Baada ya Uchaguzi Dkt. Bashiru ataendelea na nafasi ya Katibu Mkuu?

Baada ya Uchaguzi Dkt. Bashiru ataendelea na nafasi ya Katibu Mkuu?

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
20,654
Reaction score
35,887
Heshima sana wanajamvi,

Katibu Mkuu wa chama chochote ukiondoa vile vyama vya msimo wa uchaguzi ndiye mtendaji mkuu wa shughuli na utendaji wa chama za kila siku.Chama tawala CCM kimewabadili makatibu wakuu kwasababu mbali mbali lakini nyingi kati ya hizo sababu ni kushindwa kwenda na wakati au kushindwa kutimiza majukumu ya chama.

Tumewashuhudia makatibu wakuu wengi wakiondoka na wengine wakiingia katika nafasi hiyo nyeti ya kiutendaji.Tuliona kina Hayati Kawawa,Kolimba,Makamba na mwisho Mh Kinana wakiondolewa wengine kwa fedhea na wengine wakistaafu kwa heshima kubwa.

Dr Bashiru ni msomi mkubwa,kabla hajaibuliwa chamani alikuwa Mhadhiri UDSM tena mbobezi mkubwa katika fani ya siasa.Nilitegemea kuona mabadiliko makubwa ndani ya chama kupitia Mbobezi huyu wa siasa lakini katika hali ya mshangao mkubwa chini ya utendaji wake tulishuhudia CCM ikitegemea zaidi nguvu ya vyombo vya dola kuliko WANANCHI au WANACHAMA.Chini ya uongozi wake zilizaliwa siasa za kuunga mkono juhudi

Sasa tunaweza kusema pasipo shaka kwamba wasomi wetu wabobezi hawana kitu cha ziada ukiwalinganisha na Wazee wetu kama Mzee Kawawa.Wasomi wetu wa leo wanafanya mambo ya hovyo hovyo kuliko yaliyofanywa na wazee wetu wengi waliomaliza darasa la nane au kumi kipindi cha ukoloni.Elimu yetu ya leo imejaa wingi wa vyeti na mbwe mbwe nyingi pasipo maarifa.Kati ya mabo ya hovyo kuwahi kufanywa na CCM ni suala la kununua wapinzani halafu kuandaa chaguzi za kiini macho ambazo wananchi walinyimwa fursa ya kuchagua.

Ni matarajio ya wengi baada ya uchaguzi huu Dr Bashiru ataondolewa mara moja kwasababu ya kushindwa kumshauri vizuri Mwenyekiti wake.Hata baada ya kukaa katika nafasi ya Katibu Mkuu kwa muda wa kutosha bado anaonekana hakijui chama.

Wasalam Ngongo safarini Katavi Mpanda Mjini kwasasa.
 
Dk Bashiru 2018 alisema " CCM haitotumia tena wasanii kwenye kampeni na mikutano yake".
. 2020 Tumeona CCM ikifanya Fiesta kaenye majukwaa ya kisiasa.

Dr Bashiru alisema CHAMA CHA MAPINDUZI kinategemea Dola kushinda Uchaguzi.

Ukiingia CCM lazima wakutoe Ubongo kwanza.
Tumeona watu kama .

Kabugi.
Kitila.
Haraka haraka nk.

Ccm imepoteza uhalali wa kushika Dola
 
Mwajidanganya Bashiru ni mwiba wenye sumu kali Mungu Tufikishe2810 salama
 
Hawezi kuwa Katibu mkuu tena. Anaondoka na magufuli wake. Jitu la hovyo kabisa hilo.
 
Back
Top Bottom