Baada ya Watanzania kukamatwa na dawa za kulevya, hiki ndio kimemkuta Madee akiingia Afrika Kusini

palalisote

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2010
Posts
8,335
Reaction score
1,459

Kwenye Exclusive interview na millardayo.com Madee amehadithia kila kitu kilichomtokea wakati anaingia tu Afrika Kusini siku kadhaa zilizopita ambapo hii imetokea kutokana na ukubwa wa habari, uzito wa tukio la wale Watanzania wawili wasichana waliokamatwa kwenye kiwanja cha ndege Johannesburg wakiwa na dawa za kulevya wakitokea Tanzania.
Madee anakwambia alipotua kwenye kiwanja cha ndege, kawaida huwa kuna utaratibu wa kuchekiwa hati ya kusafiria na ukaguzi mwingine ambao hufanywa na mitambo maalum kwa kila abiria anaeingia Afrika kusini, ni ukaguzi ambao unafanywa Airport kabla ya abiria kuruhusiwa kuingia kwenye nchi yenyewe.

Kilichomfanya Madee kusachiwa na kuhojiwa karibu dakika 60 ni pale tu aliposema anatokea Tanzania, kuna wazungu wawili wenye sare tofauti za kipolisi wakaanza kumsachi mpaka kufikia kumwambia avue t shirt yake, alivua t shirt na kubakiwa na nguo nyepesi ya ndani wakati huo abiria wenzake aliokwenda nao walikua wameruhusiwa.
Kati ya abiria wote waliokuja pamoja kwenye ndege, Madee na Mzimbabwe mmoja ndio walikaguliwa sana ila huyo mwingine alikaguliwa kidogo tu kama dakika 10 na wala hakuambiwa avue nguo.

Sehemu yenyewe Madee aliyoambiwa avue nguo sio kwenye chumba maalum, ni palepale kwenye foleni wanaposimama watu ila kwa pembeni kidogo, ni sehemu ambayo imezibwa na kioo kinacholingana na usawa wa tumbo kushuka chini…. Madee anakwambia jamaa walinong'onezana sana wakati wanamkagua.
Hata hivyo baada ya Askari hao kumuweka sana msanii huyu wa bongofleva kutoka kundi la TipTop Connection walimuomba radhi baada ya kumaliza ukaguzi wao ambao pia ulihusika kulivuruga sana begi lake.
216.png

Wasanii wengi wa bongo ni briefcase.wanatumiwa xana na vigogo wa CHAMA CHA MAUAJI (...) kufanikisha dili zao za usafirishaji sembe!
 
huyu jamaa tokea alipoenda studio na kuharisha kwa mdomo eti"hiphop ni uhuni"sitaki kusikia habari zake,wakina ruge walimuingiza kingi kurekodi ----- huo kwa ujira mdogo,..halafu kuna track nyingine anajifanya kuimba american english eti ladies and genlomen..aaaaaghhh
 
Ndiyo maana tunapaswa sote tushiriki vita hii. Ni aibu kwamba sasa Watanzania tunaogopwa na kuchukiwa kwa sababu tu ya wapuuzi wachache wanaotaka kutajirika haraka haraka.
 
huyu jamaa tokea alipoenda studio na kuharisha kwa mdomo eti"hiphop ni uhuni"sitaki kusikia habari zake,wakina ruge walimuingiza kingi kurekodi ----- huo kwa ujira mdogo,..halafu kuna track nyingine anajifanya kuimba american english eti ladies and genlomen..aaaaaghhh

Duuuuuuhhhh.....

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Huyo Madee ni jingafulani tu yaani anadhani hapa wote ni wajinga wenzake? Watanzania wanaingia kila siku South Africa kwa shughuli zao halali na hawapati usumbufu, yeye kama alisachiwa sana maana yake walimspect na ni haki yao.

