Baadhi Wakenya wa Mombasa, jameni acheni ukaidi, mtanasa kwenye siasa za Tanzania kichwa kichwa

Naona wewe huwa unaiota Tanzania! Sijawahi ona unaanzisha thread ya Kenya kila mara TZ tu. Fanyakazi achana na Watz wewe nyang'au!!
 
unajua matokeo ya mgonjwa wa ukimwi akiishajijua ni mgonjwa?????

huo ni ukimwi ambao still mgonjwa ana nafasi ya kuishi,vipi corona ambayo kupona ni 10%???

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani wewe unasema mgonjwa wa corona kupona ni 10%?? Hesabu ulisoma kweli?? Yaani hao watu wanapona ni 10% tu kwa waathirika???!
 
Wapi huko Watanzania wanaishambulia Kenya? Mifano?
 
Ndio maana watu wanaogopa kwenda kufanya testing.
Your browser is not able to display this video.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msikize huyo.
Your browser is not able to display this video.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tangu lini Mombasa ikawa na undugu na tanga?

Sent using Jamii Forums mobile app

Wale ni ndugu bro, nawafahamu sana, kuna wabongo wa huko huko Tanga nimeishi nao na ilikua inanichukua nguvu nyingi sana kukosa kuamini wao sio watu wa Mambasani. Wanaachangia baadh ya makabila kama Wadigo vile.
Hii ndio sababu corona inapandisha sana Mombasa maana watu wa Tanga huingia tu.
 
Basi ungelinganisha hivyo pia makabila yote ambayo yapo mpakani, Mombasa haipo mpakani na tanzania,mtu kutoka tanga aje aishi Mombasa au atoke Mombasa aishi tanga haileti undugu wowote pale,huyu anabaki tu mkenya na yule anabaki tu mtanzania ,kwa taarifa yako Mombasa ni mchanganyiko wa makabila madogo ya kabila kubwa la kimijikenda Kama ni wadigo unazungumzia Basi hio itakua kwale county,tanga haina mchonyi,tanga haina mrabai,tanga haina mgiryama,tanga haina mribe wala mdhuruma Sasa huo undugu unatokea wapi ? Au kwa sababu ya wadigo wachache ambayo wapo Mombasa? Wadigo kwao ni kwale na hao ndio watu wa tanga.mombasa haina uhusiano wowote na tanga no muingiliano tu wa watu kipindi hichi kwa ajili ya mishe na Kama unazungumzia wagunya au hata bajuni Wana asili Yao sio tanga Kaka.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila siku tunawaambia kwamba Mombasa ni eneo la Tanzania lakini hamsikii!

Si mnaona binamu zetu tunavyo-match nao kila kitu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…