Baada ya tukio la Jumamosi, Putin, Lukashenko na Prigozhin wameuthibitishia ulimwengu kwamba wao ni "gangsters" halisi na Russia si nchi ya kuichezea

Wewe ulisoma wapi, hata kufanya summary tu huwezi. Bure kabisa.
 
Moja ya waandishi JF ambao naweza soma post yake ikiwa ndefu hata kama gazeti la the guardian kuanzia mwanzo hadi mwisho bila kuacha nukta wala koma.. Asante sana mkuu kwa chambuzi zako zenye akili.
 
Urusi n dubwana ambalo NATO wanashindwa kulisoma, walianza na vikwazo , wakataka mapinduzi SASA mbinu ipi imebaki kuisambalatisha urusi. Je warusi wamelala usingizi au ndo wameamshwa na kiongozi wa Wegner
 
Prigoziny na Putin wote wanatoka S. Petersburg ( Real Russian), Shoigu anatoka Tuva Eastern Russia Siberian. Putin anamlea Prigoziny kwa kuwa ni wanyumbani, ata akilopoka Putin ukaa kimya. Shoigu ndio amejitengenezea nafasi ya uridhi wa nchi Putin akiondoka, hii inawaogopesha Warusi asiria( Prigoziny, Surovikin, Gerasimov, na Waziri Mkuu wa Urusi), Nani atairidhi nchi baada ya Putin?, ndio kinachogombaniwa hapo. Sababu Shoigu ni Jamii ya Wa Tubal wanatokea Tuva karibu na mpaka wa nchi ya Mongolia na Urusi, na Warusi hawapendi mtu asie Mrusi asilia kutawala Urusi( Kumbuka Walivyomchukia Joseph Stalin M Georgia alipotawala Urusi baada ya Lenin). Putin anatimiza malengo yake ya Kuifanya Urusi kuwa nchi ya kuogopwa na yenye nguvu, lakini wapambe wake Prigoziny, Surovikin, Shoigu, Gerasimov, wanapambana kujinufaisha ili wapate ukuu. Kitakachofuata, ni Prigoziny atajijenga Kule Belarus kumkabili Shoigu kwa Pesa za Waberalus, na Shoigu atajijenga upya kumkabili Prigoziny, watajifanya kuelewana, kutakua makundi 2 katika jeshi la Urusi kichini chini, Shoigu/ Chechinia/Siberian Vs Prigoziny/ Surovikin/Real Russian. Wote watasubiri vita vingine vijavyo iwe Putin yupo au Hayupo, watauana na kugawana Mbao nchi ya Urusi. Chachinia, Dagestan, Ingushetia, Siberian kila jamii na lugha zitaachana. Kumbuka mafuta mengi yanatoka Siberia kwa Shoigu. Hakuna vita tena Kati ya NATO na Russia, lakini kutakua na vita kati ya Washirika wa Russia (Iran, Palestine, Syria, Turkey, China) Vs Washirika wa NATO ( Israel na Taiwan), Russia na Belarus watapeleka vikosi vya kukodi na Siraha nyingi. Dunia itagawanyika(Unipolar world).

Sent from my TECNO B1g using JamiiForums mobile app
 
Kwa jinsi unavyoji shebedua unaonekana kichwani mweupeeee kama sembe
 
kuna wamba wako nyuma ya putin hao ndo hatari kuna mwamba anaitwa roman abramovich
 
Kumfsnanisha rais na gangster si sifa nzuri.

Sent from my SM-S908U1 using JamiiForums mobile app
Gangster ni mwamba.

Lukashenko ni mwamba pia, miaka miwili nyuma aliwahi kutuma ndege ya kivita ya Belarus ilokuwa ndani ya anga la Belarus ikielekea Lithuania na kuirudisha ndege ya shirika la ndege la Ireland ya Rynaair mjini Misnk bila majibu ya NATO.

Ndege hiyo ilikuwa imembeba mwandishi wa habari na blogger Roman Protasevich ambae alikuwa na DOCUMENTS muhimu ambazo Lukashenko alizihitaji.

Nchi za NATO hazikujaribu hata chembe ya kuingilia zoezi hilo ambalo Lukashenko alituma ndege za kivita za Mig-29.

Sanasana walokifanya ni kuongeza vikwazo vya kiuchumi kwa Belarus kupitia baraza la EU.

Hili halikuwa tukio la kawaida na liliwastua karibu nchi nyingi za EU kwani hazikutarajia Lukashenko kuamuru zoezi hilo. Marubani kwa ndege za Mig-29 waliambiwa wahakikishe ndege hiyo haiingii anga la NATO lakini ndege ya Rynaair tayari ilikuwa karibu na mji mkuu wa Vilnius nchini Lithuania ambayo ni mwanachama wa NATO.

Hawa jamaa ni miamba si watu wa mchezomchezo.
 
Lukashenko akiamua kukuua wewe sasa hivi kwa sababu ana nguvu za kufanya hivyo, na hakuna atakayemsimamisha, utakubali na kupenda hilo?
 
Lukashenko akiamua kukuua wewe sasa hivi kwa sababu ana nguvu za kufanya hivyo, na hakuna atakayemsimamisha, utakubali na kupenda hilo?
Hawa watu ni " smarter upstairs" huwa hawafikirii hayo.

Pia yategemea na kesi kama za wasaliti huwa ni "fast trucked" na vijana wa kazi hutumwa popote pale ulipo duniani.

Watu wamefuatwa mmoja kanywa chai ya rangi na mwingine akawekewa poda kwenye kitasa hawa waliitwa wasaliti.

Mimi hapa nilipo Kibaigwa hata hawafahamu huyu Richard ni nani.

Richard Who?
 
Ngoja Watakuja kukwambia uwawekee ka~summary kidogo maana ni ndefu
Uchambuzi au kwa kiingereza huitwa analysis ni uchambuzi wa kina (detailed examination) juu ya mambo kadhaa (elements) kile ulokiona au kukisikia.

Hivyo nimetizama mahojiano ya raisi Lukashenko na waandishi wa habari na kisha nimekuja na analysis yangu ambayo yaweza kuwa mafungu kadhaa (paragraphs) ya maneno.

Hivyo ndivyo nilivyofanya.
 
Umeshindwa zoezi rahisi la fikra za kidhahania.
 
Russia is a mafia state, hili lipo wazi tu, ila huu uasi mfupi umemuaibisha sana Putin (strong man) na kuonyesha hana udhibiti wa kila kitu huko Moscow.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…