Leo Rostam aziz amejiuzulu nafasi zake zote ndani ya chama na serikali huku siku zilizotolewa na halmashauri zikielekea kuisha, leo rostam kesho ni nani kati ya mapacha wawili waliobaki?
...Nadhani ni muafaka sasa kwa Jakaya Mrisho Khalfan Kikwete (JK) aachie ngazi kama (1) Mwenyekiti wa Chama, (2) Rais wa Mtandao. Sababu ni: kwanza, ni Rostam Aziz aliyemsaidia JK kuingia Ikulu kwa fedha na mbinu za kimtandao akishirikiana na Edo Lowassa na "genge" la mafisadi papa wa mfumo wa CCM na wa ndani ya mfumo wa CCM. Pili, Rostam ndiye aliyeunda mtandao wa "uongozi wa Ikulu" na kulifanya Baraza la Mawaziri kuwa na watu wenye mahusiano ya moja kwa moja na au ya nyuma ya pazia na mafisadi waliyeongoza kampeni ya kuwaingiza wanamtandao kwenye mfumo wa utawala na menejimenti ya serikali kuanzia ngazi za kati na juu ya msonge wa uongozi wa na utendaji wa nchi. Kwa jinsi hiyo, umefika wakati sasa kwa JK (kama ni muungwana) kufuata nyayo za Rostam Aziz (aliyekuwa MNEC na MB wa Igunga).....Kwa kheri Rostam, nenda kafanye biashara zako na uache kuingilia "siasa" kwa kutafuta maslahi binafsi ya kibiashara...!