Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
February 7,2008, aliekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Edward Lowassa, alilazimika kujiuzulu kutokana na kashifa ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond ambayo ilibainika kuwa ilikuwa ni kampuni hewa(kwa mujibu wa kamati ya Mwakyembe wakati huo).
Wakati hayo yakitokea mwaka 2008, leo tumepata Makama wa Rais mpya(mteule) Mhe. Philip Mpango ambae kabla ya uteuzi huo, alikuwa Waziri wa Fedha na Mipango, wizara inayosimamia taasisi kadha ikiwemo Benki Kuu.
Juzi tarehe 28,wakati akipokea taarifa ya CAG, Rais wa Jamuhuri ya Muungano, Mama Samia Suluhu Hassan, ametoa maagizo kwa CAG kuchunguza fedha za miradi ya maendeleo zilizotolewa Benki Kuu kuanzia mwezi January mwaka huu mpaka mwezi March mwaka huu.
Hivyo, iwapo taarifa ya ukaguzi ya CAG itaibua utata, utata unaoweza kugusa mpaka wizara ya fedha kama msimamizi wa Benki Kuu huku Mpango akiwa ndie alikuwa Waziri, basi yale yaliyotokea mwaka 2008 yanaweza kujirudia hata kama yeye atakuwa hahusiki moja kwa moja.
Ukiacha hili la ukaguzi wa CAG, yako mengine tunayoyasoma humu mitandaoni yanayogusa watendaji wengine waliokuwa chini ya Waziri Mpango, watendaji aliopaswa kuwasimamia.
Kwakuwa wahusika hawakanushi wala kutolea ufafanuzi yanayosemwa, na kwakuwa Waswahili wanatuambia: "lisemwalo lipo na kama halipo laja," basi tuache muda utasema.
Tusubiri.