Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,509
- 3,756
TikTok kwa kushirikiana na Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi imeendesha Mkutano wa kuelezea sera zake ikiwa ni miezi michache tangu Mtandao huo wa Kijamii uzuiwe nchini humo
Mkutano huo uliudhuriwa na Wawakilishi kutoka vitengo mbalimbali kama Vyombo vya Kutekeleza Sheria, Kitengo cha Usalama wa Mtandao, Wizara ya Uchumi wa Dijitali na Wahusika wa ulinzi wa watoto.
Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi iliikaribisha TikTok kwenye mkutano huo huku mtandao huo ukikabiliwa na ongezeko la malalamiko kutoka kwa watumiaji.
Tume ina wasiwasi kuhusu uraibu miongoni mwa watoto na vijana kutokana na Mtandao huo unavyofanya kazi ambapo utendaji wake unawafanya Watumiaji kuutumia kwa muda mrefu.
Imesema hatua hiyo inaweza kusababisha matumizi kupita kiasi, haswa kwa watoto na vijana ambao wanaweza kukosa utambuzi unaohitajika au uwezo wa kujidhibiti ili kupunguza matumizi yao ya programu.
Kwa mujibu wa TikTok, mkutano huu ni sehemu ya dhamira ya TikTok kufanya kazi kwa karibu na washirika wake ili kulinda jukwaa dhidi ya maudhui haramu na kuonyesha dhamira yake ya kukuza usalama mtandaoni.
TikTok ilifafanua kwa wadau, miongozo yake, sera na hakikisho za udhibiti wa maudhui hata hivyo Wadau awakukosa kuhoji mamlaka ya TikTok juu ya njia za kutumia jukwaa wakati wa malalamiko, ripoti au maombi ya habari.
Katika kukabiliana na matatizo haya, Tik Tik ilifafanua kwamba ina watendaji 40,000 wanaohusika na usimamaizi wa maudhui huku wakihakikisha wanalinda na kuheshimu uhuru wa kujieleza kwenye mtandao. Aidha imesema kuwa imeweka njia kadhaa ikiwa ni Pamoja na barua pepe ili kuruhusu wadhibiti wa maudhui wananchi husika au vyombo vya sheria kuweza kuwasiliana nao kutuma maudhui yasiyofaa na wao kushughulikia haraka na kwa ufanisi