Baada ya Mzee Yusuph kuacha taarabu sasa ageukia Kaswida.

Baada ya Mzee Yusuph kuacha taarabu sasa ageukia Kaswida.

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Mfalme wa taarabu wa miaka yote ambaye aliwahi kutikisa na vibao vyake kama vile Wagombanao ndio wapatanao,Wasiwasi wako ndiyo maradhi yako,My Valentine , V.I.P,Mkuki Moyoni, Daktari wa mapenzi nk ambaye pia alikuwa mkurugenzi wa bendi ya Jahazi Modern Taarabu chini ya vijana machachali kama vile Prince Amigo,Mohammed Mtu Poli ,Fatma Mahmoud (Mcharuko) Leyla Rashid,Khadija Yusuph,Rahma Machupa nk sasa ameguikia rasmi Kaswida mara baada ya kuacha kuimba tarabu na kuamua kumrudia Mwenyezi Mungu.

Ikumbukwe mbali na uimbaji ,mfalme Mzee Yusuph alikuwa pia mtunzi na asilimia 90 ya vibao vya jahazi modern taarabu yeye ndiye hutunga na kuangalia ampe nani aimbe.

Miongoni mwa vibao alivyotunga na kuwapa wengine waimbe ni pamoja na Full Shangwe,Domo Kaya vibao vilivyoimbwa na Prince Amigo, Rohombaya haijengi kibao kilichoimbwa na Mwanahawa Ally , Nilijua mtasema kibao kilochoimbwa na Khadija Yusuph, Nipe stara kibao kilichoimbwa na Rahma Machupa, Mtaniona hivi hivi marupe rupe kibao kilichoimbwa na Fatma Mahmoud mcharuko, Sumu mpe paka kibao kilichoimbwa na Mohammed mtu pori a.k.a sharobaro wa jahazi nk.


Mzee Yusuph licha ya kuombwa mara nyingi arudi tena kwenye muziki wa taarabu na mashabiki wake kutokana na muziki huo kudorora siku baada ya siku hatimaye kufa kabisa, Mzee Yusuph bado ameendelea kushikilia msimamo wake wa kutoimba tena muziki huo kwa kuwa unaenda kinyume na mafundisho ya dini kulingana na imani yake ya kiislamu badala yake ameamua kuwafurahisha mashabiki wake ambaye walikuwa na hamu kubwa ya kusikia sauti lakini safari hii ataimba kwa njia ya kaswida na ameshaandaa kibao chake ambacho kinaitwa Mke hutunzwa.


Mbali na taarabu na kaswida Mzee Yusuph pia aliwahi kuimba muziki wa bongofleva kwenye kibao alichoshirikishwa na Chidy Benzi kiitwacho nipe raha za dunia.
 
Back
Top Bottom