Baada ya tamko lingine la Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania; Je, ni wakati muafaka kwa Serikali kutathimini upya mahusiano yake na taifa hilo?

Baada ya tamko lingine la Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania; Je, ni wakati muafaka kwa Serikali kutathimini upya mahusiano yake na taifa hilo?

Hakuna nililokuza, ubalozi wa Marekani ndio unakuza mambo kwa nini wanasema "The risk of contracting COVID-19 remains high" hii kauli utaona itakavyochukuliwa na wote wanaopingana na hatua ambazo serikali imechukuwa kupambana na hili janga, utaona taarifa kutoka vyombo kama BBC zikianza kumiminika, hii ni mbaya kwa taswira ya taifa letu. Kama hali ni mbaya kwa nini viongozi mara nyingi wajisifu kwa kutokuvaa barakoa ? Huko mtaani kwenu ni watu wangapi wanavaa barakoa ? Ni tahadhari gani hasa zinachukuliwa hivi sasa ? Maisha yanaendelea kama kawaida lakini taarifa hizi zinakinzana na kauli rasmi kutoka kwa viongozi wakuu wa nchi. Inamaana kama wanachosema ni ukweli, viongozi wetu wameamua kututoa kafara ? Lazima kuwe na uwajibikaji kutokana na kutolewa kwa taarifa kama hii, sio kuikalia kimya. Tanzania ni nchi huru.
Hizi ni chuki za waziwazi,hatuwezi kufata kila kitu wanavyotaka wao,huko kwao ndio kwenye hatari zaidi na naona kila leo maandamano,Hebu watuachie ya kwetu wapambane na hali yao kwanza,kama hali ni mbaya warudi makwao mpaka hali itakapokua sawa.
 
Hali ni mbaya okay sikupingi,hebu tutanabaishe hali mbaya nyanja gani?
Sisemi kwa undani sasa ila mtaona baadaye, twende pamoja. Nimeishi na hawa watu muda mrefu wa maisha yangu, wako very systematic na wanafuatilia viji mambo vidogo vidogo sana ilimradi vinawahusu au vinawagusa. Kwa tukio la Mbowe wameguswa zaidi na sasa wanachukua hatua ya juu zaidi kwani tukio hili limejirudia, rejea tukio la Lissu na wamesema hapa chini tayari:

1591889776243.png
 
Wametumia neno "presumed" na neno jingine "could". Hawa jamaa ni wajanja na hizo statements huwa zinapitiwa na lawyers before hazijatoka.

Hakuna grounds za kuwabana after all hiyo release imewalenga raia wao na sio Mtanzania wa kwa mtogole aliyeambiwa achape kazi tu kwani corona haipo tena
 
Hapo watamkomoa kweli,ila uko STATE watakua wanajisumbua tu.
Soma waraka wao wa kulaani tukio la Mbowe hapo juu, ndio mambo yanaanza pole pole hivyo na kwa kuwa jiwe hashauriki basi tutaona movie mbeleni.
 
Sisemi kwa undani sasa ila mtaona baadaye, twende pamoja. Nimeishi na hawa watu muda mrefu wa maisha yangu, wako very systematic na wanafuatilia viji mambo vidogo vidogo sana ilimradi vinawahusu au vinawagusa. Kwa tukio la Mbowe wameguswa zaidi na sasa wanachukua hatua ya juu zaidi kwani tukio hili limejirudia, rejea tukio la Lissu na wamesema hapa chini tayari:

View attachment 1475243
Haya matukio mkuu hayajaanza kutokea leo,na yataendelea kutokea,kwa utashi atuwezi amini kila kitu moja kwa moja,pia swala la mbowe liko na nadharia nyingi.Turudi kwenye mzizi wa mada.
 
Wapo hapa kuwalinda raia wao..na wao kwa info walizo nazo wameona bado kuna high risk mkoa wa dsm..sasa unataka wasiwape taarifa wananchi wao waliopo tz..tambua kila nchi inajukumu la kulinda raia wake..mahali popote walipo.

