Wakuu,
Mfano, mwanamke akishika mimba mwezi huu, je mwezi ujao anaweza kupata hedhi ama hukoma hapo hapo baada ya mimba kuingia?
Mfano, mwanamke akishika mimba mwezi huu, je mwezi ujao anaweza kupata hedhi ama hukoma hapo hapo baada ya mimba kuingia?
- Tunachokijua
- Hedhi ni utaratibu wa kawaida wa kibiolojia ambao huandaa mwili wa mwanamke kwa ajili ya ujauzito kila mwezi. Kwa kawaida hedhi huanza kati ya umri wa miaka 8 na 15 na inaweza kuacha kati ya miaka 45 na 55 au zaidi.
Je, mwanamke anaweza kupata hedhi kipindi cha Ujauzito?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umejirirdhisha kuwa si kweli kuwa mwanamke anaweza kupata hedhi akiwa mjamzito.
Tafiti na makala za afya zinabainisha hivyo, kuwa mwanamke hawezi kuwa mjamzito na wakati huo huo aendelee kupata hedhi ingawa haizuii yeye kutokwa na damu wakati mwingine.
Cleverland Clinic wanaeleza kuwa iwapo mtu ni mjamzito na akajihisi kutokwa na damu inaweza kusababishwa na mambo mawili. Sababu ya kwanza inaweza kuwa mwanamke si mjamzito.
Sababu ya kutokwa na damu inaweza kuwa inaweza kutokana na mambo yafuatayo, hupaswi kuogopa sana. Miongoni mwa sababu hizo inaweza kuwa;
- Damu kutoka wakati wa kijusi kinapojipachika katika mji wa mimba (Implantation bleeding)
- Kutokwa na damu kwenye shingo ya kizazi ambayo si ya hedhi (Cervical bleeding)
- Mkusanyiko wa dau iliyoganda chini ya kondo la nyuma (Inaweza kutoka ukeni miezi ya mwanzo ya ujauzito)
- Kondo la nyuma lililoshuka chini (placenta previa)
- Mimba kutungwa nje ya mji wa kizazi
- Kutengana kwa kondo la nyuma na ukuta wa mji wa mimba kabla ya wakati
- Kuharibika kwa mimba
- Rangi ya damu
- Kiwango cha damu
- Muda wa kutokea kwa damu
- Kipindi cha kutokwa na damu
- Mwonekano wa damu
- Dalili zinazojitokeza
- Dalili zinazoonesha uwezekano wa ujauzito