Baada ya Wema Sepetu kumiliki Range Rover, Wolper atangaza kubadilisha range yake

Baada ya Wema Sepetu kumiliki Range Rover, Wolper atangaza kubadilisha range yake

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Vita vikali vinaendelea kati ya wadada wanaofanya vizuri kwenye tasnia ya filamu, Wema sepetu pamoja na Jackline Wolper, ambapo hivi karibuni mrembo wolper alipost kwenye ukurasa wake wa instagram gari lake jipya la kifahari aina ya range rover evoque , baada ya siku kadhaa wema sepetu alitangaza kujizawadia gari aina ya range Rover evoque katika sherehe yake ya kuzaliwa kama aliyo post jackline wolper na kuwaacha watu katika hali ya sintofahamu kuhusu warembo hao wenye mvuto zaidi bongo movie.

Hata hivyo, baadae ilijulikana gari analolimiki msanii huyo, ni matunda ya kampeni aliyokuwa akifanya kwenye chama tawala cha ccm, ambapo yeye pamoja na msanii mwenzie Steve Nyerere walizawadiwa magari hayo ya kifahari.

Kitendo cha msanii Wema Sepetu kutangaza kujizawadia gari la aina ya range rover kinatafsiriwa kuwa mwiba kwa staa mwenzio Jackline Wolper ambaye ndiye aliyetangaza kumiliki gari hilo kabla, hata hivyo msanii huyo ametangaza kubadilisha gari hilo haraka iwezekanavyo kwani magari hayo yameonekana kuwa kama njugu mtaani, kauli iliyotafsiriwa na wapenda ubuyu kuwa Wolper hakupenda staa mwenzio kumiliki gari hilo kwani alishajihesabia yeye ndio staa pekee wa maigizo anayesukuma gari la kifahari kuwazidi warembo wenzio, kitu ambacho kimekuwa ndoto za ali nacha baada ya msanii mwenzie kuibuka na gari hilo hilo.

Wema na Wolper wanahesabiwa kuwa kati ya mastaa wachache wa kike nchini wanaosukuma mkoko wa bei mbaya, ambapo awali Lady Jaydee ndiye aliyeanza kumiliki mkoko huo kabla ya mastaa wenzie
 
Story za kishgashga peleka huko. Eti New alert!!!!
 
Inasemekana kaweka oda ya hii hapa:
0000605b5148-e9ca-4163-9.jpg
 
huo n upumbav tu wangeshindania kufungua fremu na kujenga nyumba au kufungua makampun...gar za bei chafu na nyumba hawana sio upumbav.. ni nini?
 
Ukishtuka kusikia hao bongo movie wanamiliki vitu...basi ww mshambaa
 
Kuna sehemu nlikuona ulinichekesha sana mchana eti yericko akirudi atasema alipelekwa guantanamo lol
Teh Teh huyo Gwiji wa mitandao ni hatari sana ana vituko ..huwa tunacheka sana na akirudi lazima aje na story ya uongo..
 
Back
Top Bottom