Tetesi: Baada ya Serikali kuanza mahojiano na Nyalandu kuhusu kashfa katika Wizara ya Maliasili na Utalii, atimkia CHADEMA


Watz nimeamini kwa majungu tunaoongoza.Mtu akiishatangaza kuhama kambi fulani tayari kuna kundi kubwa humu ndani kazi yao ni kutengenza threads za kuchafuana lkn akiwa na madaraka ndani ya vyama hivyo hakuna anayesema mabaya yao.kwa kweli si ustaarabu na si hulka yetu watz.hali hii naiona jinsi tunavyosonga mbele inazidi kupata kasi ya ajabu.kwa nini tunapenda kuwadhalilisha watu wengine wanapoamua kufanya maamuzi wanayotaka?
Inasikitisha sana humu ndani wanajf jinsi wanavyomshambulia nyarandu wengine wameenda mbali zaidi kiasi cha kumualia nini afanye.tuachane na hizo negativity na tuwe realistic tunapojadili mambo.tuwajadili watu kwa uzuri na tuachane na tabia ya kuchafuana ktk mitandao hii haina afya kwetu kabisa.tujifunze siasa kutoka kwa majirani zetu ndo maana watu tumechoka hata kusoma magazeti ya tz sababu hata uandishi wake hauna afya na maslahi kwa nchi bali ni wa chuki tu.
 
Moja ya kitu kibaya zaidi kwa maisha ya mwanadamu ni woga, woga humfanya mwanadamu aishi maisha ya kinyonge mpaka anaingia kaburini
 
Why now, bado keshawapiga goli ccm nijuavyo Mimi akiguswa lazima na Kikwete aguswe. Katiba mbovu huzaa majanga
 
ni upumbavu usio na kifani mtu akiwa ccm msafi akitoka mwizi
 
Mlikuwa wapi kumchafua wakati mko naye, leo amekataa kula sahani moja ndo mnatuletea tupicha picha tu, siku hizi picha zinapikwa hivyo katafute ushahidi mwingine utuletee wa tofauti na hako kapicha, kwani hiyo picha imekosa nini wakati kaipiga public mbele za watu au unaona yuko na huyo chumbani?
 
Mkuu ukisema nyalandu kamkimbia kigwangala.
Utakuwa unakosea.

KWANI NYALANDU AMEKIMBIA NCHI?
SI YUPO HAPA HAPA?

Sasa kamkimbia vipi?
Naomba ufafanuzi tafadhali.
Ufafanuzi ni kwamba alikokimbilia kuna watetezi wa UFISADI.
 
Yaani mkae na mbunge jangili kwa miaka miwili hamumshitaki, halafu leo kaondoka mnaanza? Hapo mmekosea timing, lolote mtakalofanya ni uonevu tu.
Ndio maana tunasema CCM haiwezi kupambana na ufisadi. Leo Ngeleja amerudisha mabilioni yake ya Escrow lakini amesamehewa, siku akihama chama kesi zinafufuliwa.
 
Mimi ni mkazi wa Arusha mjini na nilishawahi nunua kiwanja kule Sanawari ya Juu Arusha jirani na alikojenga Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu jumba kubwa na nafikiri anaishi humo kwa sasa na amebase Arusha badala ya Singida au Arusha na Dar kama walivyo wabunge wengi wa CCM na upinzani.

Tusishangae 2020 Nyalandu akigombea ubunge Arusha Magharibi kama atashindwa Urais kupitia CDM.

Nashauri tu tunapojadili siasa na wanasiasa tusizame sana kuwatetea maana hatuwajui wala hatutawajua unless wewe nawe ni mwanasiasa au mnufaika wa siasa chafu za TZ
 

AnayoHAKI kujenga Tanzania popote apendapo ila hana haki ya kufanya ubadhirifu,kama kuna kesi ya UFISADI au UBADHIRIFU rukhsa kumshataki
 
Facebook ndiyo source ya hizo taarabu zako alfu mbona avatar yako upo kama jike au sio riziki mkuu?
 
Amekimbia kesi zake huyu anataka kujificha nyuma ya chadema ili wananchi waseme anaonewa kwa kua kahama chama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…