Baada ya zama za kubebwa na Yamoto Band kupita, Enock Bella atoa wimbo mbaya kupitiliza

Baada ya zama za kubebwa na Yamoto Band kupita, Enock Bella atoa wimbo mbaya kupitiliza

WE KUNA KITU CHA WCB ulishawahi kusifia?
TUMESHAKUZOEA HANCE!
acha watu wasikilize watoe maoni yao!
SASA HATA KUSIKILIZA UNAWAZUIA?
WE NANI BANA?
kwa hiyo KEYBOARD YAKO AU?
 
Ama kweli majumba makubwa hustiri mambo hii kauli kwa namna fulani inashibahiana na hali inayomkuta sasa msanii Enock Bella

Huyu kijana kipindi yupo yamoto band aliwahi kutamba sana na sauti yake nzito na tungo tata zilizowachanganya vilivyo akina dada.

Mwanzoni huyu kijana alikuwa ni dancer tu wakawaida ila mkubwa fella akatumia kila aina ya ushawishi ili huyu jamaa naye aimbe kama wenzake kwenye kundi na akamsifia vilivyo kwamba sauti yake itaziba pengo la marehemu Muhiddin Gurumo lakini siku zote bwana mtu kama huna kipaji huna tu hata ufanye nini.

Alipokuwa Yamoto alijificha nyuma ya wenzake na kuimba maneno mawili matatu na hakuweza kugundulika kirahisi kwamba jamaa ni debe tupu ila tangu kundi livunjike huyu jamaa ana hali mbaya sana kimuziki na hilo limejidhihirisha mara baada ya kutoa wimbo kama solo artist uitwao Sauda.

Aisee huu wimbo ni mbaya mbaya mbayaa kupita maelezo hausikiliziki hauchezeki kwa kifupi hauvutii kabisa au kwa maneno mengine naweza kusema huu ndio wimbo mbovu zaidi kwa mwaka huu 2017/2018.

Jamaa bora aangalie tu ustaarabu mwengine mziki hawezi.

Huko IG watu wachache wamejitokeza kumsapoti lakini wapi ngoma haisapotiki ,imedoda.
Pole sana Enock Bela tafuta kazi nyingine tu huku kwenye mziki unatukera huna ulichobakiza.


Chuki zisizo kuwa na maana. Muda uliyotumia kumponda mwenzako bora ungefanya shughuli nyingine.
Wimbo upo vizuri mandhari mazuri na yavutia, sauti ipo pouwa kabisa...big up Enock. I hope kuna siku huyu mvivu wa kufikiri atakuja kukupigia magoti kukuombamsamaha kwa dharau hizi.
Kwann watanzania huwa hatupendi mafanikio ya wengine?.....Diamond mlimsema weee adi wengine wakaja na bandiko hapa kuwa anadhalilisha wanawake....ili Vodacom ivunje mkataba wake. Lakini wapi wamebaki kunamisha vichwa chini...mwenzao anakata masafa tu.
 
Kwakweli wimbo sio mzuri ila pia sio mbaya kiasi hicho kilichosemwa na mtoa mada.Kiufupi ni wa kawaida
 
Mimi nimeusikiza siyo mbaya kiasi ambacho mtoa mada kaongea eti wimbo mbaya kupata kutokea sasa utafananisha huo wimbo na lupela?
 
Amnaa kituu,,, WIMBO WA KAWAIDA WALA SIO MBOVU BWANAA ,,achen kupondea pondea watu jamn ,nakat mm nawewe ataa tungeambiwa kutunga verse mbil zakueleweka na saut hatuwezi
 
Umetumia mbinu nzuri ya kumtangaza dogo.

Ila mfahamu kujua kuimba na kuwa na mafanikio katika biashara ya mziki ni vitu viwili tofauti.
 
Hao wapumbavu walikua wanatembelea nyota ta Aslay sana aisee yanii dah ilikua inaniuma sana
 
Mtoa mada unasema wimbo hauchezeki lakini cha ajabu zaidi mwenye huo wimbo anaucheza bila shida yoyote!
 
Nimeona Leo kwenye comedy ya startv bakora wamempiga madongo sana huyo Bella.
 
JAMANI NYIE MJAMUELEWA MTOA MADA KAFANYA HIVYO ILA KUONGEZA VIEWS WA HIYO VIDEO YA ENOCK KWA WATU KUPITIA HIYO PROPAGANDA NA IMANI MTAKUA MMENIELEWA HII NI MOJA YA NJIA YA KUKUZA VIEWS WA WASANII ASILIMIA TUSINI MLIOKOMENTI HUMU MMEIWATCH SO AKTCHUARE MMEMUONGEZEA VIEWES KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE
 
Back
Top Bottom