Baada ya miezi 9 uraini Kajala aibuka tajiri wa kutisha

Baada ya miezi 9 uraini Kajala aibuka tajiri wa kutisha

Shakir

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2012
Posts
1,627
Reaction score
1,926
MIEZI tisa baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar kumhukumu staa wa filambu za Bongo, Kajala Masanja kifungo cha miaka mitatu jela au faini ya shilingi milioni 13 kwa kosa la utakatishaji fedha na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu kumlipia hivyo kuwa huru, hali ya maisha ya msanii huyo imebadilika ghafla na sasa ameibuka katika utajiri wenye maswali na majibu.

Kajala Masanja.
Chanzo makini kimeliambia gazeti hili kwamba, Kajala ambaye alitoka mahabusu ya Segerea jijini Dar, Machi 25, 2013 akiwa hana mbele wala nyuma kiasi cha kutia huruma, sasa anazikamata za kutosha kiasi cha watu wake wa karibu kumshangaa.

MANUNUZI YAKE
Chanzo kimebainisha kuwa, Kajala ameagiza kutoka China kontena lenye urefu wa futi 20 likiwa limesheheni samani za ndani. Samani za ndani ni fenicha mbalimbali.

Wema na shosti wake Kajala.
“Hivi mnajua kwamba Kajala yuko juu. Naweza kusema ni tajiri kwa sasa, maisha yake ni poa. Hivi ninavyoongea kuna kontena la futi arobaini linakuja Dar, ndani mna samani tu,” kilisema chanzo hicho.

AMWAGA MILIONI 90 KUTENGENEZA FILAMU
Katika hali inayoendelea kutafsiriwa kuwa ni kuzidi kuonesha ukwasi alionao, msanii huyo ameshatumia shilingi milioni 90 kwa ajili ya kutengeneza filamu zake tatu, kila moja ikitumia bajeti ya milioni 30 za Kibongo.
Filamu ya Kajala ambayo iko njiani kutoka inaitwa Laana. Inadaiwa mpango wake ni kutengeneza filamu 10 ambazo atakuwa akiziuza kwa nyodo. Kama ni hivyo atatumia shilingi milioni 300 kwa filamu hizo kumi.

ATUMIA MILIONI 11 KUNUNUA VITO VYA THAMANI
Mbali na kuvaa magauni na viatu vya bei mbaya, hivi karibu staa huyo alitua Dar akitokea China ambapo alipigilia vito vya gharama ya maisha ya familia nzima.
“Juzikati Kajala katoka China na cheni ya dhahabu kainunua dola za Marekani elfu tatu, bangiri pia ya dhahabu ya dola elfu mbili na mia tano na hereni za gold (dhahabu) za dola elfu moja mia tano,” kilisema chanzo.
Kwa mahesabu ya sasa, kiasi hicho cha dola kikibadilishwa na shilingi ya Tanzania, Kajala alitumia kama milioni 11 kununua vito hivyo tu.

ANAYEMPA JEURI ATAJWA
Inadaiwa mcheza filamu huyo amekuwa akipata jeuri hiyo kutoka kwa mwanaume bilionea wa Ghana aliyejulikana kwa jina moja la Safara ambaye walikutana nchini China. Inadaiwa Safara anaishi Marekani lakini ndiye anayeshika tenda ya kuinunulia serikali ya Ghana vitu mbalimbali.

MWISHO DESEMBA KUISHI NYUMBA YA KUPANGA
Habari zikazidi kumiminika kwamba, Safara amemwambia Kajala mwisho Desemba mwaka huu kuishi kwenye nyumba ya kupanga, mwakani mjengo wake utakuwa umekamilika.
Hata hivyo, haijaelezwa kama ameshapata kiwanja cha kujengea au la! Ingawa habari zinasema nyumba anayoishi sasa Kajala imeshalipiwa kodi ya mwaka mmoja na tajiri huyo wa Ghana.

MFADHILI WEMA
Ikazidi kudaiwa kuwa, katika ziara ya baadhi ya mastaa jijini Arusha hivi karibuni wakiongozwa na Wema ambako kulikuwa na shoo ya muziki wa Kizazi Kipya, Kajala alimsaidia Wema mambo mbalimbali zikiwemo pesa ili kufanikisha shughuli hiyo iliyohitaji umakini wa hali ya juu.
“Mbali na fedha hizo, Kajala wa zamani si huyu wa sasa, ila ninashomsifu bado anamheshimu sana Wema, anajua ndiye amechangia mafanikio yake, kama siku zile asingetoa zile milioni kumi na tatu Kajala angekuwa gerezani,” kilisema chanzo hicho.

ALIPOTOKA GEREZANI
Inadaiwa baada ya kutoka Segerea, Kajala aliishi maisha ya kuwa na shida hata shilingi elfu kumi ilimsumbua, Wema ndiye aliyekuwa akimbeba kwa vijisenti vya matumizi na baadaye alimwajiri kwenye kampuni yake ya filamu ya Endless Fame kama sekretari. Kampuni hiyo kwa sasa imesimama.

HUENDA CHINA KINYEMELA?
Baada ya kuona safari zake zimezaa matunda na kuhisi watu wanafuatilia nyendo zake, likiwemo gazeti hili, Kajala ambaye husafiri mara kwa mara, amekuwa akidai anakwenda Zanzibar licha ya hati zake za kusafiria kuoneshwa zimegongwa mihuri ya China na Dubai.

