Baada ya zaidi ya Miaka 50 nakutana na Rafiki yangu wa Udogoni Salum ''Gordon West'' Khalili

Baada ya zaidi ya Miaka 50 nakutana na Rafiki yangu wa Udogoni Salum ''Gordon West'' Khalili

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
23,526
Reaction score
34,057
1777642693815.png

BAADA YA ZAIDI YA MIAKA 50 NIMEKUTANA NA RAFIKI YANGU WA UDOGONI SALUM "GORDON WEST" KHALIL

Nimesimama nje ya Masjid Maamur tumetoka kwenye Akid ni baada ya swala ya Isha na kuna msongamano.

Nimesogea pembeni vurugu ya magari, Bajaj na Bodaboda ipungue.

Mtu mmoja katika kundi ananionyesha mtu kasimama karibu yangu ananiambia, "Umemuona goalkeeper wa Young Kenya?

Nikamtazama na yeye akanitazama.
Mimi sikumtambua nikajibu, "Goalkeeper wa Young Kenya alikuwa Ali Gordon Banks."

"Ali ndugu yangu mimi pia nilicheza golini Young Kenya."

"Wewe nani?
Nikamuuliza.

Jibu likaja, "Salum Khalil."
Hapo hapo nilimkumbatia.

Salum Khalil (Gordon West).
Salum Khalil alikujakuwa goalkeeper wetu Everton na kisha Saigon.

"Salum unakumbuka siku unakwenda Tabora mimi nilikuja stesheni kukuaga?
Salum Khalil alijibu anakumbuka sana.

Ilikuwa mwaka wa 1967 Salum alipelekwa Tabora na wazee wake nadhani ilikuwa shule.
Toka siku ile ndiyo leo tunakutana.

Nilimkumbusha Salum Khalil mechi yetu ya kwanza Everton na Saigon Mnazi Mmoja pembeni ya Kibarua Bar.

Anaikumbuka sana alinambia.
Nilivunjia jino la chini kipande.

Jumanne "Guu la Ngamia" Masimenti alipiga shuti kali "close range" golini kwetu Everton nami nimesimama katikati ya goli nikaweka kichwa changu.

Taya mbili juu na chini zilijikusanya pamoja jino likakatika.

"Gordon Banks yupo?
"Amefariki Yemen."

Nilikuja kusikia kuwa Salum na yeye aliondoka na kwenda Arabuni.

Mwaka jana nilipata kumuuliza Mussa Shagow kiongozi wa Saigon Club kuhusu Salim Khalil na akanifahamisha kuwa yuko Dar es Salaam lakini hakuwa na simu yake.

Milima haikutani lakini binadamu hukutana.

1777643529219.png

Gordon West
 
Assalamualaikum mzee Mohamed Said . Mlishawahi kukipiga na TPC? Hebu tupe story za hii timu iliyokuwa chini ya meneja wake Mshiriki marehemu mzee jimmy
 
Assalamualaikum mzee Mohamed Said . Mlishawahi kukipiga na TPC? Hebu tupe story za hii timu iliyokuwa chini ya meneja wake Mshiriki marehemu mzee jimmy
Logo,
Timu yetu ilikuwa ni ya mtaani tuko shule ya msingi na wengine madarasa ya kwanza sekondari.

Baadhi yetu wakaja baadae kuwa wachezaji wa club kubwa na kufikia kuvaa jezi ya taifa.
 
Back
Top Bottom