We mtu umevaa kama unakwenda sokoni unategemea nini? Mimi ninavyoufahamu uwanja wa Oliver Tambo Johannesburg ni uwanja ambao uko busy sana na una terminal nyingi kwahiyo ukivaa kama chizi kupata usumbufu kama huo ni haki yake, kikubwa hapa ninachokiona yeye alitaka tu kujipa promo ili mabwege wenzake wajuwe jamaa yupo kwa Jayzee.
 
hizo statement zenu kwenye social network lakini ukweli wa mambo hauko hivo!
Ukweli unaotaka KUULAZIMSHA wewe uwe ni upi?

Ukweli ni kwamba biashara ya madawa ya kulevya ni kinyume cha sheria za nchi hii
Ukweli ni kwamba vijana wa kitanzania wanaangamia kwa kufanywa kuwa mateja wa madawa ya kulevya
Ukweli ni kwamba kila mtanzania leo akisafiri huko nje anakaguliwa kuliko kawaida eti kwasababu anahisiwa amebeba drugs, hii ni AIBU!!!
Ukweli ni kwamba Wafanyabishara wa drugs wanalindwa na kupitishwa VIP wakisafiri pale JNIA. Only in Tanzania. AIBU!!
Ukweli ni kwamba ukikamatwa na Drugs huko nje Utapigwa Mvua za kutosha tu!!
 
but not all of them ni wasafirisha unga kaka!
 
Nimemsikiliza sasa hivi huyu boya Madee kwenye kipindi cha Mirad Ayo kuna kitu nimesense tayari, eti anadai alitumwa na bosi wake anaitwa Bonge kwenda kupress order ya Jezi wana mpango wa kufunguwa duka la vifaa vya michezo.

My take: huyu kijana kuna kitu anaficha, hakuna connection ya biashara ya nguo kati ya Tanzania na South Africa bali conection ni Asia kwa sababu ya bei ili kupata faida.

Naona hawa vijana hawajakoma bado wacha waendelee na ujanja wao siku zao zinahesabika, anavyosimulia anadhani anapiga stiry na wasela wenzake wa manzese, kumbe hajui watu tuina mashine mpaka za kupima uongo.
 
Huyo Madee ni jingafulani tu yaani anadhani hapa wote ni wajinga wenzake? Watanzania wanaingia kila siku South Africa kwa shughuli zao halali na hawapati usumbufu, yeye kama alisachiwa sana maana yake walimspect na ni haki yao.

We mtu umevaa kama unakwenda sokoni unategemea nini? Mimi ninavyoufahamu uwanja wa Oliver Tambo Johannesburg ni uwanja ambao uko busy sana na una terminal nyingi kwahiyo ukivaa kama chizi kupata usumbufu kama huo ni haki yake, kikubwa hapa ninachokiona yeye alitaka tu kujipa promo ili mabwege wenzake wajuwe jamaa yupo kwa Jayzee.
umeonaaaeeeeee
 
Ukweli unaotaka KUULAZIMSHA wewe uwe ni upi?

Ukweli ni kwamba biashara ya madawa ya kulevya ni kinyume cha sheria za nchi hii
Ukweli ni kwamba vijana wa kitanzania wanaangamia kwa kufanywa kuwa mateja wa madawa ya kulevya
Ukweli ni kwamba kila mtanzania leo akisafiri huko nje anakaguliwa kuliko kawaida eti kwasababu anahisiwa amebeba drugs, hii ni AIBU!!!
Ukweli ni kwamba Wafanyabishara wa drugs wanalindwa na kupitishwa VIP wakisafiri pale JNIA. Only in Tanzania. AIBU!!
Ukweli ni kwamba ukikamatwa na Drugs huko nje Utapigwa Mvua za kutosha tu!!
Alichomaanisha Yusuph nami pia namuunga mkono ni kwamba kwenye social network mnawaponda lakini nje ya hapo mnawashabikia kupita maelezo!
 
Back
Top Bottom