kuifunga Uganda mabao 3-0 katika mechi ya mwisho ya kufuzu ya kundi L, iliyochezwa Jumapili jioni jijini Dar es salaam.
Mabao ya Tanzania yalifungwa na wachezaji Simon Msuva katika dakika ya 21 ya mechi hiyo, huku beki Erasto Nyoni akifunga bao la pili kupitia mkwaju wa penalti.
Agrey Moris naye alihakikisha Tanzania inapata ushindi wa kuridhisha, baada ya kuifunga Taifa Stars bao la tatu katika dakika 57, kupitia shambulizi la kichwa lililomwacha kipa wa Uganda Dennis Onyango akishindwa kuokoa shambulizi hili.
Mara ya mwisho kwa Tanzania kufuzu katika fainali za AFCON ilikuwa ni mwaka 1980 nchini Nigeria na imefuzu nchini Misri, chini ya kocha Emmanuel Amunike raia wa Nigeria.
Wachezaji wote wa Taifa Stars waliocheza mechi za hatua ya makundi kufuzu kuelekea Misri, walikuwa hawajazaliwa mara ya mwisho nchi yao iliposhiriki katika michuano ya bara Afrika.
Licha ya kufungwa, Uganda imefuzu katika fainali hiyo ikiwa inaongoza kundi hilo kwa alama 13, huku Tanzania ikiwa ya pili kwa alama nane.
Kutofungana kwa Cape Verde na Lesotho, jijini Praia pia kumeisaidia Tanzania kufuzu.
View attachment 1053454
Endeleeni na chuki zenu lakini JPM ni bahati kwa watanzania kila anachojaribu kinajibu. Ferguson huwa anasema si ubora wa timu pekee na bahati lazima uwe nayo. Maximo mlimjaza manoti lakini wapi??Huwezi ukapanda mti leo na kuvuna kesho. Sifa pia zimuendee J.k. hawa wote wamepata motisha tangu kipindi cha J.K
Uganda tandika hao adi bashite arudi kwao kolomije Najua okwi hatatuangusha.
Kusema ukweli mpaka sasa sioni matumaini ya misalaba kushinda labda Uganda waamue kuwaachia tu