Trainee
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 2,660
- 3,501
Salaam wandugu,
Niliwahi kuandika jambo hili kuiomba serikali na kuishauri na leo narudia tena kwa nia ya kukujuza wewe usiyejua ujue kabisa utaratibu ulivyo. Mwishoni kama ada sitaacha kuishauri na kuiomba Serikali itekeleze jambo
Ni kwamba wengi wetu tumezoea tangu mashuleni mwezi wa ramadhani ukiisha tu basi tunatangaziwa "Kesho hatutakuja shuleni kama mwezi ukiandama na keshokutwa mtamalizia idd pili, hivyo tuonane baada ya keshokutwa!" Wakina sisi tusiopenda shule tukawa tunaomba idi iangukie siku ya alhamisi au iambatane na sikukuu zozote za kitaifa ili tuunganishe kawiki ka likizo
Dhana hii imewafanya hata waislamu wenye dini yao waamini kuwa ni kweli kwenye uislamu kuna idd pili. Jambo muhimu unalotakiwa kufahamu ewe muislamu ni kwamba IDD EL FITRI (waswahili wengi wamezoea kuiita idd ndogo) NI MOJA TU! Kama ilivyo thibiti kwa mtume Muhammad swallallaahu alayhi wa sallam na wema wengine wote waliotangulia.
Ukishakula idd kama unaweza anza kufunga siku sita ndani ya mwezi wa shawal (sitat shawwal) na kama huwezi unataka kupumzika basi kula vyakula vyako lakini usiseme idd pili (tena hapa kwenye sita tutoe msisitizo ni kwamba unafunga muda wowote ilimradi iwe ni ndani ya mwezi shawwal)
Idd el adh-ha (wengi wamezoea kuiita idd el hajj au waswahili huiita idd kubwa) ndiyo yenye siku tatu baada yake ambazo zinaitwa siku za tashriik. Siku hizi kwa mujibu wa sheria ya uislamu ndizo ambazo zinajumuishwa na idd hiyo. Kwahiyo tunapata kuona kumbe kama ni idd mosi iddd pili idd tatu...nk ilitakiwa iwe ni kwenye idd ya kuchinja (idd kubwa) na wala si kwenye idd el fitr (idd ndogo)
USHAURI WANGU KWA SERIKALI
Kwa sababu serikali imeamua kuwapa uhuru wa kuabudu wananchi wake basi kwenye swala la idd ndogo ingekuwa watu wanapewa siku zile zile mbili kama kawaida lakini isiwe kama sasa (kwa mtazamo wa idd pili) bali iwe kwa wale wanaowahi kula idd kwa kuangalia muandamo wa mwezi popote duniani na wale wanaofuatia kwa kuangalia muandamo wa mwezi maeneo ya jirani/karibu
Kwa utaratibu uliopo sasa unawanyima uhuru wa kuabudu wale wanaotumia muandamo wa mwezi popote duniani huku wale wa muandamo wa mwezi maeneo husika na maeneo jirani wakipewa siku moja ya bure ya nyongeza ambayo haina tija yoyote. Hivi kwanza ile siku ni nani aliiweka? Mbona pamoja na utofauti wa madhehebu ya waislamu sijaona hata dhehebu moja lenye hiyo siku? Serikali imeifanya siku hiyo kama holiday kwa ajili ya nani/nini?
Kwenye idd kubwa pia hivyo hivyo inatokea kula idd kwa kupishana kwahiyo serikali ingetoa siku mbili au tatu kwa kadiri ionavyo lakini siku hizo zitolewe kwa kuwazingatia wale wanaotangulia kula idd pia!
Wassalaam, nawasilisha