Baada ya njia za giza kugonga mwamba kwenye kusaka utajiri, nimeamua kufanya hivi

Kaaaaaaaah asaaalaaaleeee [emoji122] mzebaba polee saanaaa Ilaaaa appo ulikuwa unacheza game na shetani inaweza ikawa shetani anakutahini full mazingaombwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Oky Inaendelea...........

Baada ya kufika pale nikaanza kusukuma mlango bila mafanikio yoyote baada ya kuchunguza vizuri nikagundua kuna mtu amefunga kwa ndani nilisita kutoa sauti maana sikujua aliyekuwa amefunga na mama mwenye nyumba anaweza kishituka gonga sana bila mafanikio yoyote

Wakati nazidi kugonga nikashitukia yule mama yuko nyuma yangu ananiambia nyie vijana wa siku hizi mmeharibika sana sahivi unatoka wapi usiki huu wote basi ikabidi nimwabie natoka prepo ile sijamaliza nikaona mlango umefunguliwa kuangalia vizuri naona ni jamaa yangu agustino

Daa sikutaka niendelee kujibizana na yule mama ikabidi niingie ndani ndio nikamuuliza agustino hivi muda wote ulikuwa wapi akaniambia si nilikuwa humu humu nakuita uje inisaidie wewe umekomaa na yule nguruwe wako

Daa nikamwabia ulikuwa wapi mbona sikukuona mimi sinilikuwa najua kuwa wewe ndio umelala hapo ulikuwa kama umekufa asee akasema yeye alikuwa amelala tu kuamka alikiwa hawezi mpaka wakati nimetoka na yule mnyama nimebeba alijitahidi kuniita lakini mimi nilizidi kuondoka hadi wakati natafuta zile pesa alikuwa ananiambia kwa mdomo lakini mimi nikawa sisikii

Eee nikamuuliza na kule ulipokuwa umeenda kuchimba zile mbegu za maharage alisema alikuta ile sehemu yote inawaka moto ndio akarudi akaona ajilaze kitandani akasikia kitanda kunajoto kwa mbio alizokuwa ikabidi ajilaze sakafuni ndio hakuamka tena hata wakati nimeingia alikiwa ananiona lakini hakuweza hata nyanyua kidole

Nikamwabia hapa kwa huyu mama sio pazuri maana niliwahi kusikia watu wanasema yeye huwa hapangishi raia wa kawaida anapangisha wanafunzi pekee kumbe raia wamesha mshitukia kuwa ni mshirikina

Agustino akasema kesho atapeleka simu kwenye chaji ili amatafute jamaa yake wa shinyanga ili amueleze kilichotupata basi siku hiyo nililala kwa furaha sana nikihisi kama nimeamka kwenye ndoto ya mahuti usingizini kwa misuko suko niliyopitia tena namuona kwa mara nyingine agustino ilikuwa ni bonge la furaha

Basi kesho yake mimi nikamwabia tutafute chumba sehemu nyingine maana hapa pasha kuwa nongwa lakini akasema wewe angalia huu mtaa wote hapa kidogo pana hangalau pako karibu na shule na huduma kama usafiri pako karibia na centre.

Basi nikamkumbusha likizo imeisha ya mwezi tunatakiwa tuanze kwenda shuleni jamaa akasema ngoja kwanza tumalizana kesho na yule jamaa wa shinyanga tujue moja

Basi kesho yake tukaenda centre tukapeleka simu kuchaji maana skuli walikuwa wamedisconnect socket zote basi ikabidi twende tutafute chimbo wanalo uza bangi tukachukua stiki za kutosha tukaenda tukakaa mahali vuta vuta baada ya hapo piga story za utani asee tukaanza kuchekana ila alikuwa akinikumbusha baadhi ya matukio yangu tunabali kucheka sana kama wendawazimi

Basi tukapita tukachukua simu tukaenda kumtafuta yule jamaa agustino akapiga akaeleza kitu kilichotupata yule jamaa alijibu kwa zarau sana kuwa

Kuna watu wameenda kuchuma zile mbegu zilizoota kwenye midomo ya mamba, midomo ya simba yani unakuta simba wanazunguka kwenye lile eneo, kati kati ya moto, wengine wanakuta chati kajizungusha kabisa kwenye lile shimo umalotakiwa kuchuma zile mbegu

Jamaa aliongea kwa hasira acheni ujinga mnachezea utajiri ambao watu wengine wanaulilia nendeni mkazifate hizo mbegu na mkiacha zikikomaa zikaliwa na kitu chochote mtapata shida hadi mtakoma maana hicho ni chakula cha mizimu yaani viti vidogo mnaleta utani

Kisha jamaa akakata simu basi tukakaa kutafakari vile vitisho vya yule jamaa tukaanza kujiuliza tutaenda ila wote tukasema twende tu kwani shingapi

Basi tukasema ganja tulizo kuwa tumebaki nazo tusubirie hadi usiki tuvute ndio akili itakaa vizuri getto tulikuta sola hatuja toa ilibidi tutoe zipate chaji kidogo ya kutumia kwenye mishe zile za usiku

Basi ilivyofika usiku kila mmoja na njia yake tukasema kumbe yale ni majaribu tu ya msimi hata nikiona mamba anakuja kunimeza sikimbii atanikuta niko bize nachuma mbegu zangu zilizoota

Basi nilianza kutembea haraka haraka kuelekea tena kwenye ule muembe cha ajabu siku kuta aina yoyote ya maajabu nilikuta lile jiwe vizuri nikapiga tochi nikayaona yale maua nikasema yess

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Oky tuachane na habari za like tuendelee na story

Sent using Jamii Forums mobile app

yeah...like zako nakushikia..shusha story

napata hisia kama ulikuwa unaota,maana unazungumzia mambo ya kufika shuleni mmida ya saa6 usiku..
~kuonana na mlinzii mida ya saa10 alfajiri...
~wakati wote huna tochi...
~mama mwenye nyumba kukukodolea macho nonstop
~kudeki na kufua night kal
~damu kichuruzika
~usiku kuwa mchana
~kukimbia na mzoga

*maswali ni mengi ila nosweat...

story yako ni tamu; punguza ruti za arusha hasa episode ya mwisho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…