#MaendeleoHayanaChama

Hakuna nililokuza, hakuna sehemu niliyosema ugonjwa umekwisha ila ubalozi wa Marekani ndio unakuza mambo kwa nini wanasema "The risk of contracting COVID-19 remains high" hii kauli utaona itakavyochukuliwa na wote wanaopingana na hatua ambazo serikali imechukuwa kupambana na hili janga, utaona taarifa kutoka vyombo kama BBC zikianza kumiminika baadaye, hii ni mbaya kwa taswira ya taifa letu. Unajua shida ambazo Wizara ya Maliasili na Utalii wanapitia kujaribu kuleta watalii hapa nchini ?

Kama hali ni mbaya kwa nini viongozi mara nyingi wajisifu na kusifu watu katika mikutano ya hadhara kwa kutokuvaa barakoa ? Huko mtaani kwenu ni watu wangapi wanavaa barakoa ? Ni tahadhari gani hasa zinachukuliwa hivi sasa ? Maisha yanaendelea kama kawaida lakini taarifa hizi za Ubalozi zinakinzana na kauli rasmi kutoka kwa viongozi wakuu wa nchi. Inamaana kama wanachosema ni ukweli, viongozi wetu wameamua kututoa kafara ? Lazima kuwe na uwajibikaji kutokana na kutolewa kwa taarifa kama hii, sio kuikalia kimya. Tanzania ni nchi huru.
 
Wametumia neno "presumed" na neno jingine "could". Hawa jamaa ni wajanja na hizo statements huwa zinapitiwa na lawyers before hazijatoka.

Hakuna grounds za kuwabana after all hiyo release imewalenga raia wao na sio Mtanzania wa kwa mtogole aliyeambiwa achape kazi tu kwani corona haipo tena
Mkuu unaeza ona wamewalenga raia wao,lakini hizi taarifa zao ambazo hazina uhakika pia zinawafikia na mataifa mengine,matokeo yake inapelekea kuendelea kuathiri sekta ya utalii na nadhani hilo ndio lengo lao kuu kutudhofisha kiuchumi,wanapenda kutuona tuki fail,tuendelee kukopa
 
CCM wamechonga barua na kuisambaza kuwa Ubalozi wa Marekani umeomba msamaha kutokana na kutoa taarifa kuhusu Mbowe
 
Mkuu unaeza ona wamewalenga raia wao,lakini hizi taarifa zao ambazo hazina uhakika pia zinawafikia na mataifa mengine..
Dawa ya kuwajibu hao ni kutoa taarifa za COVID tu kama tunahofia mataifa mengine hawatakuja

93C330EA-EEBE-4953-B46E-6EDFEA3E2EC8.jpeg
 
Tarehe 11/06/2020 Ubalozi wa Marekani umetoa tamko lingine linaloelezea ongezeko la maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 nchini Tanzania, na kuwashauri raia wake kukaa ndani na kuachana na mizunguko isiyo ya lazima. Taarifa hii inafuatia tahadhari mbali mbali ambazo imekuwa ikizitoa tangu ugonjwa huu kufika nchini Tanzania ambazo zilipelekea kaimu balozi wa Marekani nchini Tanzania kuitwa na serikali ya Tanzania na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje. Serikali ya Tanzania ilieleza kusikitishwa na namna Ubalozi wa Marekani umekuwa ukitoa taarifa ya hali ya maambukizi ya ugonjwa huo zisizo sahihi zinazoweza kuzua taharuki kwa Watanzania na wageni kutoka nje ya nchi. Pia serikali ilimtaka kaimu balozi wa Marekani kutoa taarifa zilizothibitishwa na kuwa hakuna kizuizi serikalini kwa mabalozi kupata "taarifa sahihi na zenye ukweli."

Baada ya taarifa hiyo kwa mara mbili mfululizo Ubalozi wa Marekani umeendelea kutoa taarifa zinazokinzana na kauli ya serikali, Rais amehakikishia wananchi wake kuwa ugonjwa umepungua sana na kuwasifu watu wengi anaokutana nao kwa kutokuvaa barakoa, ikiwa ni kielelezo kuwa hali ya hatari ya maambukizi imepungua na inaelekea kuisha Tanzania. Wakati huo huo ubalozi wa Marekani umekuwa ukielezea kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa huo hatari na kuwasihi raia wake kusalia ndani ama kuondoka nchini Tanzania mara moja pale usafiri wa ndege utakapopatikana.

