Baada Ya Mo Dewj Kunyimwa Simba, Msimu Huu wa Simba Utakuwa mbaya kuliko yote

Sodoku

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2016
Posts
1,271
Reaction score
2,903
Mimi ni mwanachama hai wa Simba. sina haja ya kuweka namba yangu . Kuna mambo ambayo nayakubali katika mpira bila kupepesa macho siku zote nitasisitiza. Kwa hatua tuliyofika sasa Mpira wetu unataka pesa.

Mo Dewj amenyimwa Simba kwa sababu ambazo siwezi kusema lolote. lakini pia sitaki kusema kama mwarobaini pekee ulikuwa yeye ingawa naamini kama angepewa simba tungepata nafasi ya kuangalia msimu huu anaijengaje na nini matokeo yake.mpira ni pesa. leo tarehe 31/07/1026 nawaambia wanachama wa Simba kama suala la Mo Dewj limepigwa tena danadana na mwishowe kubutuliwa mbali kabisa nje ya uwanja. msimu huu utakuwa ni mmoja ya misimu mibaya kabisa ya Simba. wachezaji wameshaanza kukata tamaa na hili husababisha wauze mechi au wacheze chin ya Kiwango.

Tatizo si kocha, tatizo ni Uongozi na pia ukata ndo utakaoua team ya simba. wachezaji wengi wameonekana kukosa morali baada ya kuona ajenda ya Mo Dewj Kupewa Team imetupiliwa Mbali. wengi wanalalamika kuwa pesa hawapati za kutosha na kwa wakati muafaka. ukiacha mazingira mazuri n.k. watu wasisahau mpira huu wa sasa ni ajira na si mapenzi.

Nafasi hii itasababisha wachezaji wetu wanunuliwe na team zenye pesa wanapocheza nazo na hivyo kupoteza mechi hizo. NAWAHAKIKISHIA SIMBA IKIJITAHIDI SANA MSIMU HUU KAMA HAKUTAFANYIKA MABADILIKO BASI NI NAFASI YA NNE AU TANO NA UKITOKEA MUUJIZA NAFASI YA 3.

Kama Ungozi huu utaendelea ulivyo na Simba ikachukua Ubingwa Nipigwe BAN MILELE HUMU JAMII FORUMS. na ikichukua NAFASI YA PILI NIPIGWE BAN MIEZI MIWILI.

Tunaumia kuona Yanga wananunua mechi ngumu za hapa TZ wanshinda wanaenda kucheza mechi za Kimataifa huku wao wakifurahia tu kupanda ndege na si kwenda Kushindana. Sisi tunataka Simba iende kushindana na si kutaka kupanda ndege.

Mtakumbuka hadithi ile ya JOGOO ALIYESEMA.
 
agenda imetupiliwa Mbali kivipi? mkutano mkuu umeidhinisha mabadiliko ya katiba kuruhusu hilo...hii ni process hatuwezi kukamilisha ndani ya siku moja...otherwise Leo simba tumefanya maamuzi ya kihistoria
 
Umeona ukiongelea upumbavu wenu na huyo Mo Dewj wenu haitoshi hadi uitaje Yanga si ndio ???
 
Hiv huyu Aveva ana nguvu kulko wanachama wa Simba/ fan's mnamuendekeza..Simba ni ya watu na watu wameamua kumpa Dewji maana wanataka raha na si vinginevyo..
#Nitafurah kuona simba mnarud hata katika kanafasi kapili maana sisi kama Yanga pale 1 tumejichimbia miaka buku"
 
MO kama anamapenzi ya dhati na Simba amwage fedha pale kuisaidia timu msimu huu wa 2016/2017 na si anachotaka kufanya. Afadhiri timu isajiri,ijenge uwanja wake
Hawezi kumwaga pesa mahali ambapo hatokuwa na mamlaka ya kusimamia matumizi ya pesa hizo. Hicho ndicho kilichomwondoa Simba na Singida United. Huwezi weka pesa yako mahali halafu watu wanaitumia vibaya nawe unaona lakini huna nguvu ya kudhibiti. Anataka hisa asilimia 51 ili aweke menejimenti yeye. Awe na nguvu ya kuhoji na kuwajibisha.
 
agenda imetupiliwa Mbali kivipi? mkutano mkuu umeidhinisha mabadiliko ya katiba kuruhusu hilo...hii ni process hatuwezi kukamilisha ndani ya siku moja...otherwise Leo simba tumefanya maamuzi ya kihistoria

.....kwahiyo tuvumilie kuendelea kuburuzwa na yeboyebo mpk katiba irekebishwe?!

