Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 17,047
- 63,206
Siku za hivi karibuni serikali imeonekana kuacha kuweka msisitizo juu ya mapambano dhidi ya Korona, Si waziri mkuu wala Waziri wa Afya wala mganga mkuu wa serikali wameonekana kuja mbele kuendelea kuukumbusha umma kuwa tuna hali ya hatari. Hawatoi tena updates ya waliopona, walioambukizwa, vifo n. k
Nimepita katika mji wa Dar, ningependa kuwaeleza kuwa ile ari ya kupambana na Korona ni kama vile imeanza kupungua, siyo kama ilivyokuwa kipindi kile Ummy Mwalimu anakuja kila siku kutoa updates, Vijiwe vya soga vimeendelea kama kawaida huku vijana wengi wakiwa hawana barakoa na walionazo wamezishusha chini ya videvu.
Hapo mwanzo wananchi walikuwa na mwamko mkubw sana wa kuweka ndoo za maji kunawa, sasa hivi mwamko huo nao umepungua, waliokuwa wananunua Sanitizers wameanza sasa kununua sabuni tena zisizo na ubora wa kuuwa virusi, na wale ambao uwezo wao ulikuwa kununua sabuni sasa hivi wanaweka maji matupu.
Kiufupi it seems kuwa gharama za kuucontain huu ugonjwa utagharimu uchumi maradufu ya ule tuliokuwa tukihofia kuupoteza laiti tungelichukua hatua za kuhami huu ugonjwa usisambae nchini.
Nilichojifunza ni kwamba wananchi bado wanahitaji leadership ya kila siku kwenye hili janga. Serikali ikirelax nao wanarelax.
Sijui waziri mkuu yuko wapi, lakini bila shaka hili linamhusu maana kitengo cha maafa kiko chini yake.
Kassim Majaliwa hebu toka huko uliko uwe kama kawawa Simba wa Vita, Onyesha uongozi.