KAJALA SASA
Alipoulizwa kwa njia ya simu juzi kuhusiana na ukwasi wake kwa sasa, Kajala alisema anachojua yeye anaishi maisha ya kawaida, tafsiri kwamba amekuwa tajiri ghafla inafanywa na watu wanaomuona.
“Mimi naishi kawaida tu, huo utajiri wanauona wao. Unajua haya ni maisha, leo unakuwa hivi, kesho unakuwa vile ndicho ninachoweza kukisema, siwezi kusimulia kila kitu,” alisema Kajala.

Source; GLOBAL PUBLISHERS
 
Sijui wana deal gani hawa madiva..
wema, kajala na aunt Ezekiel hata siwaelewi
 
Akimtambulisha tu kwa Wema imekula kwake,hapo bado sijaona utajiri labda azifanyie cha maana zimuinuee
 
Hii dunia tunapita kama anapata pesa zote kiuhalali basi kila la kheri kajala...
 
HEBU TUANZE NA MFANO WA HUYU, WANAMWITA KAJALA:
NI MIEZI KAMA TISA TOKA ATOKE JELA, LAKINI HABARI TULIZO ZISIKIA HIVI PUNDE ETI AWA MILIONEA? MATUMIZI ALIYO YAFANYA NI YA MTU ALIYEFANYA KAZI KWA BIDII KWA COUPLE OF YEARS, HII INANITIA SHAKA NA AINA YA BIASHARA ANAYOFANYA. ETI KUNA TAJIRI WA GHANA NDIO ANAMWEKA SAWA? HIVI INAWEZEKANA MTU AKUGHARAMIKIE MILION MIA MBILI JUST FOR KITUMBUA? HAHAA I REALY DOUBT ABOUT HAWA WASANII WETU.

HEBU TUFUATILIE HUU MTIRIRIKO KAMA INAHITAJI TUME:

  1. ALIPOTOKA GEREZANI
Inadaiwa baada ya kutoka Segerea, Kajala aliishi maisha ya kuwa na shida hata shilingi elfu
kumi ilimsumbua, Wema ndiye aliyekuwa akimbeba kwa vijisenti vya matumizi na baadaye
alimwajiri kwenye kampuni yake ya filamu ya Endless Fame kama sekretari. Kampuni hiyo kwa
sasa imesimama.
2. HUENDA CHINA KINYEMELA?
Baada ya kuona safari zake zimezaa matunda na kuhisi watu wanafuatilia nyendo zake,
likiwemo gazeti hili, Kajala ambaye husafiri mara kwa mara, amekuwa akidai anakwenda
Zanzibar licha ya hati zake za kusafiria kuoneshwa zimegongwa mihuri ya China na Dubai.
3.AMFADHILI WEMA
Ikazidi kudaiwa kuwa, katika ziara ya baadhi ya mastaa jijini Arusha hivi karibuni wakiongozwa
na Wema ambako kulikuwa na shoo ya muziki wa Kizazi Kipya, Kajala alimsaidia Wema mambo
mbalimbali zikiwemo pesa ili kufanikisha shughuli hiyo iliyohitaji umakini wa hali ya juu.
“Mbali na fedha hizo, Kajala wa zamani si huyu wa sasa, ila ninashomsifu bado anamheshimu
sana Wema, anajua ndiye amechangia mafanikio yake, kama siku zile asingetoa zile milioni
kumi na tatu Kajala angekuwa gerezani,” kilisema chanzo hicho.
4.AMWAGA MILIONI 90 KUTENGENEZA FILAMU
Katika hali inayoendelea kutafsiriwa kuwa ni kuzidi kuonesha ukwasi alionao, msanii huyo
ameshatumia shilingi milioni 90 kwa ajili ya kutengeneza filamu zake tatu, kila moja ikitumia
bajeti ya milioni 30 za Kibongo.
Filamu ya Kajala ambayo iko njiani kutoka inaitwa Laana. Inadaiwa mpango wake ni
kutengeneza filamu 10 ambazo atakuwa akiziuza kwa nyodo. Kama ni hivyo atatumia shilingi
milioni 300 kwa filamu hizo kumi.
5.MANUNUZI YAKE
Chanzo kimebainisha kuwa, Kajala ameagiza kutoka China kontena lenye urefu wa futi 20 likiwa
limesheheni samani za ndani. Samani za ndani ni fenicha mbalimbali.
“Hivi mnajua kwamba Kajala yuko juu. Naweza kusema ni tajiri kwa sasa, maisha yake ni poa.
Hivi ninavyoongea kuna kontena la futi arobaini linakuja Dar, ndani mna samani tu,” kilisema
chanzo hicho.

HUU NI MFANO TU, KUNA WASANII NINA MUDA SIJASIKIA HIT SONG YOYOTE TOKA KWAO, LAKINI UTASIKIA MARA KAENDA UINGEREZA, USA, CHINA, SOUTH AFRICA...KUFANYA SHOW, VERY BIZY NA KUSAFIRI i.e AY. SHOW ZA NINI HUWA WANAFANYA? KUNA BAADHI SIJAWAHI SIKIA WAKIENDA NJE KUFANYA SHOW NA WANA NYIMBO KALI TU i.e JAYDEE.
 

Attachments

  • kajala.jpg
    kajala.jpg
    85.3 KB · Views: 474
Isijekua tunafuga mbu halafu tunawatafutia sumu..
 
Hao wamezoea promo z shigongo hamna jipya.mbna wema hana tena ofisi nae kajala walewale,kma alikua n hela c angejidhamini kipindi ana case hpo n promo 2 z kuuza papuchi zao hamna cjui pedejee wala sembe hpo n papuchimovie
 
Back
Top Bottom