Baada ya Rais Samia kuhudhuria Kariakoo Derby, atakuwa ameshajibu swali la nani hasa aliyeahirisha Mechi ya Mei 8, 2021

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Kwa miaka ya karibuni ukiwa Rais wa Tanzania na ukitaka ujihakikishie sana Kupendwa / Kukubalika na Wananchi anza Kuwapenda Vijana kisha njoo kwa Wasanii wa Muziki Kisha maliza na Wapenda Soka hasa wa Simba na Yanga.

Hata hivyo pamoja na kwamba Rais Samia alihudhuria Mechi ile ya Watani ila Jicho langu kama vile lilinionyesha kuwa Mama si mpenda Michezo (hasa Soka) kwani muda mwingi alikuwa akionekana Kuzubaa zubaa huku akiitesa Shingo yake kwa Kuangalia upande wa Kushoto wa Simba na ule wa Kulia wa Yanga.

Rais Samia alionekana kama vile kutokujua lolote na kuwa Mgeni katika Mpira wa Miguu kwani mara nyingi kuna Njemba Moja hivi (nadhani ya PSU) ilikuwa imekaa Kulia Kwake ndiyo ilikuwa ikimuelezea Mama yale Matukio ya pale Lupaso (Mkapa) Stadium na Mama (Rais) kuonekana akitikisa tu Kichwa chake na Barakoa yake nzuri isiyoambukiza Corona popote pale

Kitu pekee tu ambacho Rais Samia juzi alinifurahisha Binafsi ni kuonyesha Yeye ni Mshabiki wa Timu ipi kwani hata wakati Simba anafungwa Goli la Mazabe (Bahati Nasibu) hakufurahi au hata Kuonyesha Kushtuka kama ambavyo ingekuwa kwa Rais Mstaafu Kikwete.

Na hata wakati Mama anasimama ili kutoka Uwanjani alionekana Kuchukia na Matokeo mpaka alipoombwa Kuupungia upande wa Waliobahatisha Ushindi ambapo aliwapungia kwa Shingo upande tu huku Moyoni mwake na katika Mdomo wake uliokuwa umefunikwa na Barakoa akiwazomea tu Walioshinda na akiwaonya na kuwaonea Huruma kwa Kipigo Kitakatifu ambao Walioshinda wanaenda kukutana nacho huko Mkoani Kigoma tarehe 25 July, 2021.

Mwanaume huwa hatairiwi mara Mbili.
 
Ni kweli mzee ata mi nilishangaaa maana niliona matangazo anzia juzi kuwa mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Maji Mh Uweso wa ile mechi! Gafla Azam wanajiunga nakuja kumuona Mama kakaa jukwaani nikajua tu kuwa huyu mama kweli ndiyo alifanya mpaka ile mechi isogezwe sogezwe ila asirudie tena sio lazima kila kitu aforce mpira atuachie ye akademke kwenye siasa zao.
 
Uo ndio ukweli ndio maana alishindwa kuwafuta watu kazi

Yale yake ya Magufuli nchi kutawaliwa kwa matakwa ya Rais sio katiba na sheria.
 
Kwa miaka ya karibuni ukiwa Rais wa Tanzania na ukitaka ujihakikishie sana Kupendwa / Kukubalika na Wananchi anza Kuwapenda Vijana kisha njoo kwa Wasanii wa Muziki Kisha maliza na Wapenda Soka hasa wa Simba na Yanga.

Hata hivyo pamoja na kwamba Rais Samia alihudhuria Mechi ile ya Watani ila Jicho langu kama vile lilinionyesha kuwa Mama si mpenda Michezo (hasa Soka) kwani muda mwingi alikuwa akionekana Kuzubaa zubaa huku akiitesa Shingo yake kwa Kuangalia upande wa Kushoto wa Simba na ule wa Kulia wa Yanga.

Rais Samia alionekana kama vile kutokujua lolote na kuwa Mgeni katika Mpira wa Miguu kwani mara nyingi kuna Njemba Moja hivi (nadhani ya PSU) ilikuwa imekaa Kulia Kwake ndiyo ilikuwa ikimuelezea Mama yale Matukio ya pale Lupaso (Mkapa) Stadium na Mama (Rais) kuonekana akitikisa tu Kichwa chake na Barakoa yake nzuri isiyoambukiza Corona popote pale

Kitu pekee tu ambacho Rais Samia juzi alinifurahisha Binafsi ni kuonyesha Yeye ni Mshabiki wa Timu ipi kwani hata wakati Simba anafungwa Goli la Mazabe (Bahati Nasibu) hakufurahi au hata Kuonyesha Kushtuka kama ambavyo ingekuwa kwa Rais Mstaafu Kikwete.

Na hata wakati Mama anasimama ili kutoka Uwanjani alionekana Kuchukia na Matokeo mpaka alipoombwa Kuupungia upande wa Waliobahatisha Ushindi ambapo aliwapungia kwa Shingo upande tu huku Moyoni mwake na katika Mdomo wake uliokuwa umefunikwa na Barakoa akiwazomea tu Walioshinda na akiwaonya na kuwaonea Huruma kwa Kipigo Kitakatifu ambao Walioshinda wanaenda kukutana nacho huko Mkoani Kigoma tarehe 25 July, 2021.

Mwanaume huwa hatairiwi mara Mbili.
H vipi?
 
Back
Top Bottom