Baada ya njia za giza kugonga mwamba kwenye kusaka utajiri, nimeamua kufanya hivi

Baada ya njia za giza kugonga mwamba kwenye kusaka utajiri, nimeamua kufanya hivi

Duh huu uzi niliusoma kitambo naona Bado ni shule kwa atakae usoma
Nami nausoma naona bado nishule,
Ila memba wa jf wanavsa na Mikasa si ajabu Kuna baadhi ya memba humu wana mapete ya Bahati mixer mvuto, pia Luanda Magere angeumaliza ule Uzi wake ingekuwa poa Sana
 
Halafu Huyo Pusha alikua bwana aangu tukaachana Hivyo alikua anajua ratiba zangu..
Sikh Hiyo akamwaga Mboga ..yaani yule jamaa natamani nikutane nae nimchane Ila sidhani kama nitamkumbuka...
Mh wewe nae Hpn umepambn sana dada bila shaka kwasasa hujaacha ila upo kwenye macocopulp,Betasol na extra clair?

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
dah nmesoma sana ngoja na mimi ntoe kisa kilichosababisha niape kuwa sitakwenda kwa mganga tena kwenye maisha yangu.

ilikuwa 2002,tunatoka dar tunakwenda mkoa wa kigoma kwa wanojua bara bara enzi hizo wanajua ni jinsi gani kulikuwa na majambazi hasa ndani ya mapori ya Tabora,bahati haikuwa yetu mida ya saa 5 usiku wakati tupo road tukakuta bara bara imewekwa bonge la gogo mzee akataka kujitahid aligeuze ghafla walitokea watu wamebeba bunduki ndo kwa mara yangu ya kwanza kuone mtu kashka bunduki huku kajizungushia mkanda wa risasi mwilini bro wangu ile kuwaona tu akakata moto tuliokuwa hatujazmia tulikuwa watatu 3 mimi mzee na bimkubwa.

Tulichezea sana vitasa mzee alidhalilika mno mwisho wa siku walichukua mpka viatu nakumbuka viatu vyangu vya kitoto vya kuwaka taa,then wakaondoka mpka na gari tulikaa pale mpka saa 11 ndo tukapata msaada tukaenda polisi but hawakuwa na msaada mzee akapiga simu kigoma ikatumwa nauli tukaenda moja kwa moja mpka kwa baba yake(means babu),sasa babu yeye kila alivyokuwa anahadithiwa alikuwa anacheka mno hasa akimuangalia bro na ujanja wake ote et kazimia,upande wa baba yeye alikuwa na hasira mno alichokuwa anataka yeye ni wale watu awashikishe adabu hata kufa wafe basi ilivyofika usiku tukaelekea sehemu fulani inaitwa ujiji kwa mzee fulani alikuwa anaitwa juma njemba.

Nadhani kwa watu wa kigoma wanaweza kuwa wanamjua,akaelezewa kila kitu akasema hicho ni kitu kidogo sana,huku na yeye anacheka kisha akasema kuwa pale kwake kuna mbuzi alimchinja sababu ya sherwhe ya mwanae hvyo itatubidi tumtafutie mbuzi mwengne amreplace ili iwe kama malipo yake baba akakubali,kilichofata akawaita wajukuu zake walete (ubumba) ni udongo fulani hivi wa mfinyanzi kisha akawa anatengeneza kimdoli kidogo cha udongo kama vile vya kitoto toto,baada ya kukitengeneza akaanza kukiandika maneno yake kisha akakisimamisha chini,then akaanza kuongea maneno yake aliongea sana baada kama ya saa 1 akasema mtu yoyote ndani ya hichi chumba haruhusiwi kukimbia wala kupiga kelele kwani kwa kufanya hivyo ndo itakuwa kifo chake.

Basi aliendele kusema maneno yake ghafla yule mdoli pole pole alianza kukua na kuwa mkubwa pole pole,baada kama ya dakika arobaini alikuwa ni mkubwa kama binadamu mwenye mwili mkubwa alikuwa anamkono na kifua kikubwa na mrefu,kwa mara ya pili bro tena akazimia kwa mara ya pili mim mkojo ulishantoka natetemeka kama nmepatwa na dege dege,mwisho yule mdoli akaambiwa shtaka letu kisha akaambiwa nenda hivi vitu vinatakiwa leo leo,theb yule mtu akafungua mlango akatoka mbio alikuwa ni mwanaume lakini yupo uchi na ni mweusi tii kama mkaa mpka macho hakuwa na ichi kiini cheupe ye alikuwa na kiini cha moja kwa moja cha weusi,alivyoondoka tukaanza kumpepea na kumwagia maji bro alivyoshtuka yule mzee akatuambia kazi imeshakwisha kesho mtayapata majibu yenu.

Ilivyofika asubuhi tukapigiwa simu nakumbuka enzi hizo kulikuwa kuna buzz siyo hii tigo na hata simu zilikuwa za mezani,tukaambiwa kuwa kuna gari imepatikana Tabora yenye namba kama tuliyoripoti pamoja na vitu vingine,tukaanza safari na treni mpka tabora kufika kule tukakuta vitu vyetu na vingne vingi tu ila mzee alisema vyote vilikuwa vyetu hela zilikuwa kama 1m lakini zilipatikana 7m polisi hawakuchukua hata cent na hata walivyopewa walikataa kata kata hakikupotea hata kifungo kisha baada ya kuchukua tukaambiwa kuwa hao majambazi waliotuibia walikutwa msituni wakiwa wameuwawa wakasema wanahisi ni wanyama wakali ndo waliwauwa maana walikuwa wanaalama za meno makali milini mwao na kucha.

lakini wakashndwa kuelewa kama ni wanyama ndo waliwashambulia ni wanyama aina gani na kwanini hawakuwapiga hata risasi moja hao wanyama na wakati walikuwa na silaha nzito?Baada ya maelezo mengi mzee akawasha gari mpka kigoma stend ya kwanza mpka kwa yule mganga tulinunua mbuzi na zawadi nyingne nying lakini mzee aligoma hakutaka chochote zaidi ya mbuzi tu,basi tukampka mbuzi wake, akasema imebaki kazi moja tu na kazi yenyewe ni kumrudisha yule kiumbe(mdoli mtu)ili asitudhuru na sisi maana ni wetu hapo mdipo ilipokuwa mtihani maana kuna msharti mengi tulikosea plus kujisahau sasa akawa anatuandama sisi atuue dah kila mmoja nyumbani anaalama ya yule kiumbe yangu ni kungatwa skio na kula kipande nikipata mda ntawamalizia kisa changu but mpka leo mimi kwenda kwa waganga ni big no,but thanks god tulitoka salama

picha ya nilipongatwa kwenye skio ambyo ni alama ambayo sitaweza isahau mpka kifo

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
Boss hii story imenivutia sana, naipataje tafadhali.?
 
Back
Top Bottom