Baadhi ya dhambi zinazoweza kukufanya kuwahishwa ahera ukiwa China

Baadhi ya dhambi zinazoweza kukufanya kuwahishwa ahera ukiwa China

Dr Ahmed Albah-Shahwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2022
Posts
848
Reaction score
1,604
Nchini China, baadhi ya makosa ya jinai yanayostahiki adhabu ya kifo na marejeleo ni kama ifuatavyo:

1. Usaliti wa Nchi (Kifungu cha 102)

3. Kushirikiana na adui na usaliti (Kifungu cha 108)

4. Upelelezi au ujasusi (Kifungu cha 110)

5. Kuiba, kupeleleza, kununua na kutoa siri za serikali na ujasusi nje ya nchi kinyume cha sheria (Kifungu cha 111)

7. Uchomaji moto (Kifungu cha 115)

8. Mafuriko (Kifungu cha 115)

9. Mlipuko (Kifungu cha 115)

10. Kueneza vitu vyenye hatari (Kifungu cha 115)

11. Kuhatarisha usalama wa umma kwa njia hatari (Kifungu cha 115)

12. Uharibifu wa magari (Kifungu cha 119)

13. Uharibifu wa vyombo vya usafiri (Kifungu cha 119)

14. Uharibifu wa vifaa vya umeme (Kifungu cha 119)

20. Uzalishaji na uuzaji wa dawa ghushi (Kifungu cha 141)

21. Mauaji ya kukusudia (Kifungu cha 232)

22. Kuumia kwa kukusudia (Kifungu cha 234)

23. Ubakaji (Kifungu cha 236)

24. Utekaji nyara (Kifungu cha 239)

25. Usafirishaji haramu wa wanawake na watoto (Kifungu cha 240)

26. Wizi (Kifungu cha 263)

29. Kusafirisha, kuuza, kutengeneza madawa ya kulevya (Kifungu cha 347)

32. Rushwa (Kifungu cha 382, 383)

36. Kujisalimisha (Kifungu cha 423)

37. Kutoroka wakati wa vita (Kifungu cha 424)

38. Kuasi askari (Kifungu cha 430)
 
No 36;- kujisalimisha kwa adui (kwa vyombo vyao vya ulinzi na usalama)

Asante kwa kutujuza, weka vizuri maelezo ili usituache njiani
 
No 36;- kujisalimisha kwa adui (kwa vyombo vyao vya ulinzi na usalama)

Asante kwa kutujuza,weka vizuri maelezo ili usituache njiani
Yaani mko vitani we ndio mwanajeshi ukazidiwa/kwa kupenda ukithubutu kujisalimisha unawaachia ngome/eneo, silaha maadui na wewe mwenyewe unakuwa mateka au umesaini mapatano ya amani wao China wakikudaka ni kifo.
 
Wao china hawaafiki makubaliano ya kimataifa kukomesha adhabu ya kifo?
 
Wao china hawaafiki makubaliano ya kimataifa kukomesha adhabu ya kifo?
Swala la kukomesha adhabu ya kifo kwa nchi kama China hata kama litakuja kutekelezwa litachukua muda kwani huo usiriazinesi ndio ulioifanya ifikie hapo ilipo.
 
Back
Top Bottom