Baada ya Rais wa Ghana kuingilia Assamoh Gyan abatilisha kustaafu

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,386
Mara baada ya kuibuka taarifa ya kupokwa unahodha wa timu ya Taifa ya Ghana Assamoh Gyan alitangaza kutangaza kuchezea timu ya Taifa kuelekea AFCON 2019 nchini Misri.
Taarifa hizo zilimuibua Rais wa Ghana Nana Addo Akuffo na kumuita kwenye kikao Cha dharura kocha wa timu ya Taifa ya Ghana Kwessi Appiah na kuzungumza nae pia akamuita Gyan kuzungumza nae.
Vikao hivo vimezaa matunda na Sasa Gyan amebatilisha uamuzi wa kustaafu Mara baada ya kurudishiwa unahodha wake kwa msaada wa Rais.
Gyan mwenye miaka 33 anaecheza kwenye falme za kiarabu kwa Sasa ndio mfungaji bora wa Ghana
 
Afrika kila kitu lazima siasa iwemo ndani.

Mfano leo hii eti Bocco astaafu halafu Ngosha aingilie kati na kuishambulia TFF na baadae Bocco anabatilisha uamuzi wake na kurejea timu ya taifa.

Mpira wa bara letu bado una safari ndefu sana katika kile kinachoitwa mafanikio.
 
Ndo Africa hiyo ndugu hapo hata kocha anajiona Hana mamlaka star kamzidi nguvu.
Alafu assume asipomchezesha alafu Ghana wakafungwa kocha atatafuta pakutokea
 
Huyu Gyan ndio yule aliyekosa penati ya muhimu kwenye kombe la dunia 2010? Ilikuwa fursa ya Ghana na Afrika kutinga nusu fainali! Angeachwa tu astaafu........
Ndo huyu huyu jamaa anatabia za kususa Susa alivyokuja ile penati na Uruguay alisema hata piga Tena penati timu ya taifa
 
Gyan angepumzika tu, toka nilIvyomwona kwenye fainali ya caf cup of nations, ambayo walifungwa kwa penalty na Ivory coast. Niliona wazi hakutakiwa kuwepo kikosini, alipata nafasi kisa jina lake na cheo chake cha ukapteni.

Hadi sasa sijaona kuimarika kwake, toka siku ile ambayo aliingizwa kucheza hakufanya cha maana.
 
...siyo Afrika mkuu tu haya hutokea inaonekana hufatilii habari za mpirà kwa taarifa yako Tu Messi pia alishatangaza kustaafu kucheza NT baada kupoteza failnali mbele ya Chile nabaadae Rais alimuita pamoja na chama cha soka cha Argentina na Messi akarudi uwanjani...
 
Ni Scorali pekee alimgomea Rais wa Brazil kumuita Romario mwaka 2002 na Brazil kubeba ndoo
 
Kwaiyo Appiah( kama nitakuwa sahihi jina la kocha wa Ghana) na Asamoh watakuwa makambale wote sharubu. Kila kitu siasa kulinda ukocha na kuheshimika ange resign tu
 
Kuna wadau wanasema "hii ndo afrika"..lakin nakumbuka hata amerika imetokea kwa rais wa argentina kumuhitaj messi tim ya taifa pale alipokua na wazo(kama ckosei) la kuacha kuchezea tim ya taifa.

Kumbuken rais pia ni shabiki kama wewe unavyomuingiliaga maamuz ya amunike kwamba kwann kamuacha flan kwann ajib hayupo, , kwann nyoni hajacheza tatizo tu huna mamlaka ya kumbatilisha maamuz yake ila ungelikua nayo ungelifqnya kama huyo rais wq ghana.

Naunga mkono jitihada za rais kumrudisha asamoah3gyan
 
Kwani atgentina ilikuaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…