Tetesi: Baada ya Serikali kuanza mahojiano na Nyalandu kuhusu kashfa katika Wizara ya Maliasili na Utalii, atimkia CHADEMA

Tetesi: Baada ya Serikali kuanza mahojiano na Nyalandu kuhusu kashfa katika Wizara ya Maliasili na Utalii, atimkia CHADEMA

Wiki iliyopita Waziri wa Maliasili na Utalii, Dr. Hamisi Kigwangalla, akizungumza na wadau wa Wizara yake alisema kuwa baadhi ya mawaziri na wabunge wa awamu ya nne wangepaswa kuwa jela kwa ufisadi na ushiriki wao kwenye ujangili. Leo Nyalandu amekimbia. Ifuatayo ni historia ya kashfa moja ya Nyalandu.

Kampuni ya Kimarekani ya Friedkin Conservation Fund (FCF) ambayo inamiliki kampuni tanzu za uwindaji wa kitalii za Mwiba Holdings Ltd, Tanzania Game Trackers Safaris (TGTS) ni miongoni mwa watuhumiwa wa ujangili
Uchunguzi unaonesha kumekuwapo matukio kadhaa ya wafanyakazi wa Mwiba kukamatwa wakiwa wameua wanyamapori na kukutwa na nyara za Serikali.

Vyanzo vya habari kutoka ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii vimesema mara zote kesi zinazoihusu kampuni hizo zimekwama kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni urafiki wao wa karibu na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Nyalandu.

Urafiki wa Nyalandu na wamiliki wa kampuni hizo ulikuwa mkubwa kiasi cha kumpatia moja ya helikopta zake aitumie kwenye mbio za kuwania urais, kabla ya kushindwa na kujielekeza kwenye ubunge.

Helikopta ya kampuni hiyo ndiyo aliyoitumia wakati wote wa kampeni zake za ubunge
Nyalandu alimwamuru Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori wa wakati huo, Paul Sarakikya, kutoa Leseni ya Rais kwa familia ya Tom Friedkin (mmiliki wa kampuni hizi) kuwinda wanyamapori 700 katika vitalu vinane na eneo la wazi la Makao. Leseni hizo zilitolewa bure bila kulipiwa hata senti.

Miongoni mwa wanyamapori waliokuwa kwenye orodha ya kuuawa ni tembo walio katika hatari ya kutoweka.

Pia Nyalandu alikiuka sheria kwa kupuuza ukomo wa idadi ya vitalu vitano kwa kampuni moja. TGTS imemilikishwa vitalu vinane pamoja na eneo la wazi; hali ambayo ni ukiukwaji wa kifungu cha 38(7) cha Sheria ya Wanyamapori.

Kampuni hiyo pia ilipewa vitalu na Nyalandu kinyemela, ilhali sheria ikiagiza kuwa kitalu kinapobaki wazi sharti kitangazwe kwanza na waombaji washindanishwe katika mfumo na utaratibu ulio wa haki na uwazi [Kanuni ya Uwindaji wa Kitalii 18(1).

Pamoja na kutoa Leseni ya Rais, Wamarekani hao walileta watoto wadogo, chini ya umri wa miaka 18 kuwinda; jambo ambalo ni kinyume cha kifungu cha 43(3) cha Sheria ya Wanyamapori Namba 5 ya mwaka 2009.

FCF na kampuni tanzu imekuwa ikiendesha shughuli za utalii kwenye eneo la Makao WMA tangu 2011 baada ya Mwiba Holdings Ltd kumilikishwa eneo jirani na WMA ya Makao kwa ajili ya shamba la mifugo na wanyama (Makao Ranch).

Kampuni ya Mwiba Holdings Ltd chini ya TGTS Ltd ambazo zinamilikiwa na Friedkin Conservation Fund (FCF) imekuwa ikiendesha shughuli za utalii kwenye eneo la Makao WMA tangu 2011 baada ya Mwiba Holdings Ltd kumilikishwa eneo jirani na WMA ya Makao kwa ajili ya shamba la mifugo na wanyama.

Hata baada ya kumalizika Mkataba wake na JUHIWAPOMA, kampuni ya Mwiba Holdings Ltd iling’ang’ania na kuendelea kukalia eneo la Makao WMA kwa mabavu na kinyume cha sheria.

Tutawaletea moja baada ya nyingine.
Useless!!! Eti kuna jamaa anabwabwaja anapigana na rushwa wakati mwenyewe anashiriki kununua madiwani
 
Kumbu kumbu zangu zinaniambia kuwa waliokuwa wakiibua shutuma za ufisadi wa Nyalandu ni upinzani....haswa masuala ya vitalu......
Sio kumbukumbu zako tu. Jamiiforum imejaa records hizo za wapinzani dhidi ya Lazaro Nyalandu. Tusitegemee kamwe mabadiliko ya maana katika siasa za kitanzania. Mtu yeyote mwenye tuhuma za ufisadi akiwa CCM, akiona upepo mbaya kwake anakimbiia CHADEMA na huko atasafishwa na tuhuma dhidi yake kuzikwa. Ni afadhalli mara miamoja CCM waendelee kutawala maana tunawajua na wakigombana wanaumbuana na kufukuzana kuliko wapinzani fake, waongo na uchwara.
 
