Baada ya miaka miwili anarudi na kuomba nimuoe bila mahari

Wanakunyonya pesa. Bora uanze upya.
Nishaanza upya ndugu yangu, unajua waliniacha mweupeee! ila nikakomaa, sasa nadhani wamenipata kupitia kazi ninazofanya maana najitangaza sana! ila siwezi warudia KWA NAMNA YOYOTE
 
shauri yako wanawake hawajaisha kiasi hicho.
vijana mnaodate na wadada kwa kutumia vichwa vya chini nawahusia kabla ya kuoa mwanamke angalia pia na familia yao.
kwa ufupi tu kama ni kijana unayejitambua ulitakiwa kuachana na huyo dada baada ya kuona familia yake ilivyo na siku ukijichanganya utaishi kwa shida maisha yako yote.
vijana ebu wakati mwingine ombeni hata hekima jamani mbona jambo dogo ila upo kama kuku aliyekatwa kichwa.
umekazana binti ni mlokole hivi kuna mlokole wa hivyo?
kijana mjinga ulikuwa unajitwisha majukumu yasiyokuhusu ndo maana wanakuona boya
 
kwa kijana wa aina yako wazazi wako wana hasara
 
Kwanza kabisa pole ,
Mwanaume mwenye busara
Hujifunza kutokana na makosa.

Kama utaamua kumsamehe sitisha misaada kwa wazazi wake na kisingizio kiwe una mambo mengi ya kuyafanya kwa sasa .

Lengo ni kupima kama binti karudi ya kwamba wewe ni mkombozi wa familia yake au la , amerudi kwa upendo au la .

Then
Muhudumie yeye kama mke

Alafu sikilizia mchezo

Wakikujia juu eti ujali familia yake muache binti yao arudi kwao.

Yangu ni hayo mister
All the best.
 
Ujinga unalitesa sana ili taifa Eeh Mungu tuondolee ujinga taifa lisonge mbele
Sio ujinga, UPENDO... Kuna mzee mmoja alisema "UKITAKA KUFANIKIWA USIENDEKEZE UPENDO WALA HURUMA" sasa ndo naelewa! Kuna muda unaweza hisi unamtetea unaempenda kumbe yeye anakunyonga taratibu
 
kwa kijana wa aina yako wazazi wako wana hasara
Wazazi wangu wangekuwa wamepata hasara, pengine ninavyoandika hapa hata wasingekuwepo! ila Mungu amewapa kijana anayeweza kuwapambania na ndio maana sahivi hawafanyi kazi ila wanaishi, kuwa na adabu mkuu!
 
very stupid young man

kama taira yani hata mi nimeshangaa naona lingekuwa karibu nilizabe kibao.
unaweza kuta mama yake analia shida
Tukutane wapi unizabe kibao?! Utaweza? Usinione fala kisa haya yaliyotokea, kuna muda tunazuia hasira kuwalinda walio nyuma yetu, asie kuwa makini na maneno yako!
 
 
Nishaanza upya ndugu yangu, unajua waliniacha mweupeee! ila nikakomaa, sasa nadhani wamenipata kupitia kazi ninazofanya maana najitangaza sana! ila siwezi warudia KWA NAMNA YOYOTE
Hakika masta. Hatutapenda tusikie taarifa ya risasi.
 
sema daah binadamu sisi tunapata nafasi tunachezea yaan mtu ukishapitia msoto ndo unakuja kujua namna gan ulikua hutumii akili mtu anakupa pesa 15m ya bure bila mkopo wala nn aisee
 
sema daah binadamu sisi tunapata nafasi tunachezea yaan mtu ukishapitia msoto ndo unakuja kujua namna gan ulikua hutumii akili mtu anakupa pesa 15m ya bure bila mkopo wala nn aisee
Ni kweli aise, huyu binti angetulia tungefika mbali pamoja ila aliamua kuwa muuaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…