Mziki umechange huwezi fanya kitu chochote zama hizi ukakifanya vile vile kama kilivyofanyika miaka 10 iliyopita utafail.
Mziki bila promo now ni ngumu, kipindi jay d anaanza mziki nyimbo zilikuwa chache hata vituo vya redio vilikuwa vinapokea nyimbo chache na kulazimika kuzipiga zote yani zamani kuingia studio ukarekodi ndiyo ilikuwa kazi, ukisharekodi basi ujue umetoboa tu ndiyo maana hata watu kama akina dudu baya waliweza kutoboa.
Unaufahamu mziki flani jamaa anaimba lafudhi ya kichaga ambaye sasa hivi ni mmoja wa watengenezaji wa kipindi cha ubongo kids yule anaongea sauti ya yule twiga,
Aliimba mziki sijui ni jinsi gani ni namna gani tutawin maishani ....
Ile ilikuwa ni freestyle studio baada ya jamaa yake kufunga vifaa wakawa wanavijaribisha lakini kutokana na nyimbo kuwa chache wimbo ule ikaenda redioni.
Hata biashara now zinahitaji promo ndiyo maana sehemu kubwa ya muda kwenye tvs na redio utaona ni matangazo ya kibiashara tofauti na zamani.
In short kwasasa mziki unahitaji promo zama zimebadirika bila promo lazima ufail ndiyo maana kuna nyimbo nzuri hazijahit coz zimekosa promo kisa waimbaji ma underground hawana ela