IMG_20171031_174803_206.jpg
 
Kukimbia huko amehama nchi?.... Kama ana kosa kisheria huko alikohamia hawezi kushughulikiwa?... Alipokuwa CCM hayo hayakuwa makosa mpaka baada ya kuhama?...
Kazi mnayo, wataondoka wengi tu, anza kuorodhesha makosa yao kabisa.
 
Nitasikitika kuona Mtu Mkubwa akiwa na madhambi yanakuwa Siri akiwa Ndani ya CCM,Na Wana CCM tukiwa tunajua vema ama tukiwa na or evidence hatuzitoi ! Akituhama tu ndipo tunasema sana kwanini unafiki huu?Ni waombe wana CCM Tusifiche madhambi ya Watu bila kujali ni Wa CCM au la Tufuate Nyayo za M\kiti Wetu wa Taifa CCM tutumbuane bila kujali nyadhifa zetu jifunzeni kwangu najitolea mfano na nitazidi kuwa hivyo, kuna ujambazi ulitokea 2015April20 kaya 19 tulivamiwa kwa Bahati njema kaya yangu ilikuwa ya Mwisho kuvamiwa siku hiyo nilibahatika kutambua Mmoja mwa Majambazi nilitoa Taarifa Police wakafanya Uchanguzi wao hadi kesi Mahakama ya Wilaya nikawa Shahidi wa kwanza Mhimu kutoa ushahidi Jambazi huyo alipondua kuwa ataenda jela alijitahidi kuwatumia Viongozi wa CCM Wamsaidie kuzima kesi ikiwa ngumu hadi alikubali kuomba msamaha kwa kuwa sikuwa fahamu wenzie nilikubali Wazee 6 walishiriki kusululuhisha bada ya kusikia pande zote Wajomba zake walimuamua anilipe Tsh 500,000/= cash alikubali akalipa na kusainiana barua za Msamaha alioomba Nasikitika ilitafutwa mbinu ya kumbeba na kumpa Uongozi Ndani ya Chama CCM ingawa Nami ni CCM ila msimamo Wangu unajulikana Wala sita sema ubaya wa Mtu pale anapohama na kwenda upande fulani Ebu tufunguke tuwaseme wa baya bila kujali wana nyadhifa gani? Jamani tufunguke
 
Vipi kuhusu vichwa vya treni?

Au ufisadi ule mlio udhibitisha mbele ya vyombo vya habari,fisadi lake mmelisahau?

DOUBLE STANDARDS
 
Kinacho tushangaza ni kwa nini hamkushughulikia kwa hii miaka yenu miwili ya hapa kasi tuu
Hata lowasa mlisema hivo hivo!
Swali la msingi aliyewatuhumu kuwa ni wafisadi ni CHADEMA wenyewe au mnajitoa ufahamu?
 
Yan mpk mtu ahame ndio maovu yake yanaonekana, mimi sio mwendawazimu wa kufuata siasa za ushabiki km simba na yanga
 
Vipi kuhusu vichwa vya treni?

Au ufisadi ule mlio udhibitisha mbele ya vyombo vya habari,fisadi lake mmelisahau?

DOUBLE STANDARDS
CCM kuwa na MAFISADI ni normal.
Kinachoudhi ni MAFISADI hayo yanapojikusanya kuja kunajisi chama chetu huku!
 
Vipi kuhusu kumuvua ukurugenzi wa wanyamapori enzi zile Prof Alexander Songorwa, hujuma zake kwa waziri wake Balozi Kagasheki?
Jamaa wamekwisha sahau kabisa hasara aloileta Nyarandu ktk wizara ya maliasili na utalii.
Sio kwamba wamesahau,ila wameishajitangazia kwenda kinyume cha serikali iwe mbaya au nzuri,sijui sababu ya kunywa maji ya chupa hayana virutubisho vya asilia.
 
Kuandika majina tu ya Nyalandu umeshindwa sasa sijui hayo maneno mengine hapo chini utakuwa umeandika nini

Na wewe eti ni kiumbe wa Lumumba unayetaka kutuonyesha ni mjenga hoja mzuri

Anyway katiba inaruhusu wewe kutoa maoni yako ila chonde chonde jua hadhira unayo kusuduia kuufikishia ujumbe wako

Naona aibu mimi kwa hichi ulicho andika
 
Kuandika majina tu ya Nyalandu umeshindwa sasa sijui hayo maneno mengine hapo chini utakuwa umeandika nini

Na wewe eti ni kiumbe wa Lumumba unayetaka kutuonyesha ni mjenga hoja mzuri

Anyway katiba inaruhusu wewe kutoa maoni yako ila chonde chonde jua hadhira unayo kusuduia kuufikishia ujumbe wako

Naona aibu mimi kwa hichi ulicho andika
HICHI ULICHOANDIKA!
 
