- Source #1
- View Source #1
Nimekutana Na Chapisho Kwenye Mtandao Wa Facebook likielekeza Kuwa Dawa Ya Kufubuza Ukimwi ARV Inaweza Tumika Kutibu Ugonjwa Wa Homa ya Ini.Jamii check je Ukweli wa Hoja Hizo ni zipi.
Mfano Wa Chapisho Hilo Ni kama Unavyo onekana...
Sio kila anae tumia (ARV) Ni Muhathirika wa virus vya Ukimwi. "HAPANA"
Endapo utagundulika na Homa ya ini utatumia ARV vile vile...👇
Dawa kama Tenofovir au Lamivudine, ambazo mara nyingi hutumika kufubaza VVU, Hutumika pia kutibu Homa ya Ini (Hepatitis B)....
Hii ni kwa sababu dawa hizi huzuia virusi vya Hepatitis B kujizidisha mwilini, hivyo kulinda ini lisiharibiwe zaidi...
Homa ya ini ni hatari kwani huambukizwa hata kwa njia ya jasho kwa kugusana Tu...☠️
PIMA: Hepatitis B, Pata chanjo dhidi ya Homa ya ini kwa afya yako sasa..
...….......................

- Tunachokijua
- Madai
Kumekuwa na taarifa zinazodai kuwa baaadhi ya dawa zinzotumika kufubaza maambukizi wa ya virusi vya UKIMWI kitaalamu zikijulikana kama Antiretroviral (ARV) z.
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia na kujirirdhisha kuwa madai ya kuwa baadhi ya dawa zinzotumika kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI zinaweza kutumika pia kama dawa za kufubaza ugunjwa wa homa ya ini.
Kupitia tafiti na machapisho mbalimbali ya kitaalamu kwenye kuhusu afya ambayo yanataja baadhi ya dawa zinazotumika kufubaza homa ya ini ambazo ndizo hizo hutumika katika kufubaza virusi vya UKIMWI.
Ingawa aina ya homa ya ini inayotajwa zaidi kuwa inaweza kufubazwa na miongoni mwa dawa zinazotumika kufubaza UKIMWI ni Hepatitis B.
Tovuti ya Mayo Clinic inabainisha kuwa Hepatitis B inasabaishwa pale ambapo unakutana na virusi hivyo kwa njia mbalimbali ikiwemo kushiriki tendo la ngono, kuchangia sindano za dawa za kulevya, kuchomwa sindano yeneye virusi au kupata huduma ya kusafishwa damu.
Hepatitis B (HBV) huenea kupitia damu na majimaji ya mwilini kama mate, shahawa, na majimaji ya uke. Mjamzito mwenye HBV anaweza kumwambukiza mtoto wakati wa kujifungua. Kwa nadra, mtu anaweza kupata hepatitis B kwa kushiriki vifaa binafsi kama vile wembe au mswaki.