Baada ya uamuzi wa Mahakama ya Kenya,Zitto asema Katiba Mpya ni lazima lazima lazima

Baada ya uamuzi wa Mahakama ya Kenya,Zitto asema Katiba Mpya ni lazima lazima lazima

Tatizo la watanzania ni kuamini kwamba katiba mpya unapewa na mtesi wako. CCM hayuko tayari kukupa katiba mpya. Unapigania katiba mpya.

Uhuru tulipewa maana nchi ikikuwa under the mandate of Great Britain. Sasa tunadhani hata katiba tutapewa bure.
 
Katiba mpya haitakua na maana Tanzania endapo wagombea urais wa Tanzania ni walewale akina Lowasa na wapiga deal wenzie..!
 
Hakuna kipya ...kwani hatujui hilo? Tunawataka waje na mikakati si porojo za umuhimu wa katiba mpya ambazo tunazijua .....

..hivi kwanini SERIKALI isipeleke Bungeni muswada wa kufanyia marekebisho sheria mbalimbali?

..Kwa hali ilivyo sasa hivi suala hili likianzia upinzani litakwama kwasababu ya wingi wa wabunge wa ccm ktk bunge la jamhuri.

..Kwa uchache, na kwa kuanzia SERIKALI inaweza kupeleka mswada utakaoleta mambo yafuatayo.

1. Tume Huru ya Uchaguzi.

2. Vyama kuruhusiwa kuungana bila kulazimika kujifuta na kuanza sifuri.

3.Matokeo ya udiwani, ubunge, uraisi, kuhojiwa mahakamani.

4.Kuna na Mahakama huru. Jaji Mkuu na Jaji Kiongozi wathibitishwe na bunge.


..Nadhani Prof.Kabudi ni mhubiri wa hayo niliyoyaorodhesha hapo juu. Sielewi kwanini hapeleki mswada wenye mabadiliko hayo bungeni.
 
Katiba sio kipaumbele cha serikali ya awamu hii, tuiache serikali ijenge viwanda kwanza.

mafisadi hayana rangi
 

Nyinyi viongozi wa vyama ndio wa kusindikiza hayo mambo mkiwa ndani ya bunge na nje ya bunge muhamasishe wananchi kufanya migomo na maandamano ili watawala wajuwe kwamba wananchi wamechoka kutawaliwa wanataka kuongozwa kisheria na kufuata katiba co kila ck tundu lissu .
 
Back
Top Bottom