Narumu kwetu
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 1,888
- 4,489
Kwa wapinzani Iran, kuporomoka kwa utawala wa Bashar al-Assad ni muhimu kwa sababu Syria imekuwa msingi wa kimkakati kwa Iran katika kanda hiyo. Baada ya anguko la Assad huko Syria, je utawala wa Iran pia utaanguka?
p.dw.com
Matukio nchini Syria yaibua wasiwasi kote Iran, hata kumfanya Khamenei kutoa taarifa kwa umma.
Matangazo
Kuporomoka kwa utawala wa Bashar al-Assad nchini Syria, kumepokelewa kwa mchanganyiko wa matumaini na tahadhari. Wengi wa wapinzani ndani ya Iran waliokatishwa tamaa na utawala wao wa kimabavu wa uongozi wa Kiislamu, wanalinganisha uwiano kati ya mapambano yao na ya watu wa Syria.
Kwa raia wengi wa Iran, Syria imekuwa msingi wa mkakati wa kikanda wa Tehran, ikiashiria sio tu ushawishi wa kijiografia lakini pia mfano wa pamoja wa ustahimilivu dhidi ya utawala wa kimabavu.
Kwa hivyo, matukio ndani ya Syria yanahisiwa katika nyanja zote ikiwemo ya kijamii na kisiasa ndani ya Iran.
Kuondolewa kwa Assad kumefufua matumaini miongoni mwa Wairani wapinzani, kuhusu uwezekano wa kutokea mabadiliko nchini mwao, hasa baada ya serikali ya Iran kulikandamiza kikatili vuguvugu lililotetea haki na uhuru wa wanawake. Ukandamizaji uliosababisha vifo vya mamia na maelfu ya wengine kufungwa jela.
Baada ya Syria, je, utawala wa Iran utafuata na kuanguka? – DW – 17.12.2024