Mimi fisadi kweli, endelea kushindia vitumbua na kubeba magazeti hapo Lumumba na nikipita na Range langu uendelee kusema jamaa noma sana dah ni tajiri wakati wewe soksi tu za 500 zimetoboka

Mada imehamishwa vipi? Si umesema soon mafisadi wote watashitakiwa mimi nikakuambia hiyo mahakama ya mafisadi mtafugia mbuzi ama nguruwe

Hivi mnalishwa nini hapo Lumumba?
nyie mafisadi wa CHADEMA tutawafunga muda si mrefu siku zenu zinahesabika
 
*BAADA YA SERIKALI KUANZA MAHOJIANO NA RAZALO NYARANDU KUHUSU KASHFA MBALIMBALI KATIKA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII RASMI ATIMKIA CHADEMA.*

Baada ya Serikali ya awamu ya Tano kuanza kushughulikia kashfa mbalimbali zilizofanywa na baadhi ya viongozi waliokua madarakani katika awamu zilizopita za uongozi tayari baadhi ya watu waliobanwa na Serikali kwa kashfa hizo wameanza kuhamia upinzani hususani CHADEMA ili kuandaa mazingira ya kuonekana wameonewa baada ya kufikishwa Mahakamani.

Duru za ndani ya Serikali zinadai kuwa toka Mh. John Pombe Magufuli amechaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Nyarandu amekua katika Wakati Mgumu akihojiwa kuhusu Mikataba Mbalimbali ya Kifisadi iliyisainiwa katika Kipindi ambacho amehudumu kama Waziri wa MALIASILI NA UTALII.

Baada ya kuhojiwa na Vyombo mbalimbali na kujiridhisha pasipo na shaka kuwa Mh. Nyarandu aliingia mikataba mibovu na baadhi ya Makampuni ya Kigeni kwa maslahi yake binafsi ikiwa ni Pamoja na uuzaji wa Vitalu vya Uwindaji Pamoja na kashfa nzito ya Kupandisha ndege Twiga wa Tanzania na kuuza raslimali mbalimbali za Taifa ndipo Serikali ilipochukua maamuzi ya Kumfikisha Mh. Nyarandu Mahakamani.

Katika Kufanikisha adhima hiyo Wiki kadhaa zilizopita Mh. Rais alimteua Mh. Hamis Kigwangala kuwa Waziri wa MALIASILI NA UTALII ambaye ameanza kwa kufuta leseni zote za Uwindaji zilizotolewa na Mh. Nyarandu kwa makampuni ya Kigeni kwa misingi ya Rushwa. Baada ya kuvunjwa kwa mikataba hiyo na kurudisha Serikalini baadhi ya Vitalu vya uwindaji Mh. Nyarandu amekua katika Wakati Mgumu kwani wawekezaji aliosaini nao mikataba wamembana wakitaka arejeshe mara moja pesa zao Pamoja na fidia kwani ameonekana aliwatapeli kwa kuwahakikishia kuendesha Shughuri zao Nchini katika njia za Unyonyaji.

Kwa hiyo kutokana na shinikizo alilonalo toka kwa Makampuni hayo ya Kigeni na Kwa namna serikali ilivyodhamilia kumfikisha Mahakamani kwa makosa ya Uhujumu uchumi ameamua kukimbilia Upinzani ili atakaposhitakiwa ionekan Upinzani Nchini Tanzania unaonewa.

Baadhi ya Makada wakongwe ndani ya Chadema waliotoa maoni yao wameonyesha kuchukizwa kwao na jinsi watu wenye kashfa za Ufisadi wanavyokimbilia kwenye chama chao.

Ninadhani sasa huu ni mtego, kama tutampokea chama chetu litakua chaka la kupokea Mafisadi alisikika akisema Kiongozi mmoja mwandamizi ndani ya Chadema.

*_Je Chadema watampokea Nyarandu wakijua kuwa atafikishwa Mahakamani muda wowote kujibu tuhuma za Ubadhilifu, kuitia Nchi hasara na kufanya ufisadi mkubwa?_*

Tuendelee kusubiri Kuona maamuzi ya Chadema kuhusu Nyarandu.

I think wawe wanapeleka shule kwanza kuwafundisha namna ya kuandika, kabla hamjaanza kutoa maoni.

Mjue kutofautika kati ya “R”na “L”

Otherwise buku 7000 zinapotea bure.
 
Mtu asiyejua tofauti ya r na l inakuwa tabu sana kumchukulia kama mtu makini.
 
Back
Top Bottom