Baada Ya Mo Dewj Kunyimwa Simba, Msimu Huu wa Simba Utakuwa mbaya kuliko yote


Mo Dewj amenyimwa Simba kwa sababu ambazo siwezi kusema lolote. lakini pia sitaki kusema kama mwarobaini pekee ulikuwa yeye ingawa naamini kama angepewa simba tungepata nafasi ya kuangalia msimu huu anaijengaje na nini matokeo yake.mpira ni pesa. leo tarehe 31/07/1026 nawaambia wanachama wa Simba kama suala la Mo Dewj limepigwa tena danadana na mwishowe kubutuliwa mbali kabisa nje ya uwanja. msimu huu utakuwa ni mmoja ya misimu mibaya kabisa ya Simba. wachezaji wameshaanza kukata tamaa na hili husababisha wauze mechi au wacheze chin ya Kiwango.
 
Nadhani hujamsiiliza MO,ukijibu maswali yako namba 5 na 6 mengine yanakufa kibudu...
MO alisema hajaandika barua kuomba kununua hisa kwasababu huwezi kuomba kitu ambacho hakipo na kilichofanyika jumapili ni kupitisha kama Katiba ya Simba ibadilishwe kuweza kuwa kampuni ili wingie kwenye mfumo wa kuuza hisa...
MO alisema yeye anapendekeza wanachama wagaiwe hisa kila mmoja...
acha mabadiliko yaje..
 
Huyu jamaa aache upuuzi 20 billion ni chache kununua simba, brand yenyewe ni zaidi ya billion 20 zao.
Hiyo brand zaidi ya bil.20 inainufaidga nini Simba zaidi ya wajanja kutafuna tena hadi kutafuna fedha za rambirambi.Acha MO achukue tupate burudani.
 
acha kupotosha hajanyimwa timu timu hawezi kupewa kama anavyoweza kumpa pipi mwanao ni mchakato ambao unaweza kumaliza hata mwaka...
Na MO yuko tayari kusubiri huku akiendelea kuihudumia team...
 
Ila kwa kuwa unabisha kiunazi basi mpeni timu..... UNASEMA HAUWEZI KUOMBA KITU AMBACHO HAKIPO, HISA ZIPO !!!??? Si kaomba apewe hisa 51%... Au haulioni hilo umejaa unazi!!!?? .... Katiba kubadilishwa na kuisajili unafikiri ni kuamka na kuoga eti!!!?? .... Mihemko imejaaa kuliko uhalisia.... Kweli kwenye udhia penyeza rupia..... Wanawaza 20b bila kutumia uelewa wa mambo ....
 
Aveva alisema MO hajaandika barua kuomba kununua hisa naye mo jana kasema hakuomba his a kwasababu hawezi omba kitu ambacho hakipo ila baada ya wanachama juzi kupitisha ameshaandika maana kimsingi wanachama wameshapitisha bado mambo ya kisheria...hayo ya unazi sijui rupia ya kwako wewe...
 
Kuwa mwelewa kwanza.Unanunua hisa ya kitu ambacho hakipo? Simba si kampuni sasa hiyo hisa itatoka wapi.Muwe mnakubali mabadiliko maana mambo yanaenda kwa kasi sana dunia hii mambo ya wanachama wasioweza hata kulipia kadi zao si ya msingi sana kwa dunia ya leo ambapo mpira na michezo kwa ujumla ni suala la uwekezaji na yanahitaji fedha nyingi.
 
Nani sasa sio muelewa katika hili !!!??? Umesoma nilivyoviandika!!??? Kwa hiyo kama wanachama wanasema apewe basi apewe tu hata kesho ndio unavyotaka eti!!??? ....
 
sisi wanachama wa simba tunachotaka MO apewe timu..asajili wachezaji wa maana timu ifanye vizur kimataifa...mambo ya hisa sijui upuuzi gani tupa kuleeee
 
Nani sasa sio muelewa katika hili !!!??? Umesoma nilivyoviandika!!??? Kwa hiyo kama wanachama wanasema apewe basi apewe tu hata kesho ndio unavyotaka eti!!??? ....
No,unajua mnapinga Simba kuwa kampuni kwa kuwa mnanufaika nayo...na hii issue si ya kupewa wala kuinunua bali ni kugeuza kuwa kampuni na kufanya share katika hisa ambapo inatakiwa mtu mmoja awe na maamuzi...ukishasema mambo ya kampuni na share basi hapo kina mambo mengi sana ya kisheria.Hatutakiwi kuwa waoga katika mambo madogo sana hayo.
 
acha kupotosha hajanyimwa timu timu hawezi kupewa kama anavyoweza kumpa pipi mwanao ni mchakato ambao unaweza kumaliza hata mwaka...
Na MO yuko tayari kusubiri huku akiendelea kuihudumia team...
Ndivyo mleta habar alivyo andika
 
Asante kumbe tupo boti moja .... Tatizo upigaji wa makasia ndio tofauti .....
 
sisi wanachama wa simba tunachotaka MO apewe timu..asajili wachezaji wa maana timu ifanye vizur kimataifa...mambo ya hisa sijui upuuzi gani tupa kuleeee
Hahaaaaa tutakuja lia mbeleni ohooooo....... Kwa mapenzi tu ya soka .... Mo anataka kafanya kitu sahihi ila kwa utaratibu usio sahihi..... Shida ndio ipo hapo tu
 
Moo kashapewa timu wewe mleta mada uchwara, stupid kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…