Tetesi: Baada ya Serikali kuanza mahojiano na Nyalandu kuhusu kashfa katika Wizara ya Maliasili na Utalii, atimkia CHADEMA

Tetesi: Baada ya Serikali kuanza mahojiano na Nyalandu kuhusu kashfa katika Wizara ya Maliasili na Utalii, atimkia CHADEMA

Vipi kuhusu kumuvua ukurugenzi wa wanyamapori enzi zile Prof Alexander Songorwa, hujuma zake kwa waziri wake Balozi Kagasheki?
Jamaa wamekwisha sahau kabisa hasara aloileta Nyarandu ktk wizara ya maliasili na utalii.
wamesahau
 
Jambazi mkubwa. Kuna ile ya tozo la watalii waliokimbilia mahakamani wakashindwa, lakini Nyalandu akakataa amri ya Mahakama ya kuweka tangazo kwenye Government Gazette, ikabaki wazi hadi Bungeni walipolalamika. Mimi kama muasisi wa Chadema nashauri tumkatae huyu ndumilakuwili.
umenena ukweli :
 
Wiki iliyopita Waziri wa Maliasili na Utalii, Dr. Hamisi Kigwangalla, akizungumza na wadau wa Wizara yake alisema kuwa baadhi ya mawaziri na wabunge wa awamu ya nne wangepaswa kuwa jela kwa ufisadi na ushiriki wao kwenye ujangili. Leo Nyalandu amekimbia. Ifuatayo ni historia ya kashfa moja ya Nyalandu.

Kampuni ya Kimarekani ya Friedkin Conservation Fund (FCF) ambayo inamiliki kampuni tanzu za uwindaji wa kitalii za Mwiba Holdings Ltd, Tanzania Game Trackers Safaris (TGTS) ni miongoni mwa watuhumiwa wa ujangili
Uchunguzi unaonesha kumekuwapo matukio kadhaa ya wafanyakazi wa Mwiba kukamatwa wakiwa wameua wanyamapori na kukutwa na nyara za Serikali.

Vyanzo vya habari kutoka ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii vimesema mara zote kesi zinazoihusu kampuni hizo zimekwama kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni urafiki wao wa karibu na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Nyalandu.

Urafiki wa Nyalandu na wamiliki wa kampuni hizo ulikuwa mkubwa kiasi cha kumpatia moja ya helikopta zake aitumie kwenye mbio za kuwania urais, kabla ya kushindwa na kujielekeza kwenye ubunge.

Helikopta ya kampuni hiyo ndiyo aliyoitumia wakati wote wa kampeni zake za ubunge
Nyalandu alimwamuru Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori wa wakati huo, Paul Sarakikya, kutoa Leseni ya Rais kwa familia ya Tom Friedkin (mmiliki wa kampuni hizi) kuwinda wanyamapori 700 katika vitalu vinane na eneo la wazi la Makao. Leseni hizo zilitolewa bure bila kulipiwa hata senti.

Miongoni mwa wanyamapori waliokuwa kwenye orodha ya kuuawa ni tembo walio katika hatari ya kutoweka.

Pia Nyalandu alikiuka sheria kwa kupuuza ukomo wa idadi ya vitalu vitano kwa kampuni moja. TGTS imemilikishwa vitalu vinane pamoja na eneo la wazi; hali ambayo ni ukiukwaji wa kifungu cha 38(7) cha Sheria ya Wanyamapori.

Kampuni hiyo pia ilipewa vitalu na Nyalandu kinyemela, ilhali sheria ikiagiza kuwa kitalu kinapobaki wazi sharti kitangazwe kwanza na waombaji washindanishwe katika mfumo na utaratibu ulio wa haki na uwazi [Kanuni ya Uwindaji wa Kitalii 18(1).

