Tetesi: Baada ya wizi wa kura na mwenyekiti wa CCM wilaya kutoka wajumbe, Uchaguzi wa CCM jimbo la Hai kurudiwa

Tetesi: Baada ya wizi wa kura na mwenyekiti wa CCM wilaya kutoka wajumbe, Uchaguzi wa CCM jimbo la Hai kurudiwa

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Kuna kila dalili uchaguzi wa ccm uliofanyika tarehe 1.10.2022 kurudiwa tena.

Hii inatokana na kundi kubwa la wajumbe ambao ni wapiga kura kukutana leo na kuamua maamuzi ya kutokuwa na Imani na uchaguzi huo ambao uligubikwa na wizi was Kura, kuongeza Idadi ya wajumbe hewa Ili kuongeza Idadi ya wapiga kura, sambamba na hilo uchaguzi uligubikwa na rushwa .

Taarifa Za ndani zinainyesha Chama cha chadema kumefurahia mpasuko huo wa ccm kuelekeawaka 2025.

Iwapo uchaguzi huo hautarudiwa mbunge wa Jimbo hilo kuna Kila dalili mwaka 2025 kwenda kulima hoho badala ya kwenda bungeni Dodoma.

Kwa mantiki hiyo mbunge amepanga safe ya kuiondoa ccm madarakani kama uchaguzi huo hautarudiwa .

Sambamba na Hali kutokuwa shwari ndani ya ccm Jimbo la Hai, mwenyekiti wa ccm wa wilaya aliyechaguliwa kwa Kura Za Wizi ameamua kufanya yake baada ya kuitisha kikao kisicho esami cha wenyeviti kutoka kata 17 wa ccm na kuamua kuwatukana na kuanza kupigana mbele ya kikao hicho.

Hadi tunakwenda mitambo Tayari kata 17 zimezira kufanya kazi na mwenyekiti wa ccm jimbo la Hai na upande wa upinzani wamefanya sherehe kufurahia mpasuko huo.

Kelele Za uchaguzi huo zimetolewa kila kona ya wilaya hiyo ila Katibu wa ccm wa wilaya ameweka Pamba masikioni na hadi sasa Jimbo hilo Halina kamati ya siasa ya wilaya jambo ambalo Katibu mkuu wa ccm ameonyesha Pia kulishangaa baada ya kufanya uchaguzi huo.

Katibu mkuu wa CCM Taifa,fika Hai kuonaona na Halmashauri kuu ya ccm ya wilaya kuna jambo.

Jioni njema
 
Aliyezoea vya kunyonga., vya kuchinja haviwezi (Tundu Antipas Lissu, BMK 2014)
 
Mbona si jadi yetu kuiba kura. Wanadharirisha picha nzuri ya chama, washughulikiwe hao waliofanya jambo hilo la kizandiki.
 
Ccm ina wenyewe mbona unan'gang'ania na kulalamika hama uanzishe chako.
 
Back
Top Bottom