Vile vile Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umesema kuwa wakati wowote mlipuko utakapozidi hospitali zetu zitazidiwa na hivyo kuna uwezekano wa Raia wake kukosa huduma kutoka vituo vya afya, lakini Waziri wa Afya amenukuliwa akiwa Dodoma na kusema kuwa hakuna hata mgonjwa mmoja kwenye vituo vingi vya afya walivyokuwa wametenga kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa hao, na kusisitiza yeye mweyewe hajavaa barakoa kwa sababu hali ni shwari. Kuongezea hilo alisema kuwa kuna zaidi ya mikoa 15 ambayo haina wagonjwa wa Corona.

Tumekuwa tukiambiwa na Rais kuwa ugonjwa huu ni vita na mabeberu wamekuwa wakitufanyia hujuma bila kuambiwa hasa mabeberu ni akina nani, lakini kutokana na mkinzano huu inaonekana kabisa wale mabeberu wanaweza kuwa ni nchi ya Marekani. Kama hizi taarifa ubalozi wa Marekani unazotoa kwa kukaidi ushauri wa serikali yetu, je kuna haja gani ya kuendelea kuwabembeleza ? Tumekuwa tukiaminishwa kuwa sisi ni nchi tajiri na tuna uwezo wa kusimama wenyewe bila kuyumbishwa na msimamo wa mabeberu, kwa nini serikali isiangalie upya mahusiano na taifa la Marekani ? Ikumbukwe nchi ipo katika hatua za kujaribu kunusuru sekta ya utalii na matamko kama haya yanarudisha nyuma juhudi za serikali na wizara yake husika, kwa kupunguza imani kutoka kwa watalii.

Kama serikali ikiendelea kukaa kimya na kuacha ubalozi ufanye unachotaka, tunahatarisha sekta ya utalii na hata wananchi wanaweza kupata taharuki, kwa maana inawezekana taarifa hizi zinaukweli ndani yake, ni wakati muafaka ubalozi wa Marekani kuomba msamaha kwa kutoa taarifa potofu, ama serikali iutake ubalozi kufungashsa virago na kutuachia nchi yetu yenye amani na afya tele. Na kama serikali ikishindwa kukemea matamko haya basi ijitokeze hadharani na kueleza kwa nini inashindwa kukemea uovu huo unaofanywa na mabeberu, pengine taarifa zao ni za ukweli.

View attachment 1475216
mtu anayeweza kujitamkia anayotaka ikiwamo kupotosha hata maandiko matakatifu, utamwamini kwa lipi?

"Daniel alimezwa na samaki" - by anonymous

"Saddam ni rais wa Kuwait" - by anonymous
 
Nyerere alilifungia taifa linalojinasibu kama taifa teule la Mungu, maisha yaliendelea kama kawaida, taifa letu limebaki kuwa imara na lenye amani ukanda wetu mzima.

Hakuna cha taifa teule wala taifa laaniwa, marekani wawachukue raia wao wakaandamane huko, TZ maisha yetu yanaendelea kwenda mbele jana leo daima na milele.

Hata hivyo hao jamaa kwenye mikataba ya kupewa hizo nafasi watakuwa wanaji commit mambo fulani ambayo lije jua ije mvua lazima wayatimize, ni wakupuuzwa tu hao na mabandiko yao.

Kwangu mimi Tanzania ni bora kuliko U.S.A, Magufuli ananifaa kuliko Trump. Wa hapa hapa mimi sitishiki.
 
Wapuuzi hao kwasababu tu kunyaland bado inaburuzika na covid-19
Tarehe 11/06/2020 Ubalozi wa Marekani umetoa tamko lingine linaloelezea ongezeko la maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 nchini Tanzania, na kuwashauri raia wake kukaa ndani na kuachana na mizunguko isiyo ya lazima. Taarifa hii inafuatia tahadhari mbali mbali ambazo imekuwa ikizitoa tangu ugonjwa huu kufika nchini Tanzania ambazo zilipelekea kaimu balozi wa Marekani nchini Tanzania kuitwa na serikali ya Tanzania na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje. Serikali ya Tanzania ilieleza kusikitishwa na namna Ubalozi wa Marekani umekuwa ukitoa taarifa ya hali ya maambukizi ya ugonjwa huo zisizo sahihi zinazoweza kuzua taharuki kwa Watanzania na wageni kutoka nje ya nchi. Pia serikali ilimtaka kaimu balozi wa Marekani kutoa taarifa zilizothibitishwa na kuwa hakuna kizuizi serikalini kwa mabalozi kupata "taarifa sahihi na zenye ukweli."

