Baada ya Vitambulisho kinachofuata ni 'Health Records'

Hata sasa zipo taarifa za kitabibu zinazotunzwa na taasisi uliyokwenda kwa matibabu. Ikitokea unapelekwa taasisi nyingine kwa uchunguzi au matibabu zaidi, wataalamu wa hizo taasisi mbili huwasiliana na kutumiana taarifa za mgonjwa. Japo bado ni kwa mafaili/ karatasi /(barua pepe kwa nadra) zaidi ya wenzetu ambapo ni kielekronika (digitali).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wao zuri nankwamkuongezea Tu, Watanzania wote wapimwe maradhi ya nafsi, wazimu, wehu,. uchizi na records zao ziweze kuwa accessible nan yeyote maana nahisi kama idadi kubwa ya Watanzania ni wehu wehu.
Leo tumekukamata kwa kuchapia!
ulisomea ujinga weye
 
😂😂😂
 
Kingsmann,
Sasa mkuu tutasubiri mpaka lini hicho kizazi kipite?
Si bora tuanze kuingiza hiki kipya kidogo kidogo ili kuimarisha huduma.
 
Vitambulisho bado hawajamaliza mkuu maana taarifa nyingi za watu kama majina ya wazazi na tarehe za kuzaliwa zimekosewa sana kwahiyo ilitakiwa usajili uanze upya
 
Mr Q, Tanzania tunachukulia kirahisi sana hizi habari. Kwa sababu ya ulimbukeni.

Kutaka habari za afya ziwekwe pamoja kabla hata ya kuwa na sheria ya kuongoza hilo ni hatari sana.

Na hata sheria zikiwepo, sheria ambazo haziwezi kuwa enforced ni kama sheria ambazo hazipo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mnhhh....

Tatizo lako hamna sheria kabla ...

Kwani si tunatoa tu mawazo..

Wenyewe ndio watafanya feasibility study???

Nilitegemea utasupport..LOL...

Hii sio tu kwa wagonjwa ...

Bali its easy ku monitor vitu vingine pia ambavyo vinaweza kusaidia Afya kama Researchers, Policy makers..etc..

Data ndio zinatoa picture..vingine vinafuata
 

asante kwa kupaza sauti binti malkia...tumechoka hasaa..kila ukienda hospitali ni kuanza keulezea historia ya maisha yako...very boring and disappointing!!!
 
Sawa.

Sijapinga. Naonesha changamoto ilivyo kubwa kuliko maongezi haya yanavyoonesha.

Haya mambo nayajua, nimeyasomea, naelewa challenges za data security.

Nimesoma sheria ya Marekani inayoongoza haya mambo. Inaitwa HIPAA.

Nimeona challenges walizo deal nazo na kuzikabili.

The Health Insurance Portability and Accountability Act of 1996 (HIPAA).


Sent using Jamii Forums mobile app
 
bora hata umeliona hili.
Mtoa mada inabidi ajiulize kwanini raisi wa korea aliamua kutembea na choo chake ili end product isiangukie mikononi mwa majasusi?
Inabidi ajiulize kwanini yule raisi ambaye alitegeshwa choo cha bandia ilimradi tu haja yake ipelekwe maabara kwa uchunguzi?
Hapo juu amekana kwamba hana HIV sasa wadukuzi wakitumia taarifa zako kukuharibia mipanngo itakuwaje?

Anachoeleza kinaweza kuwa cha muhimu ila kuna mambo mengine laizima yazingatiwe kabla..
 
Haya mambo niliposikia mkongo wa taifa nilidhani sasa tunaanza kuwa na data base, kumbe ile ilikuwa kwa ajili ya mitandao ya simu tu.
Nchi hii inamatatizo mengi sana ila tatizo kubwa zaidi ni ujinga, na elimu siyo suluhisho. Maana kuna watoa maamuzi wamesoma vizuri huko nje kwenye elimu bora lakini bado ni wajinga.
HIS ipo serikalini Lakini haitiliwi mkazo kabisa. Wanufaika wa mfumo wanadai maslahi hawajali haya mambo, vitendea kazi wanavyofahamu wao ni modern diagnostic tools lakini siyo HIS.
HIS ilifadhiliwa na PEPFAR miaka mingi lakini hakuna outcome yoyote.
Nchi hii iko hivi, mradi unaanzishwa na unafadhiliwa, waanzilishi na wafadhili wakiukabidhi serikalini unakufa siku hiyo hiyo baada ya makabidhiano.
Kumbuka Malaria control program ya wajapani, ukoma na kifua kikuu ya wajerumani, ukimwi ya wamarekani, malaria ya bilimelinda gets na mingine mingi.
Hakuna mradi unaendelea ukitoka mkononi mwa wafadhili.
 
Mleta mada hajui kuwa mifumo hii ipo siku nyiingi lakini tatizo letu ni application, tuliishazoea kukaa makoridoni kutafuta rushwa mifumo hii siyo rafiki huku kwa wataalamu wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…