Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 378
- 766
Ni suala lililo wazi kuwa msanii Diamond Platnumz ndiye msanii anayeiwakilisha muziki wa Bongo Fleva kimataifa ambapo kupitia nyimbo zake Diamond ameweza kupenya na kujulikana katika mataifa mbalimbali ikiwemo Nigeria, Kenya, Ghana, Uganda na mataifa mengine mengi.
Kushinda tuzo kama MTV EMA za Ulaya, Headies za nchini Nigeria, Afrimma na nyinginezo nyingi ni ushahidi tosha kuwa Diamond Platnumz ni msanii wa kimataifa na moja kati ya vitu ambavyo vimepelekea Diamond Platnumz kujulikana kimataifa ni collabo zake ambapo msanii huyo amekuwa akishirikiana na wasanii wa, mataifa mengine.
Zifuatazo ni collabo 5 kali za kimataifa kutoka kwa Diamond Platnumz :
Komasava - Diamond ft Chley na Khalil Harrison (2024)
Yope Remix - Innos B ft Diamond (2019)
Diamond Platnumz alishirikiana na msanii Innos B kutokea nchini Congo. Yope Remix iliweza kuitambulisha vyema Bongo Fleva nchini Congo kiasi cha kuwa video ya muziki kutoka Tanzania ambayo imetazamwa zaidi Youtube kwani kufikia sasa imetazamwa mara Milioni 194 kwenye mtandao huo
African Beauty - Marion.(2017)
alimshirikisha Marion kutokea nchini Marekani ilikuwa na lengo la kumtambulisha Diamond Platnumz huko ughaibuni hasa Amerika ya Kaskazini. Wimbo huu ulipokelewa vyema sana kwani kiasi cha kushinda kipengele cha collaboration bora ya mwaka kwenye tuzo za AEUSA mwaka 2018.
My Number One Remix - Davido(2014)
Hii ni ngoma ambayo ilimtambulisha Diamond Platnumz na Bongo Fleva kwa ujumla kwenye medani za muziki wa Afrika. Kupitia ngoma hii, Diamond Platnumz alipata nafasi ya kutumbuiza kwenye jukwaa la kubwa la tuzo za MTV MAMA huko Afrika ya Kusini na pia alishinda tuzo mbalimbali kama Chanel O, tuzo za Hipipo na nyinginezo nyingi.
Hallelujah - Morgan Heritage ft Diamond.(2017)
Kwenye ngoma hii, Diamond Platnumz alishirikiana na kundi la Morgan Heritage. Namna ambavyo Bongo Fleva iliweza kujichanganya vyema na muziki wa Reggae kwenye ngoma hii ni kitu cha kupigiwa makofi. Ngoma hii iliweka rekodi mpya baada ya kufikisha watazamaji Milioni 1 ndani ya saa 15 tu na watazamaji Milioni 2 ndani ya siku mbili tu.
Ungependa Diamond afanye collabo na masanii gani wa nje?