Baada ya Trump, Bilionea Namba Moja Duniani Elon Musk anafikiria kuja na mtandao wake wa kijamii

Baada ya Trump, Bilionea Namba Moja Duniani Elon Musk anafikiria kuja na mtandao wake wa kijamii

The Assassin

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2018
Posts
4,942
Reaction score
20,077
Baada ya Trump kuzundua mtandao wake wa kijamii mwezi uliopita, Tajiri Elon Musk anafikiria kuzindua mtandao wake mpya ambao utawapa watu uhuru kamili wa kutoa maoni.

Ikumbukwe kwamba hata Trump analaumu kwamba mitandao iliyopo inaminya uhuru wa watu kujieleza, inapangia watu waandike nini waache nini.

Elon pia anasema mitandao ya kijamii kama Twitter imekuwa sio salama tena kwa kutoa maoni huru.

Watu kibao wanamshauri ainunue Twitter ili aipe uhuru kamili na watu watoe maoni wanavyotaka ama azindue mtandao wake mpya.

Tusubiri tuone.

 
Jamaa wa hovyo sana yani media zao ndo utopolo kabisa Cnn Bbc Sky newz hazina tofauti na tbc
 
Kwani wa trump unaitwaje? Mbona hata mleta mada inaonekana huujui?? [emoji848]
 
Freedom of speech, kimsingi inajengwa kisheria kisha kusimamiwa kitaasisi. Kwa nchi ambazo uminywaji wa uhuru wa maoni unatekelezwa na mamlaka za nchi (state), hata kama kukiwa na uanzishwaji wa mtandao mwingine wa kutoa maoni, nao utakutana na vikwazo vilevile.
 
Kwa nini asiinunue jamii forum na kutuliberate kutoka kwenye mikono ya mods wahuni
 
Huyu musk anajionaga mungu mtu. Ni freemason wa ajabu sana. Yani anajionaga yuko juu ya dunia kwasababu tu ya mabilion yake machache na magari yake uchwara ya umeme tesla na li space x yake ambayo inachafua mazingira anga za juu.

Simpendi
 
Huyu musk anajionaga mungu mtu. Ni freemasonry wa ajabu sana. Yani anajiona yuko juu ya dunia kwasababu tu ya mabilion yake machache na magati yake uchwara ya umeme tesla la space x yake ambsyo inachafua mazingira anga za juu.

Simpendi
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kila chombo kinachoundwa kinakuwa na sera yake na hawawezi ku-compromise sera yao ili kukidhi matakwa ya mtu au kikundi fulani cha watu.

Hata hao wanaotaka kuunda mitandao yao hawawezi kuziendesha bila sera ambazo pia bado kuna wengine hawatazifurahia kihivyo.

Hakuna mtandao utakaundwa duniani ambao utakuwa na sera ambazo zitakubalika na watu wote duniani na hata kwenye nchi za kipolisi kama Russia na China hizo za kwao ndio takataka kabisa ambapo watumiaji hutakiwa kuzisifu tu mamlaka wakati wote.
 
Back
Top Bottom