Baada ya tamko lingine la Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania; Je, ni wakati muafaka kwa Serikali kutathimini upya mahusiano yake na taifa hilo?

Hizi ni chuki za waziwazi,hatuwezi kufata kila kitu wanavyotaka wao,huko kwao ndio kwenye hatari zaidi na naona kila leo maandamano,Hebu watuachie ya kwetu wapambane na hali yao kwanza,kama hali ni mbaya warudi makwao mpaka hali itakapokua sawa.
 
Hali ni mbaya okay sikupingi,hebu tutanabaishe hali mbaya nyanja gani?
Sisemi kwa undani sasa ila mtaona baadaye, twende pamoja. Nimeishi na hawa watu muda mrefu wa maisha yangu, wako very systematic na wanafuatilia viji mambo vidogo vidogo sana ilimradi vinawahusu au vinawagusa. Kwa tukio la Mbowe wameguswa zaidi na sasa wanachukua hatua ya juu zaidi kwani tukio hili limejirudia, rejea tukio la Lissu na wamesema hapa chini tayari:

 
Wametumia neno "presumed" na neno jingine "could". Hawa jamaa ni wajanja na hizo statements huwa zinapitiwa na lawyers before hazijatoka.

Hakuna grounds za kuwabana after all hiyo release imewalenga raia wao na sio Mtanzania wa kwa mtogole aliyeambiwa achape kazi tu kwani corona haipo tena
 
Hapo watamkomoa kweli,ila uko STATE watakua wanajisumbua tu.
Soma waraka wao wa kulaani tukio la Mbowe hapo juu, ndio mambo yanaanza pole pole hivyo na kwa kuwa jiwe hashauriki basi tutaona movie mbeleni.
 
Haya matukio mkuu hayajaanza kutokea leo,na yataendelea kutokea,kwa utashi atuwezi amini kila kitu moja kwa moja,pia swala la mbowe liko na nadharia nyingi.Turudi kwenye mzizi wa mada.
 
Wapo hapa kuwalinda raia wao..na wao kwa info walizo nazo wameona bado kuna high risk mkoa wa dsm..sasa unataka wasiwape taarifa wananchi wao waliopo tz..tambua kila nchi inajukumu la kulinda raia wake..mahali popote walipo.

#MaendeleoHayanaChama

 
Mkuu unaeza ona wamewalenga raia wao,lakini hizi taarifa zao ambazo hazina uhakika pia zinawafikia na mataifa mengine,matokeo yake inapelekea kuendelea kuathiri sekta ya utalii na nadhani hilo ndio lengo lao kuu kutudhofisha kiuchumi,wanapenda kutuona tuki fail,tuendelee kukopa
 
CCM wamechonga barua na kuisambaza kuwa Ubalozi wa Marekani umeomba msamaha kutokana na kutoa taarifa kuhusu Mbowe
 
Mkuu unaeza ona wamewalenga raia wao,lakini hizi taarifa zao ambazo hazina uhakika pia zinawafikia na mataifa mengine..
Dawa ya kuwajibu hao ni kutoa taarifa za COVID tu kama tunahofia mataifa mengine hawatakuja

 
mtu anayeweza kujitamkia anayotaka ikiwamo kupotosha hata maandiko matakatifu, utamwamini kwa lipi?

"Daniel alimezwa na samaki" - by anonymous

"Saddam ni rais wa Kuwait" - by anonymous
 
Nyerere alilifungia taifa linalojinasibu kama taifa teule la Mungu, maisha yaliendelea kama kawaida, taifa letu limebaki kuwa imara na lenye amani ukanda wetu mzima.

Hakuna cha taifa teule wala taifa laaniwa, marekani wawachukue raia wao wakaandamane huko, TZ maisha yetu yanaendelea kwenda mbele jana leo daima na milele.

Hata hivyo hao jamaa kwenye mikataba ya kupewa hizo nafasi watakuwa wanaji commit mambo fulani ambayo lije jua ije mvua lazima wayatimize, ni wakupuuzwa tu hao na mabandiko yao.

Kwangu mimi Tanzania ni bora kuliko U.S.A, Magufuli ananifaa kuliko Trump. Wa hapa hapa mimi sitishiki.
 
Wapuuzi hao kwasababu tu kunyaland bado inaburuzika na covid-19
 
Utakuwa na hofu isiyo na sababu na unatumia hofu yako kutisha watu. Tusubiri kama US watafunga ofisi hapa kisa hiyo CORONA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…