.....kwani haiwezekani kuendelea na huo mchakato wa katiba huku Dewji akisaidia hata kwenye usajili?!

.....kumuweka pembeni Dewji kwa sababu yoyote ni sawa na kuruhusu kuendelea kuwa wa bei rahisi, tunasajili "rejects" kuanzia makocha mpk wachezaji!.
 
Moja kati ya timu ambazo Yanga alipiga mbele-nyuma (yaani, kampa ... kampa tena) ni Simba. Ina maana Yanga alinunua mechi za Simba au kwa maneno mengine Simba ni ____ poa?

Mimi nawashangaa sana wamatopeni. Kwani wakati ule Simba inafadhiliwa na Azim Dewji, tulikuwa hatuwabandui nyie?

Halafu mihemko ya kuzungumzia mechi za Yanga, mnaishia kwenye matokeo au mnaangalia na kiwango cha mpira kinachopigwa? Kama Yanga amenunua mechi, siku mliotandikwa bao moja (cha nguruwe) na Toto Africa, na wao walinunua mechi? Hebu acheni mambo ya kipuuzi, jadilini mambo yenu ya hina huko, mwanaume muacheni.

Kwa kuwasaidia tu...NI YANGA TU NDIO ILIWAHI KUTOKA NJE YA MIPAKA NCHI, IKATIMUA TIMBWILI NA KUJA NA NDOO HOME. Nyie ni mama wa nyumbani, kama kwenye kabati lenu kuna chochote, basi kimepatikana hapa hapa nyumbani. Ubavu wa kwenda kwenye ardhi ya watu kukinukisha nyie hamna. Mbwa koko habweki ugenini...kaeni kimya

upload_2016-7-31_15-19-17.jpeg
 
Hiv huyu Aveva ana nguvu kulko wanachama wa Simba/ fan's mnamuendekeza..Simba ni ya watu na watu wameamua kumpa Dewji maana wanataka raha na si vinginevyo..
#Nitafurah kuona simba mnarud hata katika kanafasi kapili maana sisi kama Yanga pale 1 tumejichimbia miaka buku"
Shida ya Simba shule. Tule tubabu hatujui nguvu ya pesa, bado tunaamini uchawi
 
.....kwahiyo tuvumilie kuendelea kuburuzwa na yeboyebo mpk katiba irekebishwe?!

.....kwani haiwezekani kuendelea na huo mchakato wa katiba huku Dewji akisaidia hata kwenye usajili?!

.....kumuweka pembeni Dewji kwa sababu yoyote ni sawa na kuruhusu kuendelea kuwa wa bei rahisi, tunasajili "rejects" kuanzia makocha mpk wachezaji!.
lazima tuvumilie...hii ni process
 
Hivi rais wa Simba alipofunga mkutano kwa kusema hoja imekubaliwa na mkutano Mkuu Simba ifanye mabadiliko kamati uongozi utaandaa utaratibu..umeelewa ama bado viroba vipo kichwani mwako...kubadili mfumo ni baada ya wanachama kusema ndio kwa hoja hii..kifuatacho ni utelezaji tuu
 
MO kama anamapenzi ya dhati na Simba amwage fedha pale kuisaidia timu msimu huu wa 2016/2017 na si anachotaka kufanya. Afadhiri timu isajiri,ijenge uwanja wake
ufadhili timu bila kupata faida hakuna tajiri atakayefanya hivyo
 
Back
Top Bottom