Pamoja na kutoa Leseni ya Rais, Wamarekani hao walileta watoto wadogo, chini ya umri wa miaka 18 kuwinda; jambo ambalo ni kinyume cha kifungu cha 43(3) cha Sheria ya Wanyamapori Namba 5 ya mwaka 2009.

FCF na kampuni tanzu imekuwa ikiendesha shughuli za utalii kwenye eneo la Makao WMA tangu 2011 baada ya Mwiba Holdings Ltd kumilikishwa eneo jirani na WMA ya Makao kwa ajili ya shamba la mifugo na wanyama (Makao Ranch).

Kampuni ya Mwiba Holdings Ltd chini ya TGTS Ltd ambazo zinamilikiwa na Friedkin Conservation Fund (FCF) imekuwa ikiendesha shughuli za utalii kwenye eneo la Makao WMA tangu 2011 baada ya Mwiba Holdings Ltd kumilikishwa eneo jirani na WMA ya Makao kwa ajili ya shamba la mifugo na wanyama.

Hata baada ya kumalizika Mkataba wake na JUHIWAPOMA, kampuni ya Mwiba Holdings Ltd iling’ang’ania na kuendelea kukalia eneo la Makao WMA kwa mabavu na kinyume cha sheria.

Tutawaletea moja baada ya nyingine.
Mlikuwa wapi kuyasema haya ?? Wakiwahama ndo wanakuwa mafisadi ?? Kabla ya kuhama ni wema tu siyo!
 
Vipi kuhusu kumuvua ukurugenzi wa wanyamapori enzi zile Prof Alexander Songorwa, hujuma zake kwa waziri wake Balozi Kagasheki?
Jamaa wamekwisha sahau kabisa hasara aloileta Nyarandu ktk wizara ya maliasili na utalii.
Kwahiyo CCM ni chama cha kufuga majizi siyo? Yakiwa CCM, safi tu! Yakitoka ndiyo yanaonekana machafu!!
 
Vp kuanzia 2015 hayo mbona hatukusikia!? Na Je vp tuambizane kina maige, kagasheki wao wapo safi!?
hawako safi lakini wametulia sasa huyu ambae anarukaruka wacha apate sindano zake zimuingia vizuri
 
yaani katika watu wooote kigwangala? kigwangala huyu huyu? kigwangala...jaman nasi tufikie hatua tuwe tunatumia akili hata kidogo siyo makalio tu.unaweza kweli ukamkimbia kigwangala???????????????????? why? huyu kigwangala huyu huyu? propaganda za kipuuzi kabisa na za kitoto kuwah kutokea ni kama hizi. na kwani kamkimbia walikuwa wanakaa room moja?au nyumba moja kusema sasa ameona andoke amwachie nyumba?
 
Ccm ni wapushkuna na wanafiki wakubwa...
Ni kwa nini haya yaibuke leo?
Leo hata Jaffo ikitokea akihama ccm basi maccm ni lazima yamfanyie fitina!
Kama vipi basi ccm wekeni kashfa za viongozi wote walioko madarakani na waliostaafu.

Ndio maana wanabaki kwa sababu ya woga na sio utashi. Ukibahatika kukaa na mawaziri wa JPM wanamponda kwelikweli wakiwa naye meno njenje......
 
Saidi mdogo sna kwa lazalo... mfumo wa jk uliweka mizizi mirefu... sasa john anahangaika kuichoma sasa ana vita mbili moja na edward plus ukawa huku team jk plus benard mpk 2020 itafika john anapambana na hizi team asipokua makin
 
689ef543c257256882ca95208e4cfc42.jpg

*Ajisalimisha CHADEMA iliyomtuhumu wizi wa vitalu.
*Wanaharakati na wanaCCM wampuuza.
*Jimboni wasema zama zake zilipendwa.
*Afananishwa na hadithi ya sizitaki mbichi hizi.
 
nadhani angebaki CCM ndio angekuwa amemkimbia lakini kwa kuhamia CHADEMA ndio kajiingiza kwenye mtego!
 