Baada ya taarifa hiyo kwa mara mbili mfululizo Ubalozi wa Marekani umeendelea kutoa taarifa zinazokinzana na kauli ya serikali, Rais amehakikishia wananchi wake kuwa ugonjwa umepungua sana na kuwasifu watu wengi anaokutana nao kwa kutokuvaa barakoa, ikiwa ni kielelezo kuwa hali ya hatari ya maambukizi imepungua na inaelekea kuisha Tanzania. Wakati huo huo ubalozi wa Marekani umekuwa ukielezea kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa huo hatari na kuwasihi raia wake kusalia ndani ama kuondoka nchini Tanzania mara moja pale usafiri wa ndege utakapopatikana.

Vile vile Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umesema kuwa wakati wowote mlipuko utakapozidi hospitali zetu zitazidiwa na hivyo kuna uwezekano wa Raia wake kukosa huduma kutoka vituo vya afya, lakini Waziri wa Afya amenukuliwa akiwa Dodoma na kusema kuwa hakuna hata mgonjwa mmoja kwenye vituo vingi vya afya walivyokuwa wametenga kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa hao, na kusisitiza yeye mweyewe hajavaa barakoa kwa sababu hali ni shwari. Kuongezea hilo alisema kuwa kuna zaidi ya mikoa 15 ambayo haina wagonjwa wa Corona.

Tumekuwa tukiambiwa na Rais kuwa ugonjwa huu ni vita na mabeberu wamekuwa wakitufanyia hujuma bila kuambiwa hasa mabeberu ni akina nani, lakini kutokana na mkinzano huu inaonekana kabisa wale mabeberu wanaweza kuwa ni nchi ya Marekani. Kama hizi taarifa ubalozi wa Marekani unazotoa kwa kukaidi ushauri wa serikali yetu, je kuna haja gani ya kuendelea kuwabembeleza? Tumekuwa tukiaminishwa kuwa sisi ni nchi tajiri na tuna uwezo wa kusimama wenyewe bila kuyumbishwa na msimamo wa mabeberu, kwa nini serikali isiangalie upya mahusiano na taifa la Marekani? Ikumbukwe nchi ipo katika hatua za kujaribu kunusuru sekta ya utalii na matamko kama haya yanarudisha nyuma juhudi za serikali na wizara yake husika, kwa kupunguza imani kutoka kwa watalii.

Kama serikali ikiendelea kukaa kimya na kuacha ubalozi ufanye unachotaka, tunahatarisha sekta ya utalii na hata wananchi wanaweza kupata taharuki, kwa maana inawezekana taarifa hizi zinaukweli ndani yake, ni wakati muafaka ubalozi wa Marekani kuomba msamaha kwa kutoa taarifa potofu, ama serikali iutake ubalozi kufungashsa virago na kutuachia nchi yetu yenye amani na afya tele. Na kama serikali ikishindwa kukemea matamko haya basi ijitokeze hadharani na kueleza kwa nini inashindwa kukemea uovu huo unaofanywa na mabeberu, pengine taarifa zao ni za ukweli.

Kwani bashite alifungiwa kwenda Marekani kwasababu ya nini? Na wewe bwana unaona corona ni tatizo dogo?... upo kama viongozi wako. Corona inamaanisha kila kitu, uchumi, biashara, na zaidi uhai wa watu. Serikali inapocheza na corona namna hii inamaanisha wageni wanashindwa kufanya biashara na kazi zao. Unaona sasa ubalozi unakuwa kwenye hatari pamoja na mabalozi na wafanyakazi wengine wengi ambao ni raia wa Marekani. Pia hii inaifanya Tz kuwa chimbuko la corona hata pale nchi nyingine zitakuwa zimetokomeza corona. Kwasababu ya corona?...
Utakuwa na hofu isiyo na sababu na unatumia hofu yako kutisha watu. Tusubiri kama US watafunga ofisi hapa kisa hiyo CORONA
 
Back
Top Bottom