Baada ya Tume ya uchaguzi kuvuka lengo la uandikishaji wapiga kura CCM kutoa semina elekezi kwa viongozi wake wa serikali za mitaa

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mambo mawili makubwa yamejitokeza hivi karibuni kwanza CCM imeshinda uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kishindo, pili Tume ya taifa ya uchaguzi imevuka lengo kwa kuandikisha wapiga kura wengi kuliko ilivyotarajiwa.

Hii maana yake ni kuwa uchaguzi mkuu wa 2020 utakuwa na wapiga kura zaidi ya milioni 29 hii ni historia.

Kwa kuliona hilo CCM inatarajia kutoa semina elekezi kwa viongozi wake wa serikali za mitaa ikiwa ni matayarisho ya kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu.

Ikumbukwe kuwa wananchi wengi wamejiandikisha kupiga kura baada ya kuridhishwa na maendeleo yanayoletwa na serikali ya awamu ya 5 na kwa mara ya kwanza tangu tupate Uhuru watanzania wameanza kuona thamani ya kura zao.

Hongereni CCM.

Maendeleo hayana vyama!
 
Nimeamini kama hukubaliki hata ujipake manukato hutoboi. Juzi mtendaji wa mtaa wetu kaitisha kikao kujitambulisha na kujadili maendeleo, hayo mahudhurio ni aibu.

Yeye na wapambe wake wakaishia kusema kwa sauti kubwa kuwa wao ndio waliochaguliwa, na kama kuna wengine tulikuwa tunawataka walijitoa hivyo tufanye kazi na yeye kwakuwa yuko tayari.

Alipoona inafika jioni idadi bado ni ndogo sana, akawa anasema mtu aliyetokea kwenye kikao hata akipata matatizo asiende hapo ofisini. Hapo nikawa najiuliza hiyo wanayosema wanakubalika ndio ipo hiyo?
 
tindo,
Nilidhani hamkuhudhuria kabisa!!

Kuhudhuria kwenu ndio kukubalika kwenyewe.

Maendeleo hayana vyama!
 
Ukiona baba wa familia kila dakika anasema yeye ndo baba ndo mwanaume anza kuwa na wasiwasi sana, kuwa baba au mwanaume ni majukumu tu na uwajibikaji wako unakutangaza na kuwataarifu wengine kuwa ww ni nani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Funguka zaidi bwashee!
Baba anaanza kutangaza mm ndo ninaewalisha humu ndani mm ndo nalipa bili zote humu ndani na upovu unamtoka mdomoni kuelezea hayo lazima uingie wasiwasi mkuu, ila inakulazima kuwa mpole nakusema ndiyo ni kweli na kumsaidia zaidi utasema kama sio ww kiukweli hata shule tusingeenda na tungetembea uchi lakin ya moyon unajua mwenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilidhani hamkuhudhuria kabisa!!

Kuhudhuria kwenu ndio kukubalika kwenyewe.

Maendeleo hayana vyama!

Mimi sikuhudhuria bali walikuwa karibu na kwangu. Waliohudhuria ni aibu, ilikuwa kama kikao cha ukoo.
 
tindo,
Tanapa mna tabu sana
Mtendaji hapigiwi kura,anaajiriwa na manispaa,huyo mtendaji aliekwambia amechaguliwa labda ni mashinji,halafu ulijuaje wakati umenuna?
Endelezeni dhihaka na bezo,sie tunazidi kukanyaga mafuta,mkistuka muda umeisha,mnatangaza kususa
 
Hii id na Buberwa d mko pamoja nini? Maana naona mmeuliza swali moja! Ni mtendaji au mnawaita nani lakini ni hawa waliopotishwa na Jafo SM. Kwani kusikia watu wanachoongea kutokana na ukaribu ndio kuhudhuria?
 
Mambo mawili makubwa yamejitokeza hivi karibuni kwanza CCM imeshinda uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kishindo, pili Tume ya taifa ya uchaguzi imevuka lengo kwa kuandikisha wapiga kura wengi kuliko ilivyotarajiwa.

Hii maana yake ni kuwa uchaguzi mkuu wa 2020 utakuwa na wapiga kura zaidi ya milioni 29 hii ni historia.

Kwa kuliona hilo CCM inatarajia kutoa semina elekezi kwa viongozi wake wa serikali za mitaa ikiwa ni matayarisho ya kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu.

Ikumbukwe kuwa wananchi wengi wamejiandikisha kupiga kura baada ya kuridhishwa na maendeleo yanayoletwa na serikali ya awamu ya 5 na kwa mara ya kwanza tangu tupate Uhuru watanzania wameanza kuona thamani ya kura zao.

Hongereni CCM.

Maendeleo hayana vyama!
Binafsi sikuwahi kujiandikisha ila msimu huu nimetimiza hilo.
Japo si dhani kama unachosema ni sahihi.
Lengo langu ni kuwachagua viongozi watakao kuwa tayari kupigania maslahi yangu ninayoyapa kipaumbele bila kujali chama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mambo mawili makubwa yamejitokeza hivi karibuni kwanza CCM imeshinda uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kishindo, pili Tume ya taifa ya uchaguzi imevuka lengo kwa kuandikisha wapiga kura wengi kuliko ilivyotarajiwa.

Hii maana yake ni kuwa uchaguzi mkuu wa 2020 utakuwa na wapiga kura zaidi ya milioni 29 hii ni historia.

Kwa kuliona hilo CCM inatarajia kutoa semina elekezi kwa viongozi wake wa serikali za mitaa ikiwa ni matayarisho ya kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu.

Ikumbukwe kuwa wananchi wengi wamejiandikisha kupiga kura baada ya kuridhishwa na maendeleo yanayoletwa na serikali ya awamu ya 5 na kwa mara ya kwanza tangu tupate Uhuru watanzania wameanza kuona thamani ya kura zao.

Hongereni CCM.

Maendeleo hayana vyama!
Usijidanganye, Wengi wao walienda kujiandikisha Ili wapate vitambulisho tu na si kwa ajili ya kupiga kura

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom