Baada ya miaka miwili anarudi na kuomba nimuoe bila mahari

Watu wengine, kwamba mna pesa sana ama! Anyway nafsi yako inasemaje, japo inaonyesha bado unampenda ila ni risk kishenzi🌚
Kwa akili angu kaka huyo mwanamke hata kumgusa nisingeweza tena bora nkalale na malaya
Kaka ukisoma frsh hapo utaona kuwa sahivi nna katoto kamoja kana mwaka, niliamua nipate mtoto tu kisha nitulie zangu! Siwezi rudiana nao tena ile familia
 
Kimbia fasta

Usije sema hukuambiwa
 
Huyo shemeji hata haelezeki, unajua mzee wao alikuwa ana kampuni ya kufix generators pale Mikocheni, na alikuwa ana mikataba mizuri tu clouds na cocacola! Mzee wao alivyofariki huyo jamaa ndo aliachiwa kampuni ikiwa ina gari mbili za office, kodi ya muda mrefu, team nzima pamoja vifaa vingine muhimu! Aise ndani ya miezi kadhaa aliuza kila kitu hadi staff wakaanza kuondoka mmoja baada a mwingine! In short huyo jamaa ana 43 lakini akili yake niya under 18
 
Waheshimiwa! Kwa hii story niliyoandika nimegundua kitu kimoja cha ajabu sana, imagine like 70% hawajaongea kuhusu matukio ya hiyo familia na tabia zao za ajabu ila wanashangaa kutoa 15M ??!!!

Kiukweli nimepambana sana na bado napambana, ilifikia hatua nikataka kuuza gari, na biashara nilifunga nikaanza from scratch! Lakini kwenye maisha yangu yote sijawahi kuwa na uoga wa kushtushwa na 7figures.

Mtu anasema huna uwezo wa kutoa 15M, mwingine kama story ni ya kweli basi 0 moja imeongezwa 😄... sasa hebu jiulize kitu kimoja, kama tokea umezaliwa hadi sahivi (naamini wengi ni 30s) unakosa imani kabisa mtu akiandika 15M, ramani yako (roadmap) ipoje aise? Au ndo tunaishi kwa mazoea tu kwamba ukila, ukinywa ndo baasi hayo ndo maisha? Hakuna savings, hakuna malengo, hakuna dharura? 15M si pesa rahisi kupata wala kutoa, lakini it means hata ukiipata ila ukaja kuipoteza kwenye hasara za biashara inaweza kukuzika!

Ukiendelea kushtushwa na hizo pesa hutozipata mazee, sio kwamba ninazo hata! ila sometimes act kama unazo at least ikujengee ujasiri, maana sasa kama unaisoma 15M na bado unashangaa japo ni maandishi tu na upo over 30 si hatari hiyo?! Acheni hizo mambo bhana tupambane 😄😄😄
 
We mshukuru Mungu umelenga mahala pazuri mkuu, unafikiri Yuda na Petro walikusudia kumsaliti Yesu?! 😄
 
Wadada humu jf ,jimbo lipo wazi,au mpaka atume maombi Kuna kujiongeza .Kila siku kwa mtume mwamposa haya ..changamkieni fursa
 
Ila wazazi wa kike kwa watoto wao wa kike, Ni kama jeneza Na sanda, hii story Ina fanana sana na story Moja hv . tofauti ni maokoto
 
Unapatikana wapi mkuu?

Wewe utanifaa, una pesa nyingi za kuchezea..!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…