Baadhi Wakenya wa Mombasa, jameni acheni ukaidi, mtanasa kwenye siasa za Tanzania kichwa kichwa

Baadhi Wakenya wa Mombasa, jameni acheni ukaidi, mtanasa kwenye siasa za Tanzania kichwa kichwa

Basi ungelinganisha hivyo pia makabila yote ambayo yapo mpakani, Mombasa haipo mpakani na tanzania,mtu kutoka tanga aje aishi Mombasa au atoke Mombasa aishi tanga haileti undugu wowote pale,huyu anabaki tu mkenya na yule anabaki tu mtanzania ,kwa taarifa yako Mombasa ni mchanganyiko wa makabila madogo ya kabila kubwa la kimijikenda Kama ni wadigo unazungumzia Basi hio itakua kwale county,tanga haina mchonyi,tanga haina mrabai,tanga haina mgiryama,tanga haina mribe wala mdhuruma Sasa huo undugu unatokea wapi ? Au kwa sababu ya wadigo wachache ambayo wapo Mombasa? Wadigo kwao ni kwale na hao ndio watu wa tanga.mombasa haina uhusiano wowote na tanga no muingiliano tu wa watu kipindi hichi kwa ajili ya mishe na Kama unazungumzia wagunya au hata bajuni Wana asili Yao sio tanga Kaka.

Sent using Jamii Forums mobile app

Duh! Haya nimekubali yaishe maana niko mweupe sana kwenye mambo ya Wapwani, maana huwa nashindwa kutofautisha lafudhi zao hao watu wa huko, nimeishi Pemba, Unguja, pia Tanga, Mombasa, Malindi yaani kote huko nilikua nashindwa kutenganisha lafudhi zao, nilikua nawaona jamii moja wote, kuna Msambaa namfahamu tulifanya naye mradi fulani mwaka mzima, kila siku nilikua namuona kama mtu wa Mombasa kabisa, Kiswahili chake neno kwa neno yaani lafudhi ya Kimambasani.
 
"Wakennya sio kama Wabongo ambao kule kwao wakikaripiwa na mkulu wanaufyata wote mpaka hata Corona yenyewe inaingia mitini, kwa Wakenya ukiwajia kwa hasira ndio utakua unawapandisha full mzuka na utashindwa kuwatawala au kuwaelekeza."
Jamaa amekiri kwamba corona Tz imeingia mitini. Kuweni na imani mtashinda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lafudhi zao ni nyepesi Sana kutofautisha ,Kama wewe ni gwiji wa hii lugha au kiswahili chako sio Cha kubahatisha Basi huwezi ukaona ugumu wowote ,matamshi wa watu wa tanga , tanzania mkoa wa pwani ,dar haswa wale ambao sio wabara kiswahili Chao kinatesti flani hivi ,ukija Mombasa Mara nyingi wanatumia maneno asili ya kingozi ambayo watu wa tanga na Dar hawatumii.
Duh! Haya nimekubali yaishe maana niko mweupe sana kwenye mambo ya Wapwani, maana huwa nashindwa kutofautisha lafudhi zao hao watu wa huko, nimeishi Pemba, Unguja, pia Tanga, Mombasa, Malindi yaani kote huko nilikua nashindwa kutenganisha lafudhi zao, nilikua nawaona jamii moja wote, kuna Msambaa namfahamu tulifanya naye mradi fulani mwaka mzima, kila siku nilikua namuona kama mtu wa Mombasa kabisa, Kiswahili chake neno kwa neno yaani lafudhi ya Kimambasani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeona baadhi ya Wakenya wa Mombasa wakitishia kugoma kupimwa Corona na kutolea mifano ya Tanzania ambako matikiti maji, mapaipai n.k. zinapmwa na kukutwa na Corona.
Uzi huu ulikuwa mzuri kama ungeletwa kwa dhamira ya kutoa elimu. Lakini umeharibika kwa kuwa umeletwa kwa dhamira ya mipasho! Siku zote huwa namuambia huyu ndugu yangu
MK254 kuwa inawezekana ana points nzuri ila aangalie upya namna ya uwasilishaji wake
 
Lafudhi zao ni nyepesi Sana kutofautisha ,Kama wewe ni gwiji wa hii lugha au kiswahili chako sio Cha kubahatisha Basi huwezi ukaona ugumu wowote ,matamshi wa watu wa tanga , tanzania mkoa wa pwani ,dar haswa wale ambao sio wabara kiswahili Chao kinatesti flani hivi ,ukija Mombasa Mara nyingi wanatumia maneno asili ya kingozi ambayo watu wa tanga na Dar hawatumii.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mimi mzawa wa mikoani bana, Waswahili nimetangamana nao ukubwani, hivyo sina huo ujuzi au ufundi wa kutabainisha hizo lafudhi zao.
 
Akishajijua ni mgonjwa anawacha kusambaza, ni simple....naona kwenu hadi wabunge wameikimbia bunge, Makonda anawasaka kama machangudoa ili awarudishe bungeni kwa ulazima...
https://www.jamiiforums.com/data/attachment-files/2020/05/2390738__CoqjfLhVKKaluf7.mp4
hao ni wahuni tu,hivi eneo kama bungeni unaweza sema unaogopa kuambukizwa corona!!!!

mbali na kwamba ukumbi wa bunge wabunge hawabanani kabisa,lakini kwa aina ya watu wanaoingia humo lazima kuna jitihada za kuzuia ueneaji,pale sio kilabuni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha uboya ww yani mimi mchaga ningekuwa mkenya.. my foot
Wachagga wenyewe ni Wakenya na ndio maana wameshikilia uchumi wa Tanzania, isingekua kwa Ukenya wao, wangekua wzembe wa kutupwa kama wengine huko.
 
ona baadhi ya Wakenya wa Mombasa
Hili ndio lenu kuu,ubaguzi na ukabila
Kwani ukisema wakenya kuna tatizo gani mpaka uweke msisitizo wa mombasa
Naamini katiba yenu ya 1,000 pages inatoa uhuru kwa mkenya kuamini anachoona kinafaa
Umeumia sana kusikia wezako wanamsifu magufuli,wewe pia una haki ya kutetea mass tests lakini usikataze wenzio wasiamini vingine
Hiyo mass test utanipima leo nipo negative,narudi mtaani kesho naambukizwa itakuaje
Ndio maana kwa ujuha wenu mmekubali kuwa sehemu ya majaribio ya chanzo ili kufurahisha wazungu,kwani ulaya hakuna watu?
 
Sijaelewa nini kimekuumiza hapo maana kila taifa ina watu na asilia ya wanakotokea humo ndani, Tanzania hiyo hiyo sampuli na matokeo ya Wanzazibari hutajwa kama ya Watanzania wa Zanzibar, kwanza kwenu ndio huwa mkanganyiko maana kule Zenji huwa na takwimu zao pembeni na walikua wanazitoa kila siku wakati Watanganyika mumeghubikwa na usiri na uwoga.
 
Wangekuwa mbali kiuchumi kwa lipi walilo nalo?

Sent using Jamii Forums mobile app

Jaribuni kuwaskliza, maana hata wakoloni zama zile walikua wanauliza maswali unayoyauliza, kwamba tuwaache hawa Waafrika kwa lipi wanalo.
Huwa napitia nyuzi za Wazenji humu JF, hoja zao zina mashiko sana.
 
Back
Top Bottom