Hivi wa-TZ na hasa walio kunywa maji ya bendera za vyama siasa nani amewaroga? Siku zote mwanasiasa akiwa upande wenu ni mzuri na atasifiwa kwa kila jambo. Hutasikia kashfa toka chamani hata kama amefanya ufisadi au uovu mchana kweupe. Zaidi sana utaona watu wakitokwa povu kumtetea. Haya sasa Nyalandu katoka CCM, leo tunasikia kila uovu wa ukweli na uongo ukiwemo uzushi unaletwa humu. Mbona alipokuwa huko hayakusemwa haya? Na wengine (i.e., Upinzani) waliposema walizodolewa kwamba ni wazushi. Leo Nyalandu kaamua kujitakasa, imekuwa nongwa. Najaribu kuwaza tu, hivi ikitokea Mh. Magufuli akihamia upinzani, sitashangaa hao hao wanaomsifia leo kumgeuka kwamba aliuza nyumba za serikali kwa maslahi binafsi, alifisadi kwenye mabarabara bila kusahau kaliingizia taifa hasara kupitia kashfa ya samaki wa magufuli, makinikia nk. Ndugu zanguni tuache ukigeu geu!
 
hayo yote yangesemwa kabla ya hajajiuzulu hoja ingekuwa na mashiko sana!!! ila kwa sasa hoja hiyo itakuwa haiaminiki,basi kuna uchafu mwingi unafumbiwa macho humo ndani hatuambiwi sababu ya kulindana ila mpaka mtu ajiuzulu ndio muutoe!!
 
hayo yote yangesemwa kabla ya hajajiuzulu hoja ingekuwa na mashiko sana!!! ila kwa sasa hoja hiyo itakuwa haiaminiki,basi kuna uchafu mwingi unafumbiwa macho humo ndani hatuambiwi sababu ya kulindana ila mpaka mtu ajiuzulu ndio muutoe!!
Aliyemtuhumu nyalandu kwa madudu yake aliyokuwa anayafanya akiwa waziri wa maliasili na utalii awamu ya jk ( ya 4)
1.kuua wanyama kwenye mbuga za taifa kupitia kampuni za wazungu
2. Kusafirisha twiga kwenye ndege
3. Kuuza vitalu vya loliondo kinyume cha sheria na taratibu
4. Waliomuita nyalandu ni mzigo kwenye serikali ya jk
Je ni
CCM au CHADEMA???
 
Ccm ni chama cha wafitini, wazandiki, wachawi. N.k wao huwa hawapendi ukweli, bali uongo uliotukuka.
 
Aliyemtuhumu nyalandu kwa madudu yake aliyokuwa anayafanya akiwa waziri wa maliasili na utalii awamu ya jk ( ya 4)
1.kuua wanyama kwenye mbuga za taifa kupitia kampuni za wazungu
2. Kusafirisha twiga kwenye ndege
3. Kuuza vitalu vya loliondo kinyume cha sheria na taratibu
4. Waliomuita nyalandu ni mzigo kwenye serikali ya jk
Je ni
CCM au CHADEMA???

Kwanza watu ni wasauhulifu sana; aliyepandisha twiga kwenye ndege ni Maige na si Nyalando. Maige bado yupo ccm na hamsemi kashfa yake? Na bado kwao msafi? Akiondoka hii itamrudia?
 
Ccm ni chama cha wafitini, wazandiki, wachawi. N.k wao huwa hawapendi ukweli, bali uongo uliotukuka.
chama cha fitina ni chadema Lowassa mlimutaje?,nyarandu je si mlisema anauza twiga wetu na akina Lawrence masha si mlisema ni wahuni mpaka ubunge mkataka kumpa ?? fitina hapo ipo wapi chadema au CCM badilikeni msipakazie watu kashfa ambazo hamna ushahidi Nazo...
 
Back
Top Bottom