wamesahauVipi kuhusu kumuvua ukurugenzi wa wanyamapori enzi zile Prof Alexander Songorwa, hujuma zake kwa waziri wake Balozi Kagasheki?
Jamaa wamekwisha sahau kabisa hasara aloileta Nyarandu ktk wizara ya maliasili na utalii.
umenena ukweli :Jambazi mkubwa. Kuna ile ya tozo la watalii waliokimbilia mahakamani wakashindwa, lakini Nyalandu akakataa amri ya Mahakama ya kuweka tangazo kwenye Government Gazette, ikabaki wazi hadi Bungeni walipolalamika. Mimi kama muasisi wa Chadema nashauri tumkatae huyu ndumilakuwili.
Mlikuwa wapi kuyasema haya ?? Wakiwahama ndo wanakuwa mafisadi ?? Kabla ya kuhama ni wema tu siyo!Wiki iliyopita Waziri wa Maliasili na Utalii, Dr. Hamisi Kigwangalla, akizungumza na wadau wa Wizara yake alisema kuwa baadhi ya mawaziri na wabunge wa awamu ya nne wangepaswa kuwa jela kwa ufisadi na ushiriki wao kwenye ujangili. Leo Nyalandu amekimbia. Ifuatayo ni historia ya kashfa moja ya Nyalandu.
Kampuni ya Kimarekani ya Friedkin Conservation Fund (FCF) ambayo inamiliki kampuni tanzu za uwindaji wa kitalii za Mwiba Holdings Ltd, Tanzania Game Trackers Safaris (TGTS) ni miongoni mwa watuhumiwa wa ujangili
Uchunguzi unaonesha kumekuwapo matukio kadhaa ya wafanyakazi wa Mwiba kukamatwa wakiwa wameua wanyamapori na kukutwa na nyara za Serikali.
Vyanzo vya habari kutoka ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii vimesema mara zote kesi zinazoihusu kampuni hizo zimekwama kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni urafiki wao wa karibu na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Nyalandu.
Urafiki wa Nyalandu na wamiliki wa kampuni hizo ulikuwa mkubwa kiasi cha kumpatia moja ya helikopta zake aitumie kwenye mbio za kuwania urais, kabla ya kushindwa na kujielekeza kwenye ubunge.
Helikopta ya kampuni hiyo ndiyo aliyoitumia wakati wote wa kampeni zake za ubunge
Nyalandu alimwamuru Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori wa wakati huo, Paul Sarakikya, kutoa Leseni ya Rais kwa familia ya Tom Friedkin (mmiliki wa kampuni hizi) kuwinda wanyamapori 700 katika vitalu vinane na eneo la wazi la Makao. Leseni hizo zilitolewa bure bila kulipiwa hata senti.
Miongoni mwa wanyamapori waliokuwa kwenye orodha ya kuuawa ni tembo walio katika hatari ya kutoweka.
Pia Nyalandu alikiuka sheria kwa kupuuza ukomo wa idadi ya vitalu vitano kwa kampuni moja. TGTS imemilikishwa vitalu vinane pamoja na eneo la wazi; hali ambayo ni ukiukwaji wa kifungu cha 38(7) cha Sheria ya Wanyamapori.
Kampuni hiyo pia ilipewa vitalu na Nyalandu kinyemela, ilhali sheria ikiagiza kuwa kitalu kinapobaki wazi sharti kitangazwe kwanza na waombaji washindanishwe katika mfumo na utaratibu ulio wa haki na uwazi [Kanuni ya Uwindaji wa Kitalii 18(1).
Pamoja na kutoa Leseni ya Rais, Wamarekani hao walileta watoto wadogo, chini ya umri wa miaka 18 kuwinda; jambo ambalo ni kinyume cha kifungu cha 43(3) cha Sheria ya Wanyamapori Namba 5 ya mwaka 2009.
FCF na kampuni tanzu imekuwa ikiendesha shughuli za utalii kwenye eneo la Makao WMA tangu 2011 baada ya Mwiba Holdings Ltd kumilikishwa eneo jirani na WMA ya Makao kwa ajili ya shamba la mifugo na wanyama (Makao Ranch).
