Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Mkuu wa Wilaya ya Tanga Japhar Kubecha akiwa ameambatana na Katibu Tawala wa Wilaya ya Tanga Dalmia Mikaya kwa kushirikiana na Taasisi ya Watoto Foundation wamekabidhi madaftari zaidi ya 1000 katika Shule tatu za msingi kwa Wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika Jiji la Tanga.
Akiongea wakati wa kukabidhi madaftari hayo DC Kubecha amesema kuwa dhumuni la kufanya hivyo ni kuunga mkono juhudi za Serikali katika sera ya elimu bila malipo kwa kutoa madaftari yenye picha ya Rais wa Tanzania Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo yatachochea juhudi za Watoto wa kuke kusoma ili kuweza kutimiza ndoto zao..
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Watoto Foundation Ally Pingizi amesema kuwa ugawaji wa madaftari hayo ni harambee ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha Watoto kusoma kwa bidi na kuwa na upendo na Rais Samia.
Madaftari hayo yenye picha ya Rais wamegawa bure kwa Shule ya Pongwe, Majani mapana, na Usagara kwa Watoto wenye mahitaji maalumu na wasio jiweza.