Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Nimetoka hapo Tegeta one time, wakati naperuzi peruzi hapo ndio nikaipata hii.
Ni kwamba baada ya tukio lile la TRA sasa hivi kila siku polisi wanaenda maeneo hayo saa nne usiku, ukikutwa unazubaa zubaa hapo hakuna cha msalia mtume, wanakubeba kama mtuhumiwa na wewe unaingizwa kwenye kesi.
Majuzi wanasema polisi walienda mchana na difenda wakiwa na boda watatu ambao wamechakazwa kwa kipigo, walipofika pale boda walikuwa wananyoosha vidole tu kwa bajaji na boda waliokuwa hapo, walioangukiwa na vidole wakasombwa. Kwa mazingira hayo its obvious mtu ananyoosha mkono tu apate ahueni ya vipigo.
Pia soma: Jeshi la Polisi linawashikilia watu 4 kwa tuhuma za mauji ya Mtumishi wa TRA Amani Simbayao kutoka tukio la Tegeta
Kwahiyo ni mwendo wa kubambikiwa kesi tu. Boda na bajaji sasa hivi wako mguu sawa hapo, ikikaribia saa nne watu wanajiondokea kwa hofu ya kujumuishwa kwenye sakata hilo.
Sasa hivi ukipata tatizo maeneo hayo hata ufanye nini hupati msaada kwa terror iloyosambazwa hapo.
Huu ni uonevu wa hali ya juu, na mnatengeneza bomu jingine watu waanze kuvizia polisi na kuwawahi kabla hawajawahiwa. Hivi ndio mnafanya uchunguzi kwa kufosi kukamata watu hovyo na kubambikia kesi?
Mngekuwa mnatumia nguvu hii kukamata wasiyojulikana wlkwenye matukio lukuki yaliyotokea nchini tusingefika huku.
Fanyeni kazi kwa weledi na si huu uhalifu mnafanya, mnazidi kuharibu na kubomoa badala ya kujenga.