Kampuni ya Mwiba Holdings Ltd chini ya TGTS Ltd ambazo zinamilikiwa na Friedkin Conservation Fund (FCF) imekuwa ikiendesha shughuli za utalii kwenye eneo la Makao WMA tangu 2011 baada ya Mwiba Holdings Ltd kumilikishwa eneo jirani na WMA ya Makao kwa ajili ya shamba la mifugo na wanyama.
Hata baada ya kumalizika Mkataba wake na JUHIWAPOMA, kampuni ya Mwiba Holdings Ltd iling’ang’ania na kuendelea kukalia eneo la Makao WMA kwa mabavu na kinyume cha sheria.
Tutawaletea moja baada ya nyingine.
Kwahiyo CCM ni chama cha kufuga majizi siyo? Yakiwa CCM, safi tu! Yakitoka ndiyo yanaonekana machafu!!Vipi kuhusu kumuvua ukurugenzi wa wanyamapori enzi zile Prof Alexander Songorwa, hujuma zake kwa waziri wake Balozi Kagasheki?
Jamaa wamekwisha sahau kabisa hasara aloileta Nyarandu ktk wizara ya maliasili na utalii.
hawako safi lakini wametulia sasa huyu ambae anarukaruka wacha apate sindano zake zimuingia vizuriVp kuanzia 2015 hayo mbona hatukusikia!? Na Je vp tuambizane kina maige, kagasheki wao wapo safi!?
Ccm ni wapushkuna na wanafiki wakubwa...
Ni kwa nini haya yaibuke leo?
Leo hata Jaffo ikitokea akihama ccm basi maccm ni lazima yamfanyie fitina!
Kama vipi basi ccm wekeni kashfa za viongozi wote walioko madarakani na waliostaafu.
Ushujaa wa Nyalandu umetukuka , kuleta fyofyoko mbele ya watu wasiojulikana si mchezo .
Hiki kijarida cha kishamba sana !
*Ajisalimisha CHADEMA iliyomtuhumu wizi wa vitalu.
*Wanaharakati na wanaCCM wampuuza.
*Jimboni wasema zama zake zilipendwa.
*Afananishwa na hadithi ya sizitaki mbichi hizi.
Aliyemtuhumu nyalandu kwa madudu yake aliyokuwa anayafanya akiwa waziri wa maliasili na utalii awamu ya jk ( ya 4)hayo yote yangesemwa kabla ya hajajiuzulu hoja ingekuwa na mashiko sana!!! ila kwa sasa hoja hiyo itakuwa haiaminiki,basi kuna uchafu mwingi unafumbiwa macho humo ndani hatuambiwi sababu ya kulindana ila mpaka mtu ajiuzulu ndio muutoe!!
Aliyemtuhumu nyalandu kwa madudu yake aliyokuwa anayafanya akiwa waziri wa maliasili na utalii awamu ya jk ( ya 4)
1.kuua wanyama kwenye mbuga za taifa kupitia kampuni za wazungu
2. Kusafirisha twiga kwenye ndege
3. Kuuza vitalu vya loliondo kinyume cha sheria na taratibu
4. Waliomuita nyalandu ni mzigo kwenye serikali ya jk
Je ni
CCM au CHADEMA???
vipi na nyie mbona hamukumsifia akiwa CCM ?? ndo vita imetangazwa hivyo Mzee tuliaVp kuanzia 2015 hayo mbona hatukusikia!? Na Je vp tuambizane kina maige, kagasheki wao wapo safi!?
Kwa nn na nyie mlikuwa mnamuita mwizi akiwa CCM Leo mnamsafisha ?? wewe ni kada wa chademaWell, lakini kwa nini ccm walikuwa kimya?
Huyu aliyeleta huu uzi ni kada wa ccm!
chama cha fitina ni chadema Lowassa mlimutaje?,nyarandu je si mlisema anauza twiga wetu na akina Lawrence masha si mlisema ni wahuni mpaka ubunge mkataka kumpa ?? fitina hapo ipo wapi chadema au CCM badilikeni msipakazie watu kashfa ambazo hamna ushahidi Nazo...Ccm ni chama cha wafitini, wazandiki, wachawi. N.k wao huwa hawapendi ukweli, bali uongo uliotukuka.