Baada ya zama za kubebwa na Yamoto Band kupita, Enock Bella atoa wimbo mbaya kupitiliza

wimbo safi, video safi.. mtoa mada huna lolote zaidi ya chuki binafsi za ki,ke.. wewe ni nani mpaka ufanye conclusion ya wimbo na kushawishi tusiitazame
Yaah.. Huo wimbo nimeuskiliza, ni moja kati ya nyimbo chache mbaya kuwahi kushuhudiwa katika ulimwengu wa Industry ya Music

Namshauri jamaa akawe Bodyguard wa Dogo Janja
 
Lile besi lake lisingeweza kupendeza kwenye Verse ndefu,
Abadili tu sauti aimbe kawaida
 
Kusema ukweli ni jambo zuri na huo ni ukweli wako kwake kwamba hujakubali ok ni sawa. Basi wengine wataukubali/watamkubali jamaa na kama kuna sehemu kakosea washauri afanye marekebisho next time. Bidii hushinda yote
 
Mtoa post makalio ya shangazi yako! Na liroho lako baya tena la kichawi heshimu juhudi na bidii ya enock nyama weeeee ....ulitaka amuimbe wewe ? Nadiriki kusema wimbo mzuri sana wahusika Ujumbe wake tunauelewa .....wewe na gubu lako tupakule
 
Mtoa post makalio ya shangazi yako! Na liroho lako baya tena la kichawi heshimu juhudi na bidii ya enock nyama weeeee ....ulitaka amuimbe wewe ? Nadiriki kusema wimbo mzuri sana wahusika Ujumbe wake tunauelewa .....wewe na gubu lako tupakule
Tatizo hujui mziki ,sikushangai
 
Naujua tena sana hadi kidedea pumb**** acha bwana mdogo Bella apambane ....wewe kinacho kuuma nini ....ulitaka aimbe nini?

Harafu hizi post zako peleka Facebook kule hapa siyo mahali pake JF
 
Sipendi kuchuma dhambi kwa Mwenyezi Mungu wala kuwa ' Mnafiki ' ukweli ni kwamba Wimbo ni mzuri tena sana tu na unachezeka isipokuwa nadhani alimpata Director mbaya wa Video kwani kuna baadhi ya ' scene ' hazikupangiwa vyema na Wahusika waliokuwepo hasa huyo Video Queen aliyemtumua alikuwa hachangamki na ni kama vile anajishtukia.

Kuhusu sauti tena nadhani sauti yake ameitumia vile inavyotakiwa na imekaa mule mule. Huyu Kijana kama akiendelea kujipanga vizuri na kurekebisha tu baadhi ya changamoto ndogo ndogo na akatulia namuona ni mzuri kuliko hata Dogo Aslay isipokuwa tu anazidiwa nae ' Kinyota ' tu.

Mwisho nitoe tu ushauri nadhani tujifunze ustaarabu wa kuwatia moyo hawa Wasanii wetu kuliko kuwaponda kwani nakumbuka kwamba hata wakati Diamond anaanza kuimba na kutoa ile Single yake ya Kwanza alipondwa mno ila hakukata tamaa akapambana na hatimaye leo anafanya vizuri huku akiwa na Pesa pamoja na Utajiri ambao kuna uwezekano mkubwa Mimi na Mleta mada hata tukisema tuchanganye Pesa zetu na tuuze mali zetu bado hatuwezi hata kufikia tu robo tatu ya Pesa alizonazo Diamond Platinum.

Kwa taarifa yenu ni kwamba huyu Msanii wa Kikongo Christian Bella ambaye huku Tanzania anaonekana ni ' Mfalme ' wa muziki na masauti wakati alipokuwa akiimba katika Bendi ya Koffi Olomide ya Quarter Latin pamoja na Kaka yake mkubwa alionekana hafai na hadi kudhihakiwa na Wakongo mpaka akaamua kuondoka huko na kuja Tanzania ambapo alikutana na Wenzake akina Tarsis Masela wakaanzisha Bendi yao ya AKUDO Impact ambapo kupitia hiyo Bendi ndipo ' nyota ' yake ikaanza kuwaka vyema na hadi leo ni Msanii mkubwa tu hapa nchini Tanzania.

Achilia mbali huyu Christian Bella huko nchini Congo DR mara baada ya huyu Mwanamuziki Kipenzi kwa sasa Fally Ipupa ' Dicaprio ' kuhama / kutoka kwa katika Bendi ya Koffi Olomide na kutoa ile album yake ya Kwanza ya ' Bakandja ' alichekwa na kudhihakiwa mno kwamba hajui na asingeweza kushindana na Mpinzani wake mkubwa Msanii Ferre Gola na alipokuja kutoa sasa album yake ya pili iitwayo Droit Chemen ndipo Wakongo na hasa wale ' Critics ' na ' Haters ' wake walipompigia ' Salute ' na leo amekuwa ndiyo Msanii Tajiri wa Kizazi cha Tatu cha nchini Kongo achilia kile cha pili cha akina Koffi Olomide, JB Mpiana ,Ngiama Makanda Werrason, Kanda Bongoman na Aurlus Mabele huku Kizazi cha Kwanza kikiwa ni kile kile cha akina Marehemu Luanzo Makiadi Franco, Yoka Longo, Madilu System, Tabu Ley ' Roucherou ' na Pepe Kalle.

Namtabiria makubwa sana ' Kimuziki ' huyu Kijana Enock Bella na namwomba Mwenyezi Mungu ampe ambariki, awe mvumilivu, asikate tamaa kwani naona taa ya Kijani na ya Kimafanikio Kwake inakuja na kuna siku huyu huyu aliyemponda vibaya leo atakuja kumpigia ' salute ' tena kubwa sana.

Yangu ni hayo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…