Lavit
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 14,834
- 32,522
Wakuu leo nimekumbuka takribani miaka 20 iliyopita nilikuwa kidato cha nne shule ya serikali huko Mbeya.
Sasa pale shule toka tunafika form 1 kulikuwa na malalamiko makubwa sana kuhusu chakula kibovu, malalamiko yalikuwa mengi sana ila yalipuuzwa hasa na second master aliyekuwa amekaa pale kwa zaidi ya miaka 20.
Sasa 2005 miezi kama hii vuguvugu likawa kubwa sana kwa wanafunzi kuchoshwa kula dona (sisi tulikuwa tunaita shudu), na yalikuwa mashudu kweli maana yale mahindi yalikuwa yanasagwa yakiwa machafu na muda mwingine yakiwa yameoza kabisa.
Nakumbuka tetesi za mgomo zilianza kama utani zikihusisha viongozi wote wa mabweni, second master alivyopata taarifa aliitisha kikao ambacho aliishia kututisha kwamba hata kama watabadilisha chakula sio kwa ajiri ya kale kamgomo ketu.
Muda ulienda na ikawa bahati walimu walikuwa na sherehe yao, wakiwa wamepika pilau na bia za kutosha huku sisi wakiwa wametuachia "shudu"
Sasa kilichotokea, ile sherehe haikufanyika maana staff ilivamiwa na vioo vilivunjwa, baadaye ofisi ya nidhamu na madarasa mawili yalichomwa moto. Nakumbuka FFU walikuja usiku ule ule, huku wakikuta watu wengi hatupo pale shuleni!
Kulipokucha wengi tulirudi, cha ajabu na kushangaza siku ile tulikula ugali wa sembe na kwa mara ya kwanza tukagaiwa matunda.
Matokeo yake wengi walifukuzwa shule, na tuliobaki tulipigwa fine. Ila toka hapo mambo yalibadilika, yule second master kiburi aliomba uhamisho maana alidai hawezi tena kubaki ile shule labda kuwe hamna shule nyingine hii nchi.
Nb; nilichojifunza ni kwamba ni ngumu sana kuleta mabadiliko kwa kuongea tu, maongezi yetu ya miaka nenda rudi yalikuja kuhitimishwa na vurugu ya siku moja. Wale walimu wasingeweza kufanya mabadiliko hivi hivi wakati walikuwa wanufaika wa kutulisha chakula kibovu.